Mradi wa Kuku wa Kienyeji

Mradi wa Kuku wa Kienyeji

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Posts
3,018
Reaction score
1,151
Hello Wana Forum Habarini za Asubuhi
Nafikiri kuanzisha Mradi wa kuuza kuku wa Kienyeji ambao nitawafuga kijijini na kisha kuwaleta hapa jijini Dar! Ningependa mtu mwenye uzoefu na biashara hii tubadilishane uzoefu, Do's and Don'ts
Masoko yanatafutwaje, Worst case scenarios....! Profit margin nk...nk...

Nafahamu hapa ni kisima cha Maarifa and I hope nitapata mawazo mazuri ya kuendeleza shughuli hiii!
 
Wao....... Wao kijiwe kimenuna........!
Ngoja nimtafute kubota Mie!!! Hata Consultancy tu...!!
 
kufugia kijijini na kuuza mjini katika mkoa mmoja sio tatizo pia ni kurahisisha gharama ila kazi ngumu kuwasafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine nasikia kuna vibali na usumbufu unaoweza kukusababishia kuwaweka muda mrefu njiani ktk mazingira magumu na hatari ya kuambukizana magonjwa. Ulizia kuna vibali vya mifugo pia vibali kuwa wamepewa chanjo still roadblocks. Ila kama unauza mkoa huo huo inakuwa poa. Soko la kuku kienyeji pure ni grocery baadhi ya baa na hotel na watu binafsi mfano unawapa taarifa unapark gari na kuku wazima wananunua jioni au unachinja na kuuza supermarket au kwa oda. Ushauri mjini itabidi uwe na kwa kuwatunzia wakati ukichinja au kutafuta soko maana huwezi uza wote kwa siku moja
 
Thank you Mama Joe
 
Thank you Mama Joe
Thanks unaweza google RIU uone wanavyofanya haina tofauti na unachotaka kufanya. Kikubwa ujue soko lako ni lipi watakufuata shamba, utawapelekea wazima, utawapeleka waliochinjwa fresh au frozen kasha utajua jinsi gani uwasafirishe toka shamba hadi mjini.
 
Hello Wana Forum Habarini za Asubuhi
Nafikiri kuanzisha Mradi wa kuuza kuku wa Kienyeji ambao nitawafuga kijijini na kisha kuwaleta hapa jijini Dar! Ningependa mtu mwenye uzoefu na biashara hii tubadilishane uzoefu, Do's and Don'ts
Masoko yanatafutwaje, Worst case scenarios....! Profit margin nk...nk...

Nafahamu hapa ni kisima cha Maarifa and I hope nitapata mawazo mazuri ya kuendeleza shughuli hiii!

safi matu kama nyny ndo mnatakiwa ktk mataifa ,sna la kukuambia zaid ya Mungu kukuongoza ktk mrad unaotaka udevelope
 
kazi kwako!

UTUNZAJI WA VIFARANGA-KUKU WA ASILI/KIENYEJI NA WA MAYAI USHAURI BINAFSI

(1) Utunzaji wa vifaranga

  • Siku ya kwanza. (1) Waweke katika brooder wape glucose kwa masa 6 hadi 8 ya kwanza kurudisha nguvu iliyopotea
  • Siku hiyo hiyo ya kwanza baada ya kuwapa glucose wape Esb3 au S-dime au Amprolium kwa siku ya 1 hadi 3
  • Siku ya 3 hadi 5 wape Chick formula
  • Siku ya sita wape maji peke yake (plain water)
  • Siku ya saba wape NCD Vaccine (New Castle) kwa muda wa masaa mawili tu, kisha wape maji yenye vitamins.
  • Siku ya 10 wape chanjo ya gumboro
  • Siku ya 13 wape Typhoprim na Neoxyvital kwa muda wa siku saba (7) baadaye wape vitamin/dawa hizi kila mwezi siku tatu (3)
(2) Utaratibu wa chanjo

  • Siku ya saba (7) wape New Castle Vaccine
  • Siku ya kumi (10) wape chanjo ya Gumboro

  • Siki ya ishirini na moja (21) rudia kuwapa chanjo ya Gumboro

  • Siku ya arobaini na mbili (42) rudia chanjo ya New Castle, kisha rudia kila baada ya miezi mitatu
  • wiki ya kumi (10) hadi kumi na mbili (12) wapate chanjo ya ndui (Fowl pox)
(3)Minyoo
Wape dawa ya minyoo kuku wako wanapofikia umri wa wiki 8 na rudia kila baada ya miezi mitatu
(4) Magonjwa

