Eliphaz the Temanite
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 3,018
- 1,151
kufugia kijijini na kuuza mjini katika mkoa mmoja sio tatizo pia ni kurahisisha gharama ila kazi ngumu kuwasafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine nasikia kuna vibali na usumbufu unaoweza kukusababishia kuwaweka muda mrefu njiani ktk mazingira magumu na hatari ya kuambukizana magonjwa. Ulizia kuna vibali vya mifugo pia vibali kuwa wamepewa chanjo still roadblocks. Ila kama unauza mkoa huo huo inakuwa poa. Soko la kuku kienyeji pure ni grocery baadhi ya baa na hotel na watu binafsi mfano unawapa taarifa unapark gari na kuku wazima wananunua jioni au unachinja na kuuza supermarket au kwa oda. Ushauri mjini itabidi uwe na kwa kuwatunzia wakati ukichinja au kutafuta soko maana huwezi uza wote kwa siku moja
Thanks unaweza google RIU uone wanavyofanya haina tofauti na unachotaka kufanya. Kikubwa ujue soko lako ni lipi watakufuata shamba, utawapelekea wazima, utawapeleka waliochinjwa fresh au frozen kasha utajua jinsi gani uwasafirishe toka shamba hadi mjini.Thank you Mama Joe
Hello Wana Forum Habarini za Asubuhi
Nafikiri kuanzisha Mradi wa kuuza kuku wa Kienyeji ambao nitawafuga kijijini na kisha kuwaleta hapa jijini Dar! Ningependa mtu mwenye uzoefu na biashara hii tubadilishane uzoefu, Do's and Don'ts
Masoko yanatafutwaje, Worst case scenarios....! Profit margin nk...nk...
Nafahamu hapa ni kisima cha Maarifa and I hope nitapata mawazo mazuri ya kuendeleza shughuli hiii!
Thanks unaweza google RIU uone wanavyofanya haina tofauti na unachotaka kufanya. Kikubwa ujue soko lako ni lipi watakufuata shamba, utawapelekea wazima, utawapeleka waliochinjwa fresh au frozen kasha utajua jinsi gani uwasafirishe toka shamba hadi mjini.
safi matu kama nyny ndo mnatakiwa ktk mataifa ,sna la kukuambia zaid ya Mungu kukuongoza ktk mrad unaotaka udevelope
kazi kwako!
UTUNZAJI WA VIFARANGA-KUKU WA ASILI/KIENYEJI NA WA MAYAI USHAURI BINAFSI
(1) Utunzaji wa vifaranga
(2) Utaratibu wa chanjo
- Siku ya kwanza. (1) Waweke katika brooder wape glucose kwa masa 6 hadi 8 ya kwanza kurudisha nguvu iliyopotea
- Siku hiyo hiyo ya kwanza baada ya kuwapa glucose wape Esb3 au S-dime au Amprolium kwa siku ya 1 hadi 3
- Siku ya 3 hadi 5 wape Chick formula
- Siku ya sita wape maji peke yake (plain water)
- Siku ya saba wape NCD Vaccine (New Castle) kwa muda wa masaa mawili tu, kisha wape maji yenye vitamins.
