Uchumi wa China ulianza kukua kwa kasi miaka ya 1980 baada ya kufunguliwa na kuruhusu sekta binafsi kushamiri chini ya Deng Xiaoping, hii China yenye uchumi mkubwa unayoina leo ni matokeo ya Sekta binafsi kuruhusiwa kuchukua hatamu japo kwa kuendelea kubanwa na sera za kikomunisti. Kwa sasa viwanda na makampuni mengi China yanamilikiwa na watu binafsi au umma kupitia mfumo wa hisa.
Russia ilishatoka kwa kiasi kikubwa kwenye mfumo wa serikali kufanya biashara,ilifanya ubinafsihaji mkubwa wa makampuni ya umma miaka ya 1990 chini ya Boris Yeltsin na imeenda mbali sana kwenye sekta binafsi.
Fahamu pia kuna nchi nyingi zina utajiri mkubwa kiasi kwamba kuna mambo ya kibiashara zinafanya bila dhana ya biashara, Hizo ni pamoja na Russia, Saudi Arabia, Qatar n.k.Hizi ni nchi ambazo zitajenga na kuendesha miradi ya reli, mwendokasi, mashirika ya ndege bila kujali upatikanaji wa faida yoyote, zina huo uwezo, sisi hatuna.
North Korea ni shit hole country haifai hata kuzungumziwa.