  • Chunguza tabia ya kuku kama wanakula vizuri, wanakunywa maji ya kutosha, wanatembea vizuri na kuchangamka. Sikiliza sauti zao, angalia mwenendo wa ukuaji wa kuku wako na mwenendo wa utagaji. Angalia kila siku kama kuna vifo vimetokea bandani
  • Ukiona mabadiliko yasiyo ya kawaida mwone mtaalamu wa mifugo aliye jirani na wewe kama hayuko bwana/bibi mifugo jirani yako piga simu kwa bwana Mtera 0716 612 858 (Tigo) , 0784 334 730 (Zain) na 0753 280 648 (Voda)
UpatikajiVifaranga wa kuku wa asili/ kienyeji
Wanapatikana Mbezi Msigani -Zoni (off Morogoro Road) simu 0784 646 381(Zain) au 0655 646 381(Tigo)au 0767—646 381 (Voda)Bwana Mrindwa au simu 0784 824 846 (Zain) au 0715 824 846 (Tigo), au 0767-824 846 (Voda) kwa mama Mrindwa. Simu ya mezani 022- 2420502
May 2010 -Dar es salaam
 
Thanks unaweza google RIU uone wanavyofanya haina tofauti na unachotaka kufanya. Kikubwa ujue soko lako ni lipi watakufuata shamba, utawapelekea wazima, utawapeleka waliochinjwa fresh au frozen kasha utajua jinsi gani uwasafirishe toka shamba hadi mjini.

Mama Joe! Nakushukuru sana umekuwa msaada mkubwa! Changamoto kubwa ni kuwa eneo ninalotaka kuanzisha mradi liko mbali nitapaswa kuwasafirisha, Uzuri wake ni kuwa nitasafirisha kwa njia ya train nadhani usumbufu hautakuwa mkubwa sana!
 
safi matu kama nyny ndo mnatakiwa ktk mataifa ,sna la kukuambia zaid ya Mungu kukuongoza ktk mrad unaotaka udevelope

Nashukuru kwa maombi yako Mkuu, Mungu hupendezwa na wale wanaombea wengine Ubarikiwe na wewe katika shughuli zako
 
kazi kwako!

UTUNZAJI WA VIFARANGA-KUKU WA ASILI/KIENYEJI NA WA MAYAI USHAURI BINAFSI

(1) Utunzaji wa vifaranga

  • Siku ya kwanza. (1) Waweke katika brooder wape glucose kwa masa 6 hadi 8 ya kwanza kurudisha nguvu iliyopotea
  • Siku hiyo hiyo ya kwanza baada ya kuwapa glucose wape Esb3 au S-dime au Amprolium kwa siku ya 1 hadi 3
  • Siku ya 3 hadi 5 wape Chick formula
  • Siku ya sita wape maji peke yake (plain water)
  • Siku ya saba wape NCD Vaccine (New Castle) kwa muda wa masaa mawili tu, kisha wape maji yenye vitamins.
  • Siku ya 10 wape chanjo ya gumboro
  • Siku ya 13 wape Typhoprim na Neoxyvital kwa muda wa siku saba (7) baadaye wape vitamin/dawa hizi kila mwezi siku tatu (3)
(2) Utaratibu wa chanjo

  • Siku ya saba (7) wape New Castle Vaccine
  • Siku ya kumi (10) wape chanjo ya Gumboro

  • Siki ya ishirini na moja (21) rudia kuwapa chanjo ya Gumboro

  • Siku ya arobaini na mbili (42) rudia chanjo ya New Castle, kisha rudia kila baada ya miezi mitatu
  • wiki ya kumi (10) hadi kumi na mbili (12) wapate chanjo ya ndui (Fowl pox)
(3)Minyoo
Wape dawa ya minyoo kuku wako wanapofikia umri wa wiki 8 na rudia kila baada ya miezi mitatu
(4) Magonjwa