- Siku ya 10 wape chanjo ya gumboro
- Siku ya 13 wape Typhoprim na Neoxyvital kwa muda wa siku saba (7) baadaye wape vitamin/dawa hizi kila mwezi siku tatu (3)
- Siku ya saba (7) wape New Castle Vaccine
- Siku ya kumi (10) wape chanjo ya Gumboro
- Siki ya ishirini na moja (21) rudia kuwapa chanjo ya Gumboro
(3)Minyoo
- Siku ya arobaini na mbili (42) rudia chanjo ya New Castle, kisha rudia kila baada ya miezi mitatu
- wiki ya kumi (10) hadi kumi na mbili (12) wapate chanjo ya ndui (Fowl pox)
Wape dawa ya minyoo kuku wako wanapofikia umri wa wiki 8 na rudia kila baada ya miezi mitatu
(4) Magonjwa
UpatikajiVifaranga wa kuku wa asili/ kienyeji
- Chunguza tabia ya kuku kama wanakula vizuri, wanakunywa maji ya kutosha, wanatembea vizuri na kuchangamka. Sikiliza sauti zao, angalia mwenendo wa ukuaji wa kuku wako na mwenendo wa utagaji. Angalia kila siku kama kuna vifo vimetokea bandani
- Ukiona mabadiliko yasiyo ya kawaida mwone mtaalamu wa mifugo aliye jirani na wewe kama hayuko bwana/bibi mifugo jirani yako piga simu kwa bwana Mtera 0716 612 858 (Tigo) , 0784 334 730 (Zain) na 0753 280 648 (Voda)
Wanapatikana Mbezi Msigani -Zoni (off Morogoro Road) simu 0784 646 381(Zain) au 0655 646 381(Tigo)au 0767-646 381 (Voda)Bwana Mrindwa au simu 0784 824 846 (Zain) au 0715 824 846 (Tigo), au 0767-824 846 (Voda) kwa mama Mrindwa. Simu ya mezani 022- 2420502
May 2010 -Dar es salaam
kama kwa train hapo poa maana hizi roadblocks na vibali ndo vinatukwamisha sana watu kutanuka tunabanana mjini wakati ni gharama sana. All the bestMama Joe! Nakushukuru sana umekuwa msaada mkubwa! Changamoto kubwa ni kuwa eneo ninalotaka kuanzisha mradi liko mbali nitapaswa kuwasafirisha, Uzuri wake ni kuwa nitasafirisha kwa njia ya train nadhani usumbufu hautakuwa mkubwa sana!
pamoja na kuwa mbali dunia ni kijiji sasaivi kutokana na emails na simu waweza fanya biashara toka huko uliko ukaja na idadi yako kamili mradi uwe umeishapata soko la uhakika. Pia waweza fanya kwa kutumia soko la mwingine sijui ni outsourcing incase yeye wake bado au hana kwa wakati huo. Tatizo wakulima wengi hatuna umoja hivyo tunashindwa kushika masoko makubwa ya mahoteli na supermarket maana once ukiambiwa uwe unaleta kuku say 500 kwa siku utaishia kupotea maana ni impossible wakati kwa umoja tungeweza shika soko na leo akileta Kubota kesho Neggir, Elifaz etc soko linakuwa maintained wanachofanya RIU hao wakenya ni kuwakusanya kuku huko mashambani na kuwauza huku mjini. Sio lazima umoja ila walau mawasiliano nadhani tunahitaji kitu kama network na standardized format ya aina ya mazao yanayohitajika kwa mwezi sijui ninaeleweka?
Thanks yaani tunatakiwa tufike hapo ndipo tutajikwamuaUmeeleweka sana, sio muda mrefu tutafikia hapo.
Thanks yaani tunatakiwa tufike hapo ndipo tutajikwamua
pamoja na kuwa mbali dunia ni kijiji sasaivi kutokana na emails na simu waweza fanya biashara toka huko uliko ukaja na idadi yako kamili mradi uwe umeishapata soko la uhakika. Pia waweza fanya kwa kutumia soko la mwingine sijui ni outsourcing incase yeye wake bado au hana kwa wakati huo. Tatizo wakulima wengi hatuna umoja hivyo tunashindwa kushika masoko makubwa ya mahoteli na supermarket maana once ukiambiwa uwe unaleta kuku say 500 kwa siku utaishia kupotea maana ni impossible wakati kwa umoja tungeweza shika soko na leo akileta Kubota kesho Neggir, Elifaz etc soko linakuwa maintained wanachofanya RIU hao wakenya ni kuwakusanya kuku huko mashambani na kuwauza huku mjini. Sio lazima umoja ila walau mawasiliano nadhani tunahitaji kitu kama network na standardized format ya aina ya mazao yanayohitajika kwa mwezi sijui ninaeleweka?
Tuanze mimi na wewe na wengine watafuata, hatimaye timu/network itakamilika.