Sosinsa Unswe
Member
- Oct 30, 2016
- 91
- 76
Habari wanajamvi,
NIkiitizama fugo ya ng'ombe wa maziwa naona kama ni fugo nzuri na yenye kuweza kuongeza kipato lakini kila niingiapo humu jukwaani sioni hamasa ya wadau kuizungumzia.
Ningependa kufahamu ni wapi inapatikana mbegu nzuri ambayo inaweza kutoa walau 20ltrs kwa siku.
Lakini pia si mbaya kama atatokea mfugaji mmoja mzoefu wa ng'ombe akatueleza faida na changamoto za fugo ya ng'ombe wa maziwa.
Thnx!

shukran sana mkuuKuna ofisi za shamba la serikali la ng'ombe wa maziwa linaloitwa KITULO hapo Mwanjelwa karibia na Maranatha pharmacy, ofisi yao inatazamana na jengo la Century Plaza. Nenda pale ninaamini watakusaidia kwa mambo kadhaa kuhusu shida yako, zile ofisi ni kwa ajili yetu wananchi, nenda tafadhali utapata kitu fulani.
asante sana mkuuKama upo mbeya ni rahisi sana, unaweza kwenda hapo chuo cha kilimo na utafiti uyole, unaweza kwenda kitulo (makete), rahisi zaidi pia unaweza kwenda Rungwe (Tukuyu) hasa hasa kiwira au ushirika huko kuna wafugaji karibu kila nyumba na ufugaji wao ni wakisasa kabisa....maziwa yanayozalishwa tukuyu yameinua maisha ya watu sana hata asasi ameweka collecting points za maziwa huko!
mwenye maziwa mengi ni Friesian ingawa kumpata pure atakusumbua sana maana ni ng'ombe wa nchi za baridi. kwa hapa Tz wanaweza kufanya vizuri Makete na Njombe kwa ujumla au baadhi ya maeneo ya Arusha. wengi waliopo ni chotara wenye uwezo wa kutoa mpaka lita 25 per day under high plane of nutrition! hawa chotara unaweza kuwapata kwenye mashamba ya uzalishaji mitamba (Mabuki MZA, Nangaramo Mtwr, west Kilimanjaro)Ni aina gani ya ng' ombe wanaotoa maziwa mengi? Na hivyo vituo ulivyotaja hapo nao wanauza hao ng' ombe