stakehigh
JF-Expert Member
- Aug 9, 2019
- 7,134
- 4,556
Chini ya CCM hii nchi haiwezi kwenda popote hata wakitawala miaka 10000.
unataka nchi iwe chini ya nan dogo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chini ya CCM hii nchi haiwezi kwenda popote hata wakitawala miaka 10000.
Reli ya Tazara ilipingwa vikali na WB/IMF kwa sababu za nguvu kwamba was not economically viable na mbaya zaidi feasibility study haikufangika hivyo wakakataa kutoa mkopo kwa Nyerere.
Hapo sasa ikabidi mwalimu akajisalikishe kwa beberu mpya China matokeo yake reli ikajengwa ndio hadi leo hii ni hasara kwa kwenda mbele.
Jiulize kama Tazara inakula hasara na 70% za mzigo wa bandara ya Dar unakwenda Sadc region unadhani hiyo sgr ya TRC itakuaje?
Kwa miaka yote TRc inakula hasara mara wafanye wao mara walete wawekezaji lakini ni loss loss loss na zero kila wakati.Sasa subiria sgr ikamilike loss yake Atcl na Tanesco watasoma.
Hii nchi tutaendelea kula hasara na maisha magumu kwa mda wote kutokana na maamuzi yasiyo na tija hayakuzingatia weledi bali hisia za kikanda na kisiasa.
As for me muda wa kujenga sgr ulikuwa bado Sana ilitakiwa tuimarishe barabara na tusubirie Congo drc iwe na stability huku mashariki kwake na biashara yake iwe vizuri ndio Tujenge hiyo sgr .
Hakuna shirika la serikali linapata faida halipo labda mabenki ambako ina hisa,hata huo mwendokasi ni bora wafanye private sector au njia hizo ziwe za daladala tuu.Kila siku nawaambia mtu wa serikali anaepokea salary hawezi leta tija Serikalini hata siku moja,kinachofanyika private sector Ili mambo yaende ukileta Serikalini watu wataacha Kazi na wengi watafukuzwa.
Lengo lilikuwa ukiendeshwa kws ufanisi daladala zingeondoka katikati ya jiji ili ibaki mwendokasi, na ndivyo mipango ya majiji makuu duniani.kwan mwendokasi umeharibu biashara ya daladala?
Iwe chini ya Hashim Rungwe sister.unataka nchi iwe chini ya nan dogo?
Lengo lilikuwa ukiendeshwa kws ufanisi daladala zingeondoka katikati ya jiji ili ibaki mwendokasi, na ndivyo mipango ya majiji makuu duniani.
Iwe chini ya Hashim Rungwe sister.
kwan mwendokasi haiendeshwi kwa ufanisi? yaani vitu unavyoongea bora tu umeficha id
chato kuna watu pia,kisogo lako limejaa ubinafsi ndio sababu huoni
Nimewahi kuhoji zaidi ya mara moja humu jukwaani kwa washabiki wa hiyo reli ya SGR, je ni faida gani inapatikana kutoka kwenye reli ya kati na TAZARA, mpaka tuamini SGR itakuwa na ufanisi kuliko hizi zilizopo? Sioni majibu ya maana zaidi ya propaganda mfu. Nilisema iwapo watu wanaamini hiyo SGR itakuwa na ufanisi,ni kipi kinafanya huu mradi wa mwendo kasi uendeshwe kwa ufanisi duni, wakati abiria ni wa kumwaga?
BRT haipo kuleta faida direct, faida yake ipo indirect kwa maana Wananchi/watu wanafika maeneo ya kazi/biashara kwa wakati, Pili utendaji kazi unaongezeka ivyo serikali inapata faida kupitia uzalishaji wa wafanyakazi Na pia wafanyabiashara kuzalisha Na kulipa kodi. Kabla ya BRT kutoka Mbezi to Posta vice versa mtanzania alikuwa anapoteza masaa 5-6barabarani anafika sehemu ya uzalishaji kachoka hatari! BRT imespend around 400Billion lakin faida zake ni kubwa kiuchumi!
