Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

heheeeeeeeee nimecheka kweli comment zako we sio Mpare unatafuta kesi ya kuku wewe? joking
Halafu Mangi inawezekana tunajadili kitu ambacho hakipo! Hebu chungulia heading "Ng,ombe wangu wamenishinda nahitaji ushauri wako" hapo kwenye red ndo nini mkuu
 
[QUOTE=Mama Joe;7143211Baada ya kupata maelekezo hapa nimenunua majani ya mahindi hekta (2)je ninaweza kuwapa hicho hich
 
Mimi sio mfugaji wa ng'ombe ila najifunza ili nianzie na mbuzi, ninakuwekea maelezo haya uyafanyie kazi: Akiba ya malisho
Majani ya miti husaidia wakati kuna uhaba wa malisho hasa wakati wa kiangazi. Ulishaji wa virutubisho mbadala vinavyotokana na Calliandra, Leucaena diversifolia, Gliricidia sepium, na vinginevyo huongeza uzalishaji na ubora wa maziwa kwa wanyama wa maziwa, na pia hupunguza gharama ya chakula kwa ajili ya ng'ombe wa maziwa. Lisha kiasi cha asilimia 30 ya majani kutoka kwenye miti ya malisho. Wakulima wanashauriwa kulima malisho ya mifugo kama njia ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa malisho wakati wa ukame, pia kujiongezea kipato kwani malisho hayo yanaweza kuvunwa kuhifadhiwa na baadaye kuuzwa kwa wafugaji wengine wasiyo na maeneo kwa ajili ya kilimo cha nyasi.
Wafugaji wanashauriwa kupanda malisho mchanganyiko ambayo ni nyasi kama vile rhodes grass, African fox tail, na majani aina ya mikunde kama vile desmodium spp. Mbegu za malisho hupatikana katika maeneo yafuatayo; Chuo cha Mifugo Tengeru, na Vikuge wilaya Kibaha. Nakuwekea hii doc uisome ni wafugaji wa Moshi huko. Kifupi ni kuwa majani ya mahindi sidahni kama yatakidhi mahitaji ya protein, huwa inatakiwa waongezwe protein concentrates za kununua, kusaidia hilo ndio walifundishwa kulima hii mikunde in protein nyingi, ukisoma hii doc utaona matumizi yake. Lakini mtafute Prodigal Son alisema atakuelekeza vizuri zaidi
 

Attachments

Mkuu una ushauri mzuri
Nikijipanga vizuri nitawasiliana nawe kwani nami ninafikiria kufuga ng'ombe
Ahsante
Sidhani kama unahaki ya kulalamika........tunaishi huku duniani ili tuitawale hii dunia na sio dunia ikutawale wewe.......namaanisha nini.....kama unajua unachokifanya sidhani hata kidogo chakula kinaweza kikawa chngamoto...
nikulize swali...unafuga kibiashara??????

Ushauri wa BURE.......kama umehamua kuwa mfugaji....usichoke kujifunza....unatakiwa uelewe kwa siku ngombe moja anakula majani/chakula cha kiasi gani inaweza ikawa unapima kwa kilo na maji kwa siku anatakiwa anjwe lita ngapi................ukishajua hilo fanya hivi........kipindi chamvua/masika hakikisha unakusanya majani ya kutosha(kumbuka unatakiwa uwe na stoo ya kuhifadhi) kulingana na idadi ya ngombe unaahakikisha unakusanya chakula cha kutosha kuwalisha ngombe wako miezi 12 au hata miezi 24

Unafanyaje..............kama unakiu ya kujifunza....soma namna ya kutengeneza .....sailage......ukikusanya majani ( kumbuka sio kila majani kwa moshi kuna majani fulani yanaitwa ya tembo yanafaa saana...unaweza yaotesha..au kuwashawishi majirani zako wakuoteshee..kipindi cha mvua unaweza vuna kila baada ya wiki tatu kama umeyatunza vizuri........kama hiyo itakuwa ngumu unaweza tafuta karatasi ngumu yanapatikana Balton chimba shimo kusanya maji ya kutosha kipindi cha mvua unaweza otesha hayo majani kwa kumwagilkia

Muda wa kulalama mabadiliko ya tabia nchi sidhani kama una nafasi hapa......nchi kama Norway na sweden ukienda kaskazini kuna maeneo wanaliona jua kwa miezi 4tu kwa mwaka lakini hawalii lii hata kidogo......chukulia hayo mazingira kama changamoto.......kama unavyojiwekea chakula cha kutosha cha familia na ngombe wanatakiwa ufanyie hivyo

Ukitaka maelezo zaidi unaweza ni ibox kila la kheri
 
Ndugu yangu kila jambo unalolifanya hakikisha unakua na vitu vitatu;Sense of purpose,Responsibilty and Efficiency....inaonekana hujajipanga vizuri ktk field hii ya ufugaji ndo mana unashindwa na hao ngombe wanne tena kwa sehemu kama kilimnjaro ambayo kimsingi nyasi zipo za kutosha. Nakushauri ufikirie ujasiliamali mali mwingine kama kulima mbogamboga kwa sababu huu utakusumbua.
 
Vizurl lakin tiyar nimewekeza katika ufugaji,ingekua vizur kama ungeonyesha njia nzuri ya kuwafu

Mkuu samahani nilkua sijakupata vizuri,kuusu namna kupata chakula hua inategemea na wee mwenyewe na sehemu uliopo, kwa uzoefu wangu maeneo ya tanga na kilimanjaro chakula kikuu ni nyasi(majani):Labda ungeeleza chakula gani ndo hakipatikani,na wee upo mazingiara gani...tuanzie hapo
 
Habar JF Mimi ni fugaji mkoani Kilimanjaro,nina ng,ombe (4) wote ni jike,tatizo ni chakula chao kinapatikana kwa shida,

Bw. Apolinary, nikiangalia mtiririko wa uzi wako, ukweli ninashindwa kujua usaidiwe vipi zaidi.
Ushauri wangu wa haraka haraka, jaribu kumuona Mtaalamu wa Mifugo wa Kata yako. Pamoja na mengine mengi anayotakiwa kukushauri, umuombe akuunganishe na Wajasiriamali ambao ni Wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa kama wewe katika Kata yenu ili ukajifunze kwao (Shamba Darasa) ili uelewe ni vipi wao wanakabiliana na changamoto kama za kwako. Usiku mwema!
 
Back
Top Bottom