Mradi wa Stieglers: Mwarabu anaharibu mradi hana utaalam wala ujuzi wa kujenga bwawa, italeta hasara kubwa kwa taifa na ubora hafifu

Mtera imejengwa na Italia, Ujerumani, Merkel alipiga simu labda kuomba hiyo tenda lakini walipewa Waarabu wa jangwani kujenga Bwawa.
Wakongwe wa hii kazi Ni wajerumani na mchina anachipukia sijui aliye mpa muarabu hii kazi aliwaza nini, nilitaka nisahau Mrusi angefanya better pia mkorea sio muarabu
 
Mimi ni CHADEMA lakini katika hili napingana na wewe, haiwezekani Mchina apewe asilimia 90 ya mradi halafu useme kazi za mwarabu hazieleweki! Ina maana 10% iliyobaki ndiyo icheleweshe mradi? Wacha porojo wewe!
 
Mkuu mwarabu ni Consultant na Mchina main contractor. Kazi ya waarabu ni kuhakikisha wachina wanafanya kazi vizuri
 
10% ya mtu kati labda ndo inauma...ila tofauti na hapo hamna shida.
 
Hakuna kiongozi anayejali watu washapiga 30% wametulia tu hata wakiboronga mtajijua wenyewe.
 
Usimlaumu mwarabu, huyo alijaribu bahati yake kwenye tender ilivyotangazwa akashinda, mlaumu aliempa kazi mwarabu, huyo ndie tatizo haswa, huwezi jua huyo mwarabu alitoa nini mpaka akapewa hiyo kazi.
Great Mind.
 
. Kama hakuto athiri napendekeza huu mradi angepewa mchina utaisha kwa wakati ila huyu mwarabu hasara iliyo mbele ni kubwa sana katika pesa na wakati
Wewe ni kibarua una hasira za kukatwa jina lako,kajambe mbele huko
 
Huu mradi sio wa leo. Hadi 2059. Ikifika 2025 jamaa ataomba aongezwe muda amalize miradi yake. Au atasisitiza awekwe mtu amtakaye kwa madai kuwa ndye atamaliza miradi yake
 
Nikajua unaandika haya kama mtaalamu, kumbe ni mwananchi wa kawaida.

Tunatakiwa mambo kama haya tuwaachie wataalamu.
 
Hili haliitaji mjadara, wamisri hawana uwezo wa kujenga power plantS za megawatts 200, tutakuja laumiana mbele ya safari....
Unatumia vigezo gani vya kitaalamu kusema haya.
 
Hilo limeshatoka, ukiona mannyoya jua kaliwa. Miradi mikubwa ukizembea au kukiuka taratibu za tender mwisho ni kuibebesha nchi zigo.la madeni.
 
Kwani ni nani hapati hasara kipindi cha mafuriko? Na ndiyo maana kuna Bima, au unafikiri kazi ya Bima ni ipi?
Kwa hiyo Bima ipo kugharamia uzembe wako, sivyo!? Yaani ukajiweke kwenye hatari kwa sababu ya bima!? Wewe ndio wale mnaojidhuru ili bima yako unayolipia isiende bure pale unapoona majanga hayakupati huku miaka ikisogea. Hiyo Bima mbona haiwasaidii abiria wanaolazimika kushukia Magomeni Mapipa wakati wanaenda Kariakoo au Posta!? Au hiyo Bima inawasaidia wewe na wenzako wenye Private cars ndio maana ni poa tu kwako!?
 
Mkuu mwarabu ni Consultant na Mchina main contractor. Kazi ya waarabu ni kuhakikisha wachina wanafanya kazi vizuri
Design anatoa nani? Unajua kazi ya Consultant site? Unadhani anaongoza kwa mdomo kama ulivyomeza?
 

November 2020

MAISHA HALISI YA WAFANYAKAZI WA MRADI WA (STIEGLER'S Gorge) , JNHPP BWAWA LA UMEME LA JULIUS NYERERE.

 
Miradi ya mfukoni ya magufuli haina tija.
 
3. Wafanyakazi wengi wazawa mikataba yao na maslai yao sio mazuri na mahusioano kati ya mwarabu na mtanzania yako kibaguzi utadhani enzi za utumwa, wana mentality za kitumwa sana na kutomjali mwafrika.
KELELE NYIIIIIIIIIIIIIIIINGI ILA HII NDIO POINT YAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…