pamoja na kuwa mbali dunia ni kijiji sasaivi kutokana na emails na simu waweza fanya biashara toka huko uliko ukaja na idadi yako kamili mradi uwe umeishapata soko la uhakika. Pia waweza fanya kwa kutumia soko la mwingine sijui ni outsourcing incase yeye wake bado au hana kwa wakati huo. Tatizo wakulima wengi hatuna umoja hivyo tunashindwa kushika masoko makubwa ya mahoteli na supermarket maana once ukiambiwa uwe unaleta kuku say 500 kwa siku utaishia kupotea maana ni impossible wakati kwa umoja tungeweza shika soko na leo akileta Kubota kesho Neggir, Elifaz etc soko linakuwa maintained wanachofanya RIU hao wakenya ni kuwakusanya kuku huko mashambani na kuwauza huku mjini. Sio lazima umoja ila walau mawasiliano nadhani tunahitaji kitu kama network na standardized format ya aina ya mazao yanayohitajika kwa mwezi sijui ninaeleweka?
Kuna jamaa yangu alikuwa amepata soko la kuuza kuku wakienyeji saba tu kwa siku kwenye hotel moja, alishindwa aliuza kwa mwezi mmoja tu kuku wakaisha bandani kwake, akawa ananunua kwa watu wengine akawa hapati anaowahitaji na kwa uhakika na kununua sokoni ikawa haimlipi sana kutokana na bei ya manunuzi na mtaji wake kuwa ni kidogo. network ni nzuri sana kama unavyosema mama Joe.