Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

Umeandika jambo kubwa lakini bila vielelezo na uthibitisho mfano umeandika serikali inatoa fedha kwenye mradi wa mwendokasi ilitakiwa useme inatoa kiasi gani na mradi unapata hasara kiasi gani na kwanini unashindwa kujiendesha.Umeandika kuhusu SGR lakini sijaona facts kuthibitisha mradi utashindwa.
Hakuna mradi ulioendeshwa na Serikali ukafanikiwa. Sio kampuni za simu, posta, Tanesco. Reli ya Kati na Tazara. Sijui unataka mfano gani. Juzi mkaguzi mkuu alitangaza hasara ya bilion zaidi ya 90 kila mwaka kwenye Air Tz Sasa unategemea miujiza ipi?!
 
Mwaka 1970-1974 mchina alijenga reli ya Tazara ya kisasa kwa wakati huo na watanzania waliaminishwa makubwa Sana juu ya faida ya mradi husika. Miaka 25 tu baada ya mradi kukamilika reli ikachoka, ikakosa wateja, usimamizi mbovu. Zile hadithi na simulizi tamu za manufaa ya mradi huo walioaminishwa watanzania hakuna Tena na njia kuu ya uchukuzi Tanzania to Zambia kubaki NI barabara ya Rami.

Pia Serikali ililithi reli ya Kati kutoka kwa mkoloni. Na reli ilibaki njia kuu ya uchukuzi Hadi miaka ya 90s katikati. Lakini shirika liliendeshwa kihuni Sana. Shirika liliuza tiketi chache Sana. Zaidi ya 80% ya abilia walilipa Ela keshi zilizoishia mikononi mwa walinzi na wafanyakazi wa shirika lenyewe.

Mpaka leo reli haikujiendesha. Inakula Kodi zetu kila siku kukarabatiwa lkn maingizo hakuna NI hasara tu.
Nisiwachoshe kabisa. Sizungumzii kbs mradi wa Mabasi ya mwendokasi unavyoumiza taifa ikiwa NI chini ya miaka kumi tu uanshwe. Serikali inamwaga fedha kuuokoa Ila watachoka tu. Mabasi kibao yameharibika yakatelekezwa na kuoza.
Ndege zipo kwaajili ya kujisifu lkn hakuna faida ya . Kila mwaka Serikali inakula lose ya mabilioni

Ambao wanachukulia Mambo kirahisi hawataelewa. Wataamini propaganda na hadidhi za bulicheka na ndoto za abunuasi za kuvuka bahati kwa kugeuza meza na kupanda juu yake.

Ukweli NI kuwa mradi utakausha kau fedha mtaani, Utajiendesha kwa hasara, hautaleta faida.

Serikali ingejitoa kabisa kwenye ujenzi na uendeshaji ikakaa kusubili kodi.
Ila Kama Serikali itafanya biashara hii ni hatari kwake na Sekta binafsi za usafirishaji. Haina ubunifu. Wanachojua Serikali NI kuwafungia Sekta binafsi ili wao wauze. Kama ilivyofanya Air Tz dhidi ya fast jet. lkn Serikali haifaidiki chochote na abiria wanaumia.

Tunaitaji reli nzuri lkn bila hakukuwa na ulazma wa Serikali yenyewe kuhusika.

Hayo matilioni yatapotea. Tulikuwa tunapiga hatua Ila Sasa tunatumia ma tilion kuliundia taifa zigo la kuhudumiwa na matilioni kila mwaka.
Kwenye nchi yoyote, mitandao ya barabara na reli ni jambo la muhimu kweli kweli. Huwezi kuendesha nchi bila mizigo na watu kusafiri. Na reli ni moja ya njia za kuaminika na rahisi kwa usafirishaji. Tatizo liko kwenye uendeshaji. Ndiyo maana watu wenye akili wanasema tunatakiwa kufumua system yetu yote ya utawala na kuisuka upya. Viongozi wawe wanapimwa kwa wanachofanya na siyo wanavyoropoka.
 
