Mimi sio mfugaji wa ng'ombe ila najifunza ili nianzie na mbuzi, ninakuwekea maelezo haya uyafanyie kazi: Akiba ya malisho
Majani ya miti husaidia wakati kuna uhaba wa malisho hasa wakati wa kiangazi. Ulishaji wa virutubisho mbadala vinavyotokana na Calliandra, Leucaena diversifolia, Gliricidia sepium, na vinginevyo huongeza uzalishaji na ubora wa maziwa kwa wanyama wa maziwa, na pia hupunguza gharama ya chakula kwa ajili ya ng'ombe wa maziwa. Lisha kiasi cha asilimia 30 ya majani kutoka kwenye miti ya malisho. Wakulima wanashauriwa kulima malisho ya mifugo kama njia ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa malisho wakati wa ukame, pia kujiongezea kipato kwani malisho hayo yanaweza kuvunwa kuhifadhiwa na baadaye kuuzwa kwa wafugaji wengine wasiyo na maeneo kwa ajili ya kilimo cha nyasi.
Wafugaji wanashauriwa kupanda malisho mchanganyiko ambayo ni nyasi kama vile rhodes grass, African fox tail, na majani aina ya mikunde kama vile desmodium spp. Mbegu za malisho hupatikana katika maeneo yafuatayo; Chuo cha Mifugo Tengeru, na Vikuge wilaya Kibaha. Nakuwekea hii doc uisome ni wafugaji wa Moshi huko. Kifupi ni kuwa majani ya mahindi sidahni kama yatakidhi mahitaji ya protein, huwa inatakiwa waongezwe protein concentrates za kununua, kusaidia hilo ndio walifundishwa kulima hii mikunde in protein nyingi, ukisoma hii doc utaona matumizi yake. Lakini mtafute Prodigal Son alisema atakuelekeza vizuri zaidi