Serikali ya Tanzania haina uwezo wa kuendesha mradi wowote kwa faida.
Siyo kweli kuwa eti sekta binafsi ndiyo inayosababisha serikali ishindwe kuendesha miradi ya biashara kwa faida. Kusema kwamba sekta binafsi inaihujumu miradi ya serikali ili sekta binafsi ipate biashara ni uwongo mkubwa:
1) TANESCO haijawahi kutengeneza faida hata mwaka mmoja, inashindana na nani?
2) ATCL haijawahi kupata faida hata mwaka mmoja. Waliiondoa Fastjet kwa mizengwe. Je, sasa wanapata faida?
3) Serikali ilikiwa inamiliki viwanda vya bia kabla ya kubinafsishwa, haikuwahi kutengeneza faida hata mwaka mmoja. Ilikuwa inashindana na nani wakati huo?
4) Serikali ilikuwa inamiliki kiwanda cha sigara, haikuwahi kutengeneza faida, ilikuwa inashindana na nani?
5) Serikali ilikuwa inamiliki viwanda vya zana za kilimo, kampuni ya simu na posta, na mengine mengi, lakini ilishindwa.
Serikali, kama ilivyo kwenye taasisi nyingine, imejaza watu wa ajabu, watu wenye uwezo mdogo, wanaoteuliwa kuendesha miradi hiyo wanateuliwa kwa mtazamo wa kisiasa, watu ambao uwezo na maarifa yao ni duni sana. Watu kama Sabaya, Mwigulu, Kalemani, Biteko, unategemea wanaweza kuendesha mradi wowote ukapata faida? Watu wa namna hiyo, ndiyo wamejaa kwenye taasisi za Serikali ambazo zilistahili kuongozwa na watu kwa kuangalia weledi na siyo siasa za ulimbukeni.
Nani atumie usafiri wa TAZARA, wakati ukitaka kusafirisha mizigo yako, mlolongo wa kupitia ni kama umeenda kuomba msaada. Watendaji wengi wa sekta ya umma wanachojua ni kuabudiwa, siyo time sensitive. Vivyo hivyo itakuwa kwa SGR.