Pili si kila mradi wa serikali upo pale kuleta faida, mingine inakuwa ni vichocheo vya uchumi,
Kwani wewe ukiona serikali inajenga barabara za lami kwa mabilioni ya shillingi unategemea serikali ipate faida ya moja kwa moja?

Mkuu, naona unadogosha tatizo la ufanisi kwa kutumia dhana kuwa vitu hivi ni vichocheo vya shughuli za uchumi. Kama tukienda na dhana hiyo, je kufa kwa reli za kati na TAZARA ni vielelezo kuwa hakuna tena shughuli za uchumi?? Je hiyo imekaaje ukilinganisha na ukuaji wa usafiri wa barabara ambao ni aghali zaidi kukiko reli??

Kama huna taaluma na usafirishaji, nyamaza na usiyaone mambo haya kama ni siasa. Usafiri wa barabara umekuwa kwa kasi ukiziba matatizo ya usafirishaji wa reli kuanzia wizi, ucheleweshaji na ukosefu wa taarifa! Dunia ya sasa inahitaji mnyororo wa ugavi (supply chain) ulio haraka, ufanisi na gharama ndogo. Mambo hayo matatu yameleta reli kuwa za gharama - gharama kubwa ndio zinafanya supply chain moja kuwa aghali kuliko nyingine na hata kuondoa watu katika biashara kabisa.

Ulilotaja kama sababu ya miundombinu kuwepo ndio hasa sababu ya miundombinu hiyo kufa. Kwa kuwa uongozi unaiona kama huduma, kumekuwa hakuna bidii hata kubreak-even, achilia mbali kupata faida kidogo!!

Unachoshangilia ni kuifanya serikali kukosa kiasi cha fedha kuangalia mambo mengine katika jamii na badala yake ku-safe face kwa miradi hii na kama hilo litatokea kwa SGR - itakuwa ni jambo kubwa sana!!

Niliwahi kushauri hapa, hatukuhitaji SGR kwenda Mwanza bali Tunduma. Ingekuja mpaka Dodoma kisha ikapita Iringa, Mbeya hadi Tunduma!! TRL ingeimarishwa kutoka Dodoma kwenda Kigoma na Mwanza. SGR ingelenga Zambia, Malawi, DRC.

Interest declaration: mimi ni supply chain professional!
 
LOooh, mkuu 'William Mshumbusi', umeweka bonge la mada hapa, lakini najua, kama kawaida yetu siku hizi hapa JF, tutaigusagusa tu na kwenda zetu kwenye utani wetu wa CCM na CHADEMA!

Umeanza na mfano mzuri sana wa TAZARA, jinsi reli ile ilivyojengwa haraka na kwa ufanisi na wachina. Madhumuni wa ujenzi wa reli ile ulijulikana bayana, kuondokana na utegemezi wa nchi za mstari wa mbele katika ukombozi kuwategemea makaburu katika maswala yao ya uchukuzi na usafirishaji wa mizigo yao.
Kabla ya mchina kujenga ile reli, wafadhiri wa nchi za Magharibi waliombwa kusaidia kuijenga, wakang'aka, huku wakisema reli eneo hilo haina faida. Hao hao, walipoona mchina anaijenga reli, haraka wakawa mbioni kwenye ujenzi wa barabara. Unaweza kutafsiri mwenyewe maana ya hayo yote.

Reli, kama ulivyoeleza ilifanya kazi vizuri mwanzoni mwa utumikaji wake, na umeeleza kwa nini kadri miaka ilivyoendelea, ndio ufanisi wake ulivyozidi kufifia hadi sasa.
Binafsi ningependa sana ukazie hapa, penye udhoofu wa ufanisi. Ueleze sababu hasa ni zipi, pamoja na kwamba umegusia kama kawaida yetu sote siku hizi, lawama za kwamba serikali haiwezi kufanya biashara. Mimi sikubaliani na jibu hilo jepesijepesi hivyo. Serikali inaweza sana kufanya mambo yake kwa ufanisi iktaka kufanya hivyo. Nyakati hizi haifanyi hivyo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo hiyo ya sekta binafsi unayoipigia chapuo hapa, ikiwa ndio kikwazo kikubwa sana katika kudhoofisha shughuli za serikali.

