Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Yeah pia kuna centers za kilimo na ufugaji kama Ukiliguru Mwanza,Mwabuki,Tengeru Arusha na maeneo kibao.ila pia ufugaji wa ng'ombe wa maziwa unategemea na hali ya hewa ya wewe ulipo,kama ni eneo lina joto basi ni lazima upate breed inayofanya vyema ktk halijoto,mfano wa Mwanza wanakufaa,ila kama uko ktk hali ya baridi baridi wa Tengeru wanakufaa.ukimchukua wa Tengeru ukaja kumfugia Dar hato perform vizuri likewise wa Mwanza kumpeleka Arusha.ni hayo tu mkuu
 
Habari wanajamvi,
NIkiitizama fugo ya ng'ombe wa maziwa naona kama ni fugo nzuri na yenye kuweza kuongeza kipato lakini kila niingiapo humu jukwaani sioni hamasa ya wadau kuizungumzia.

Ningependa kufahamu ni wapi inapatikana mbegu nzuri ambayo inaweza kutoa walau 20ltrs kwa siku.

Lakini pia si mbaya kama atatokea mfugaji mmoja mzoefu wa ng'ombe akatueleza faida na changamoto za fugo ya ng'ombe wa maziwa.
Thnx!

Wasiliana na wataalam wa mifugo katika kituo cha NAIC- ARUSHA, utapata ushauri na mbegu bora
 
Habari wanajamvi,
NIkiitizama fugo ya ng'ombe wa maziwa naona kama ni fugo nzuri na yenye kuweza kuongeza kipato lakini kila niingiapo humu jukwaani sioni hamasa ya wadau kuizungumzia.

Ningependa kufahamu ni wapi inapatikana mbegu nzuri ambayo inaweza kutoa walau 20ltrs kwa siku.

Lakini pia si mbaya kama atatokea mfugaji mmoja mzoefu wa ng'ombe akatueleza faida na changamoto za fugo ya ng'ombe wa maziwa.
Thnx!

Kama bado hujapata

Nenda Tanga, karibu na hale ......Mruazi Heifer Breeding Unit, wanazo ngombe mitamba mizuri saana wanauza. kumbuka huu mradi ni ushirikano kati ya watanzania na waholanzi...kwanini wanauza,,,,,kwa mfululizo kwa muda wa miaka miwili hawajapata mvua so wanachangamoto ya chakula.....Mtamba mzuri mwenye mimba ya kuanzia miezi mitatu wanauza 1,800,000/= mtamba ambao hauna mimba wanauza 1,600,000/= Manager wa shamba number yake ni 0782 421 612 anaitwa Bwana Mgunya

Please note wametangaza mpaka Kenya so bora ukawahi kwani wakenya hawapendi mchazo ktk hili hata kidogo

Kila la Kheri
 
Wanabody... Naomba KUJUA aina za ng'ombe wa maziwa na uwezo wao wa kutoa maziwa kwa siku.
 
Wakuu habari zenu, naombeni kujuzwa wapi yanapatikana mashamba ya Ngo'mbe wa maziwa mkoani Mbeya. Lengo langu ni kujifunza jinsi ya kufuga ngo'mbe wa maziwa ili hapo baadae na mimi niingie kwenye biashara hiyo , kama wewe ni mfugaji naomba unipe mwaliko nije kujifunza.

Shukrani
 
Kitaaluma Mimi ni mtaalam wa Animal science and production.
Njoo DM unijuze unachotaka kufahamu kuhusu ng'ombe wa maziwa na tutajua tusaidiane vipi..!?
 
Kuna ofisi za shamba la serikali la ng'ombe wa maziwa linaloitwa KITULO hapo Mwanjelwa karibia na Maranatha pharmacy, ofisi yao inatazamana na jengo la Century Plaza. Nenda pale ninaamini watakusaidia kwa mambo kadhaa kuhusu shida yako, zile ofisi ni kwa ajili yetu wananchi, nenda tafadhali utapata kitu fulani.
 
shukran sana mkuu
 
Kama upo mbeya ni rahisi sana, unaweza kwenda hapo chuo cha kilimo na utafiti uyole, unaweza kwenda kitulo (makete), rahisi zaidi pia unaweza kwenda Rungwe (Tukuyu) hasa hasa kiwira au ushirika huko kuna wafugaji karibu kila nyumba na ufugaji wao ni wakisasa kabisa....maziwa yanayozalishwa tukuyu yameinua maisha ya watu sana hata asasi ameweka collecting points za maziwa huko!
 
asante sana mkuu
 
Good mkuu naona unatembea kwenye ndoto zang, m niko Njombe ukipata taarifa tupeane mafunzo
 
Ni aina gani ya ng' ombe wanaotoa maziwa mengi? Na hivyo vituo ulivyotaja hapo nao wanauza hao ng' ombe
 
Ni aina gani ya ng' ombe wanaotoa maziwa mengi? Na hivyo vituo ulivyotaja hapo nao wanauza hao ng' ombe
mwenye maziwa mengi ni Friesian ingawa kumpata pure atakusumbua sana maana ni ng'ombe wa nchi za baridi. kwa hapa Tz wanaweza kufanya vizuri Makete na Njombe kwa ujumla au baadhi ya maeneo ya Arusha. wengi waliopo ni chotara wenye uwezo wa kutoa mpaka lita 25 per day under high plane of nutrition! hawa chotara unaweza kuwapata kwenye mashamba ya uzalishaji mitamba (Mabuki MZA, Nangaramo Mtwr, west Kilimanjaro)
 
Back
Top Bottom