Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

Hivi changamoto ni mradi haufai au changamoto ni uendeshaji mbovu wa mradi?kwenye mwendokasi umesema vyema,abiria wapo wakutosha,Shida nini?nadhani itafutwe dawa ya usimamizi na uendeshaji mzuri wa hii miradi na sio kusema haifai kabisa
 
Unamaanisha hakuna nchi ambako serikali zimefanikiwa kuendesha miradi kama hii ya reli au ndege?hivi Fly Emirates ni Kampuni binafsi,au ya Serikali?Ethiopia Airline je?tutafute tiba ya kuhakikisha haya mashirika na hii miradi inaendeshwa kwa ufanisi na sio kulalamika tu
 
Kaka hoja yako Inawelekeo chanya Sana ila umeiwasilisha kinadharia Sana, no data, no cross reference! Kwa hiyo inabakia kuelea kama fiction!
 
Ni kweli serikali haiwezi kufanya biashara, lakini biashara zote kubwa zilianza kidogokidogo, makampuni mengine yalianza karne ya 18. Yakaendelea kukua kwa kufuatia uendelevu wa teknologia. Kwa sasa ni nani angeweza kujenga reli ya mwendo kasi au bwawa la Nyerere au miradi mikubwa inayofanyika sasa? Hao wawekezaji walikuwa hawaoni fursa hizo? Hiyo miradi kwa gahrama zake hakuna budi serikali ifanye. Inafanya hivi kwa kodi zetu kwa kutuhudumia sisi wenyewe. Faida ipo ila ni Indirect, na kama walivyosema wengine hizo ni huduma kwa wananchi. Hebu nenda vijijini uone wananchi wanavyofaidika na huduma za umeme. Isingewezekana umeme kutoka Njombe, Songea mpaka Mtwara ujengwe kwa kutegemea faida, hicho kitu hakingewezekana milele, Mtanzania gani angeweza kulipia? Tuliona huko nyuma gharama halisi ya kuingiza umeme nyumbani ilikuwa ni zaidi ya laki sita, huko vijijini wangeweza? Tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha miradi hii baada ya kukamilika ijiendeshe yenyewe. Tuendelee kulipa kodi ili Watanzania wenzetu wafaidike, sisi tunaoongea sana tuko mijini hatujui maisha ya tabu wanayoyapata wenzetu vijijini.
 
Biashara ya malori itakuwepo tu kwani wenye bidhaa wataangalia na gharama nyingine za usafirishaji. Reli haifiki kila eneo lakini malori yanafikisha mzigo mpaka mlangoni. Hata abiria vile vile. Kama unakwenda Chalinze kutoka Morogoro, utapanda treni ya mwendo kasi au utapanda basi? Sasa hivi mabasi mengi hayachukui abiria wanaoshukia njiani vinginevyo ulipe nauli ya mpaka mwisho wa safari, ikiwepo reli ya mwendo kasi hii kero itaondoka tu.
 
Bado sijapata jibu hivi ni kwa nini SGR isingeanzia Pugu...kulikuwa na haja gani kujenga daraja la juu namna hii kwanza kuokoa gharama pia nafasi (msomgamano) katikati ya jiji.
 
Tujenge reli ya kawaida katika vipande vilivyobaki
 
Watakuja kukuelewa tu
 
Bado sijapata jibu hivi ni kwa nini SGR isingeanzia Pugu...kulikuwa na haja gani kujenga daraja la juu namna hii kwanza kuokoa gharama pia nafasi (msomgamano) katikati ya jiji.
Huu mradi hautaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…