Mradi Wa SGR Ya Tanzania Ni Mradi Mkubwa Kuwahi Kufanyika Barani Afrika

Mradi Wa SGR Ya Tanzania Ni Mradi Mkubwa Kuwahi Kufanyika Barani Afrika

Tz boy 4tino

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
1,598
Reaction score
1,822
Mradi wa SGR ya Tanzania wenye Kilomita zaidi ya elfu 2,000, ni Kati ya miradi mikubwa ya reli kuwaikufanyika Afrika.
Katika utafiti wangu, miradi mengine mikubwa inayoendelea barani Afrika ni ule wa Nigeria, ambao una lengo la kuunganisha miji mikubwa na bandari ya Lagos. Pamoja na wa Misri ambao ni wa kilometa 1,800.
Lakini ukilinganisha miradi hii na ule wa SGR Tanzania tofauti kuu ni mmoja, mradi wa Tanzania unaunganisha nchi 5 wakati ile ya Nigeria na Misri lengo ni kuunganisha miji ya ndani. Hivyo in terms of umuhimu na hadhi bado mradi wa Tanzania upo juu zaidi ya hii miwili, na unatazamiwa na wengi kama mradi wa reli wa mfano barani Afrika, kama ilivyokuwa mradi wa TAZARA katika miaka ya 70.

Jambo lakushanganza ni namna watanzania hatuna habari nao, vipi ni kukosa uzalendo ama wengi hawana taarifa??.

Na uhakika huu mradi ungekuwa hapo Kenya Dunia nzima lazma ingeutambua.

Katika tafiti yangu pia nimegundua hata video zinazo zungumzia mradi huu na miradi mengine ya Tanzania hazina watazamaji wengi ukilinganisha na miradi ya nchi nyengine za Afrika.
Hii inaonyesha watanzania bado hawana interest na taarifa za maendeleo ya nchi yao. Nini tatizo?

6C5BBB65-0EB2-410F-9A17-35AD8CC7E121.jpeg

CEB98C9D-A63C-4927-B962-A806C56CD8BA.jpeg

2E537913-D628-46EA-AABB-E8BCCAD62464.jpeg

35ECA5EE-2D94-49F5-8DBE-F8C458A5E916.jpeg

43120507-07E2-41FF-80A5-48C456D427DA.jpeg

E7F47ED9-4352-4391-ACD3-436044F23F0D.jpeg
 
True ila kupunguza gharama SGR ingeanzia kituo cha pugu station. Barabara ya mabus ya mwendokasi ndo ingeenda hadi pugu station.
 
Kuliko kujenga madaraja ya magari juu treni chini, ingefaa tuta la reli ndo liinuliwe juu mita 5.kisha magari ndo yapite chini kwa kuweka tunnel yaani matobo ya watu na magari kupita chini kila baada ya mita 500 kuwezesha watu na magari kupita chini. Hili la kuweka fence Ili kudhibiti watu wasipite juu ya reli, wabongo sio waelewa wa kutunza miundombinu hata shaka za huo uzio wanauweka sio garantii Sana ya kudumu. Kuwakomesha watu ilikuwa ni kuinua tuta juu mita 5 Ili atakaeifata treni huko juu ni halali yake kuliwa kichwa.
Hata maporini Ili kutozuia mapitio ya wanyama wainue tuta juu mita 5,vifusi sio vya kuuliza milima tele imejaa ni kusomba tu kisha unajengea kingo pande zote kuzuia mmomonyoko.
 
HONGERA RAIS WETU MPENDWA MAMA SAMIAH, AFRICA YOTE INAKUTUPIA JICHO WERE,
#SSH_2025-2030,TAYARI UMESHAPITA.
 
Zamani kabla ya uzio pande mbili za mtaa zilizotenganishwa na reli ziliweza wasiliana kwa umbali wa mita 60 sawa na dakika 2.Baada ya fence unalizimika kuzunguka kilometa 4 au 5 dakika 30 au 45 Ili ufike point ya zamani uliyotumia dakika 2.Hili ni kuwanyima watu wa pande mbili haki ya kuwasiliana, pia kwa utafiti kuweka fence pande mbili sio solution ya kuzuia watu kukatiza vivuko visivyo rasmi kutokana na akili ya mswahili ilivyo kwenye uharibifu. Lengo la uzio wa fence ni jema kiusalama zaidi watu wasigongwe na treni pili wasiathirike na nguvu ya high voltage ya umeme. Sidhani kama ni solution ya kudumu. Salama zaidi hasa huko porini na vijijini ni kujaza kifusi juu mita 5 then KILA mita 500 yanawekwa matobo Ili watu na mifugo imudu kupita.
Kwa uzoefu case study kulikuwa na kampuni ya kuchimba visima jina Hesawa kwa ufadhili wa jumuiya za kimataifa walijitolea nchi nzima kuchimba visima vya maji na kuweka pump za mkono, cha ajabu mswahili alivyo na akili fupi anaenda kufungua nati ya pump kisha anaweka kwenye fimbo yake fahari tu, then pump zinakufa Jamii inakosa maji. So hata hizi nguzo na fence kuna hati hati ya mswahili kuhujumu wanaangusha nguzo za fence chini kisha wanaponda wanatoa nondo wanakwenda kuweka kwenye madirisha ya nyumba zao. Njia pekee ya kuwakomesha ni tuta juu mita 5 pembeni ukuta kama ilivyo Buguruni Hakuna atakaemudu kupanda juu kwa njia hii itakuwa salama zaidi.
 
Wataangalia na nini wakati internet imekuwa biashara badala ya huduma.......ma ISP wote ni wezi na mijizi ya mb za watumia mb......hapo unadhani Nani atajisumbua........tufeeee......labda tufeee
 
Mradi wa SGR ya Tanzania wenye Kilomita zaidi ya elfu 2,000, ni Kati ya miradi mikubwa ya reli kuwaikufanyika Afrika.
Katika utafiti wangu, miradi mengine mikubwa inayoendelea barani Afrika ni ule wa Nigeria, ambao una lengo la kuunganisha miji mikubwa na bandari ya Lagos. Pamoja na wa Misri ambao ni wa kilometa 1,800.
Lakini ukilinganisha miradi hii na ule wa SGR Tanzania tofauti kuu ni mmoja, mradi wa Tanzania unaunganisha nchi 5 wakati ile ya Nigeria na Misri lengo ni kuunganisha miji ya ndani. Hivyo in terms of umuhimu na hadhi bado mradi wa Tanzania upo juu zaidi ya hii miwili, na unatazamiwa na wengi kama mradi wa reli wa mfano barani Afrika, kama ilivyokuwa mradi wa TAZARA katika miaka ya 70.

Jambo lakushanganza ni namna watanzania hatuna habari nao, vipi ni kukosa uzalendo ama wengi hawana taarifa??.

Na uhakika huu mradi ungekuwa hapo Kenya Dunia nzima lazma ingeutambua.

Katika tafiti yangu pia nimegundua hata video zinazo zungumzia mradi huu na miradi mengine ya Tanzania hazina watazamaji wengi ukilinganisha na miradi ya nchi nyengine za Afrika.
Hii inaonyesha watanzania bado hawana interest na taarifa za maendeleo ya nchi yao. Nini tatizo?

View attachment 2219262

View attachment 2219263

View attachment 2219264

View attachment 2219265

View attachment 2219266

View attachment 2219267

Uchawa si kwa mtu tu. Unaonaje tuseme ndiyo mradi mkubwa kabisa duniani? Si ingependeza zaidi?
 
Back
Top Bottom