Wenye malori bila shaka hawawezi kulaza damu wakiona shughuli za reli zinafana huku zikiwapunguzia wao wanachokitafuta. Tunaweza sana kulijadili hili, hata kama hatuwezi kukubaliana.

Matatizo yanayojitokeza ndani ya mashirika ya umma, yanaanzia huko huko kwenye sekta binafsi, na ukosefu wa usimamizi bora ndani ya mashirika yenyewe. Hii haimaanishi kwamba udhaifu huo hauwezi kudhibitiwa kama serikali ikiamua na kuwa na nia ya kufanikisha shughuli zake. Kusema serikali haiwezi kufanya biashara, ni sawa pia na kusema serikali haiwezi kufanya shughuli yoyote kwa ufanisi. Kwa hiyo tuondoe serikali tubinafsishe shughuli zote zinazofanywa na serikali?

Tusifanye uwekezaji ndio uwe muarobaini wa matatizo yetu, kila mara tunaposhindwa kwa uzembe tu, eti tukimbilie kwenye uwekezaji.

Kwa nadhalia Serikali Inaweza ikafanya kilakitu. Ila unapotengeneza hoja lazma tuje na vividi. Tuje na mifano halisi. Lini na wapi ilifanya biashara kwa ufanisi na kufanikiwa? Ila kwa biashara za kitabuni wako vizuri sana. Kama motivation speaker na hadithi ya faida ya kilimo Cha matikiti. Juzi walijaribu kwenye korosho ikawaacha watu kwenye maumivu makali sana ambayo hawatayasahau.
Kama Serikali ikiamua kufanya biashara hiyo ya usafirishaji inabidi ijiandae tu kukabiliana na figisu na kila changamoto kutoka kwa wenye mabasi na reli. Isitegemee mseleleko. Ipambane iwe Bora kuliko wao na iweze kujisimamia isihujumiwe. Na ndio maana halisi ya ushindani lkn isiwafunge mikono washindani wengine. Na Kama haiwezi isifanye biashara.
 
Pili si kila mradi wa serikali upo pale kuleta faida, mingine inakuwa ni vichocheo vya uchumi,
Kwani wewe ukiona serikali inajenga barabara za lami kwa mabilioni ya shillingi unategemea serikali ipate faida ya moja kwa moja?
Tunazungumzia option za kuufanya mradi uwe na faida. Lkn huu mradi akitaka aujenge na kuuendesha mchina. Angeachiwa tu. Serikali ikawa inakula Kodi tu za Vat na nyingine. Swala sio kujengwa. Swala itaweza kujisimamia. Na Kama unagarimu ma tilion unachochea au fifisha uchumi?
 
Mwaka 1970-1974 mchina alijenga reli ya Tazara ya kisasa kwa wakati huo na watanzania waliaminishwa makubwa Sana juu ya faida ya mradi husika. Miaka 25 tu baada ya mradi kukamilika reli ikachoka, ikakosa wateja, usimamizi mbovu. Zile hadithi na simulizi tamu za manufaa ya mradi huo walioaminishwa watanzania hakuna Tena na njia kuu ya uchukuzi Tanzania to Zambia kubaki NI barabara ya Rami.

Pia Serikali ililithi reli ya Kati kutoka kwa mkoloni. Na reli ilibaki njia kuu ya uchukuzi Hadi miaka ya 90s katikati. Lakini shirika liliendeshwa kihuni Sana. Shirika liliuza tiketi chache Sana. Zaidi ya 80% ya abilia walilipa Ela keshi zilizoishia mikononi mwa walinzi na wafanyakazi wa shirika lenyewe.

Mpaka leo reli haikujiendesha. Inakula Kodi zetu kila siku kukarabatiwa lkn maingizo hakuna NI hasara tu.
Nisiwachoshe kabisa. Sizungumzii kbs mradi wa Mabasi ya mwendokasi unavyoumiza taifa ikiwa NI chini ya miaka kumi tu uanshwe. Serikali inamwaga fedha kuuokoa Ila watachoka tu. Mabasi kibao yameharibika yakatelekezwa na kuoza.
Ndege zipo kwaajili ya kujisifu lkn hakuna faida ya . Kila mwaka Serikali inakula lose ya mabilioni

Ambao wanachukulia Mambo kirahisi hawataelewa. Wataamini propaganda na hadidhi za bulicheka na ndoto za abunuasi za kuvuka bahati kwa kugeuza meza na kupanda juu yake.