Naona uwezo wako wa kutambua mambo ni wa chini, inatosha.kwan mwendokasi haiendeshwi kwa ufanisi? yaani vitu unavyoongea bora tu umeficha id
Hii ndio sababu biashara za serikali huwa zinashindwa vibaya sana
Unalalamika sana kama mwajuma ndala ndefuMwaka 1970-1974 mchina alijenga reli ya Tazara ya kisasa kwa wakati huo na watanzania waliaminishwa makubwa Sana juu ya faida ya mradi husika. Miaka 25 tu baada ya mradi kukamilika reli ikachoka, ikakosa wateja, usimamizi mbovu. Zile hadithi na simulizi tamu za manufaa ya mradi huo walioaminishwa watanzania hakuna Tena na njia kuu ya uchukuzi Tanzania to Zambia kubaki NI barabara ya Rami.
Pia Serikali ililithi reli ya Kati kutoka kwa mkoloni. Na reli ilibaki njia kuu ya uchukuzi Hadi miaka ya 90s katikati. Lakini shirika liliendeshwa kihuni Sana. Shirika liliuza tiketi chache Sana. Zaidi ya 80% ya abilia walilipa Ela keshi zilizoishia mikononi mwa walinzi na wafanyakazi wa shirika lenyewe.
Mpaka leo reli haikujiendesha. Inakula Kodi zetu kila siku kukarabatiwa lkn maingizo hakuna NI hasara tu.
Nisiwachoshe kabisa. Sizungumzii kbs mradi wa Mabasi ya mwendokasi unavyoumiza taifa ikiwa NI chini ya miaka kumi tu uanshwe. Serikali inamwaga fedha kuuokoa Ila watachoka tu. Mabasi kibao yameharibika yakatelekezwa na kuoza.
Ndege zipo kwaajili ya kujisifu lkn hakuna faida ya kipato.
Ambao wanachukulia Mambo kirahisi hawataelewa. Wataamini propaganda na hadidhi za bulicheka na ndoto za abunuasi za kuvuka bahati kwa kugeuza meza na kupanda juu yake.
Ukweli NI kuwa mradi utakausha kau fedha mtaani,
Serikali ingejitoa kabisa kwenye ujenzi na uendeshaji ikakaa kusubili kodi.
Ila Kama Serikali itafanya biashara nk hatari kwake. Haina ubunifu. Usimamizi mbovu.
Kwa jinsi tulivyo
Tunaitaji reli nzuri lkn bila kupitiachito reli.
Tukubali tu tungevutia mwekezaji binafsi. Serikali ikiuchukua usimamizi na hivi haijui ubunifu, Itapiga marufuku maroli ya mizigo ili wao wapate mzigo.
Hayo matilioni yatapotea Kama mradi usio na uhakika.
BoraUmeandika jambo kubwa lakini bila vielelezo na uthibitisho mfano umeandika serikali inatoa fedha kwenye mradi wa mwendokasi ilitakiwa useme inatoa kiasi gani na mradi unapata hasara kiasi gani na kwanini unashindwa kujiendesha.Umeandika kuhusu SGR lakini sijaona facts kuthibitisha mradi utashindwa.
Anaongea jambo la muhimu serikali sio wabunifu na hawawez competition si umeona kwenye airtavel wameua baadhi ya Makampuni yenye nguvu kama fastjetWewe nazani ni Mmiliki wa molori
Nikushauri tu kuwa mbunifu na biashara yako itakuwa poa
Acha majungu kwa wenzako
Fact kwako huwa ni kitu gani? Huoni suala la TAZARA alivyoliongelea na kuoanisha na SGR? Ndiyo fact yenyewe hiyo.kujiendesha.Umeandika kuhusu SGR lakini sijaona facts kuthibitisha mradi utashindwa.
Ukiona mikataba ya wachina SGR Tazara na Urafiki utakuwa mpumbavu wa kuingia mkenge mkataba wa bandari ya bagamoyo...hizo lawama unazopeleka kwa serikali siyo sisi wala wazambia tunaweza kufanya chochote kuhusu hiyo reli.
Tatizo lipo kwa watendaji, wamekosa ubunifu...
Kuhusu reli, kuna matajiri wana magari yakusafirisha mizigo kibao, unadhani wataruhusu reli ifanye kazi...