  • Chunguza tabia ya kuku kama wanakula vizuri, wanakunywa maji ya kutosha, wanatembea vizuri na kuchangamka. Sikiliza sauti zao, angalia mwenendo wa ukuaji wa kuku wako na mwenendo wa utagaji. Angalia kila siku kama kuna vifo vimetokea bandani
  • Ukiona mabadiliko yasiyo ya kawaida mwone mtaalamu wa mifugo aliye jirani na wewe kama hayuko bwana/bibi mifugo jirani yako piga simu kwa bwana Mtera 0716 612 858 (Tigo) , 0784 334 730 (Zain) na 0753 280 648 (Voda)
UpatikajiVifaranga wa kuku wa asili/ kienyeji
Wanapatikana Mbezi Msigani -Zoni (off Morogoro Road) simu 0784 646 381(Zain) au 0655 646 381(Tigo)au 0767-646 381 (Voda)Bwana Mrindwa au simu 0784 824 846 (Zain) au 0715 824 846 (Tigo), au 0767-824 846 (Voda) kwa mama Mrindwa. Simu ya mezani 022- 2420502
May 2010 -Dar es salaam

Haya ndio maujanja yaani hapa na copy and paste!!!! Natengeneza doc moja yenye combination ya uzoefu na technical expertise
 
Mama Joe! Nakushukuru sana umekuwa msaada mkubwa! Changamoto kubwa ni kuwa eneo ninalotaka kuanzisha mradi liko mbali nitapaswa kuwasafirisha, Uzuri wake ni kuwa nitasafirisha kwa njia ya train nadhani usumbufu hautakuwa mkubwa sana!
kama kwa train hapo poa maana hizi roadblocks na vibali ndo vinatukwamisha sana watu kutanuka tunabanana mjini wakati ni gharama sana. All the best
 
pamoja na kuwa mbali dunia ni kijiji sasaivi kutokana na emails na simu waweza fanya biashara toka huko uliko ukaja na idadi yako kamili mradi uwe umeishapata soko la uhakika. Pia waweza fanya kwa kutumia soko la mwingine sijui ni outsourcing incase yeye wake bado au hana kwa wakati huo. Tatizo wakulima wengi hatuna umoja hivyo tunashindwa kushika masoko makubwa ya mahoteli na supermarket maana once ukiambiwa uwe unaleta kuku say 500 kwa siku utaishia kupotea maana ni impossible wakati kwa umoja tungeweza shika soko na leo akileta Kubota kesho Neggir, Elifaz etc soko linakuwa maintained wanachofanya RIU hao wakenya ni kuwakusanya kuku huko mashambani na kuwauza huku mjini. Sio lazima umoja ila walau mawasiliano nadhani tunahitaji kitu kama network na standardized format ya aina ya mazao yanayohitajika kwa mwezi sijui ninaeleweka?
 
Umeeleweka sana, sio muda mrefu tutafikia hapo.
 
Jambo moja umesema, networking! ubadilishanaji mawazo na uzoefu! Ni muhimu sana kwenye biashara! Through umoja tuna create more markets, badala ya wageni kuja kuchukua soko simply because wajasiliamali wetu watuwezi ku meet demand inasikitisha sana!
Im so excited, hii kitu nitaianza, najua nitakutana na changamoto hapa na pale, yatakayo nisubu nita share na wana forum, Lakini finally nadhani ipo haja ya ku strengthen ushirikiano katika nyanja hizi
Waswahili wanasema "Ngege wenye manyoya ya kufanana huruka pamoja"
 
sure Malila we need to be an example by leading tusiishie kuongea tu. Unajua ktk ufugaji East Africa anasikika Muguku lakini ilikuwa rahisi kwake kwasababu kuku wa kisasa tayari wako in standardized format ukimwambia mtu ni wa wiki ya 6, 7 anapata picha huyo ni uzito gani kwa hiyo alipata mteremko kwenye soko hata nyenzo kama incubator etc. lakini pia kuna Shalom Organic Farm ya mwanamama wa Uganda aliyeweza ku fight hadi kuweza kuuza kuku wake Shoprites na mahotel na kumaintain soko karibia kuku 5000 kwa wiki am not sure.... hii ilibidi awatrain wakulima wengine ili wapate kulishika soko. Yeye ni pure organic mayai na kuku. Kwahiyo tukiitengeneza network ni rahisi sana kulishika soko.
Tuanze mimi na wewe na wengine watafuata, hatimaye timu/network itakamilika.
 
Back
Top Bottom