Mradi wa mabasi maalumu kwa wanafunzi chini ya DART

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Kwa muda mrefu, wazazi wamekuwa wakiamka na presha za usafiri wa watoto wao—wakati mwingine mtoto anaondoka nyumbani akiwa na matumaini, anarudi na hadithi ya huzuni tupu.

Hata hivyo, nyuma ya pongezi kuna maswali mazito yanayohitaji majibu ya wazi. Kwanza ni suala la usalama ndani ya mabasi. Mabasi haya yanabeba watoto wa rika na jinsia tofauti, je, kuna mifumo madhubuti ya kuwalinda dhidi ya unyanyasaji? Tusije tukatengeneza basi la wanafunzi lakini tukasahau kuweka suala la “maadili.” Vipi kuhusu vijana wajanja watakaovaa sare za shule kama “uniform”?

Pili, msongamano wa asubuhi—hii siyo siri, Dar saa moja asubuhi ni fujo mtindo mmoja. Je, mabasi yatatosha au watoto wataendelea kujifunza somo la “kusimama bila kushika”? Au kubanana ili mlango ufunge?

Na mwisho, iwapo basi litapata hitilafu, kuna mpango gani mbadala? Tusije tukawaacha watoto njiani wakijifunza jiografia kwa miguu pamoja na historia ya Tanzania na Maadili kwa macho.

Ni muhimu pia kukumbuka: huu ni mradi wa wananchi. Heshima iende kwa walipa kodi—maana bila wao, hata basi lenye AC lingebaki kwenye ndoto. Msianze kuleta porojo za Rais Samia utadhani yeye ndio katoa pesa zake mfukoni.
 
Nadhani Wanafanya Pilot study.
Acha tuone itakuaje, Ila Kwa hili Wanastairi PONGEZI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…