Ukweli NI kuwa mradi utakausha kau fedha mtaani, Utajiendesha kwa hasara, hautaleta faida.

Serikali ingejitoa kabisa kwenye ujenzi na uendeshaji ikakaa kusubili kodi.
Ila Kama Serikali itafanya biashara hii ni hatari kwake na Sekta binafsi za usafirishaji. Haina ubunifu. Wanachojua Serikali NI kuwafungia Sekta binafsi ili wao wauze. Kama ilivyofanya Air Tz dhidi ya fast jet. lkn Serikali haifaidiki chochote na abiria wanaumia.

Tunaitaji reli nzuri lkn bila hakukuwa na ulazma wa Serikali yenyewe kuhusika.

Hayo matilioni yatapotea. Tulikuwa tunapiga hatua Ila Sasa tunatumia ma tilion kuliundia taifa zigo la kuhudumiwa na matilioni kila mwaka.
Majizi yameshaanza kupapatuka
kama hili sijui hata kama yanaelewa vizuri faida ya mradi wa SGR kwamba utakomboa wengi.....
hamtaki kuona wtz wananyanyuka
 
Serikali ya Tanzania haija uwezo wa kuendesha mradi wowote kwa faida.

Siyo kweli kuwa eti sekta binafsi ndiyo inayosababisha serikali ishindwe kuendesha miradi ya biashara kwa faida. Kusema kwamba sekta binafsi inaihujumu mirafi ya serikali ili sekta binafsi ipate biashara ni uwongo mkubwa:

1) TANESCO haijawahi kutengeneza faida hata mwaka mmoja, inashindana na nani?

2) ATCL haijawahi kupata faida hata mwaka mmoja. Waliiondoa Fastjet kwa mizengwe. Je, sasa wanapata faida?

3) Serikali ilikiwa inamiliki viwanda vya bia kabla ya kubinafsishwa, haikuwahi kutengeneza faida hata mwaka mmoja. Ilikuwa inashindana na nani wakati huo?

4) Serikali ilikuwa inamiliki kiwanfa cha sigara, haikuwahi kutengeneza faida, ilikuwa inashindana na nani?

5) Serikali ilikuwa inamiliki viwanda vya zana za kilimo, kampuni ya simu na posta, na mengine mengi, lakini ilishindwa.

Serikali, kama ilivyo kwenye taasisi nyingine, imejaza watu wa ajabu, watu wenye uwezo mdogo, wanaoteuliwa kuendesha miradi hiyo wanateuliwa kwa mtazamo wa kisiasa, watu ambao uwezo na maarifa yao ni duni sana. Watu kama Sabaya, Mwigulu, Kalemani, Biteko, unategemea wanaweza kuendesha mradi wowote ukapata faida? Watu wa namna hiyo, ndiyo wamejaa kwenye taasisi za Serikali ambazo zilistahili kuongozwa na watu kwa kuangalia weledi na siyo siasa za ulimbukeni wa siasa.

Nani atumie usafiri wa TAZARA, wakati ukitaka kusagirisha mizigo yako, mlolongo wa kuoitia ni kama umeenda kuomba msaada. Watendaji wengi wa sekta ya umma wanachojua ni kuabudiwa, siyo time sensitive. Vivyo hivyo itakuwa kwa SGR.
Una Akili kubwa Sana. Ubaya kwa Akili hii huwezi kupata nafasi kubwa serikalini.
 
TAZARA ilishindwa nini kuwakomboa wengi kwa miaka 50 ya uwepo wake?
Hizi ndio zile hadithi zenu za Muongo za gesi ikipatikana tataizo la umeme litakuwa la kihistoria..propoganda ni rahisi sana.
Majizi yameshaanza kupapatuka
kama hili sijui hata kama yanaelewa vizuri faida ya mradi wa SGR kwamba utakomboa wengi.....
hamtaki kuona wtz wananyanyuka
 
Mradi wa mwendokasi ulianza kipindi cha mwendakuzimu, na bado ulifeli, nikawa najiuliza na hata humu ndani nimeuliza zaidi ya mara moja, nini kinafanya tuamini SGR itakuwa na ufanisi?
hofManya mradi wa mwendo kasi usijiendeshe kwa ufanisi wakati abiria wa kumwaga ndicho kitakafanya SGR isijiendeshe kwa ufanisi!

Uvivu, ufisadi na ujinga wa mwafrika
 
Nauli wanayotoza inalingana na vyombo vya usafiri vya watu binafsi. Inakuwaje wao washindwe wakati watu binafsi wanamudu kwa nauli hiyo hiyo? Au umeishiwa na utetezi?
Yaani mpaka iwe bure kabisa ndo ujue ni huduma kwa jamii?
 
Inaleta faida indirect kwa hayo mabasi yaliyoharibika?
haipo kuleta faida direct, faida yake ipo indirect kwa maana Wananchi/watu wanafika maeneo ya kazi/biashara kwa wakati, Pili utendaji kazi unaongezeka ivyo serikali inapata faida kupitia uzalishaji wa wafanyakazi Na pia wafanyabiashara kuzalisha Na kulipa kodi. Kabla ya BRT kutoka Mbezi to Posta vice versa mtanzania alikuwa anapoteza masaa 5-6barabarani anafika sehemu ya uzalishaji kachoka hatari! BRT imespend around 400Billion lakin faida zake ni kubwa kiuchumi!
 
BRT haipo kuleta faida direct, faida yake ipo indirect kwa maana Wananchi/watu wanafika maeneo ya kazi/biashara kwa wakati, Pili utendaji kazi unaongezeka ivyo serikali inapata faida kupitia uzalishaji wa wafanyakazi Na pia wafanyabiashara kuzalisha Na kulipa kodi. Kabla ya BRT kutoka Mbezi to Posta vice versa mtanzania alikuwa anapoteza masaa 5-6barabarani anafika sehemu ya uzalishaji kachoka hatari! BRT imespend around 400Billion lakin faida zake ni kubwa kiuchumi!
Izo Basi zikiwa za kampuni binafsi kipi kitaharibika. Serikali kumiliki mabasi NI ujinga uliopitiliza. Landcruser mkonge mpya halmashauri inazitumia miaka minne tu zinalala. Leo imiliki bus kweli.
 
Mradi wa mwendokasi ulianza kipindi cha mwendakuzimu, na bado ulifeli, nikawa najiuliza na hata humu ndani nimeuliza zaidi ya mara moja, nini kinafanya tuamini SGR itakuwa na ufanisi?
Yani wewe huyo mwendakuzimu wako bado anakuchapa hata baada ya kufa!

Miradi ya selikali inafeli sababu moja tu!
Uvivu, ufisadi na ujinga wa mtu mweusi.

Hapa nlipo nmelipia kwa ajili ya kuwekewa maji, lakini ni wiki ya pili hii sijaletewa maji naambiwa mita zimeisha!

Nayo hii mwendakuzimu wako yupo?

Huyo mtu atakutesa sana maisha yako.
 
Kwani kipi kilikuwa tofauti kipindi cha mwendakuzimu?
 
Kuna watu waliamini hiyo reli inajengwa na fedha za serikali na sio kwa mkopo..

Yule jamaa alijua kuwafanyia hadaa watu sana!
 
Kwa mawazo yako unafikiri kila kitu kiko sawa usipoona huo ushahidi?
 
Ni jambo Jema sana Mradi kujiendesha,
Lakini Muhimu zaidi na lengo namba moja la serikali inatakiwa iwe ni kutoa huduma kwa wananchi, profit iwe ni lengo la pili,
Ziko nchi kama China hawa madereva Wa madaladala wanalipwa kama wafanyakazi Wa umma. They know this.
mbaya zaidi hizo huduma hazitolewi. leo hii TAZARA inatoa huduma gani?
 
Back
Top Bottom