Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Asante kaka hao chotara wanaweza kuwapata kwa sh ngapi mmoja mana ninampango wa kufuga ng' ombe hao wa kisasa.
 
mwenye maziwa mengi ni Friesian ingawa kumpata pure atakusumbua sana maana ni ng'ombe wa nchi za baridi. kwa hapa Tz wanaweza kufanya vizuri Makete na Njombe kwa ujumla au baadhi ya maeneo ya Arusha. wengi waliopo ni chotara wenye uwezo wa kutoa mpaka lita 25 per day under high plane of nutrition! hawa chotara unaweza kuwapata kwenye mashamba ya uzalishaji mitamba (Mabuki MZA, Nangaramo Mtwr, west Kilimanjaro)
Ahsante kwa nondo hizi... kifanyike nini kuwezesha ng'ombe chotara aongeze uzalishaji... na mmoja anaweza kugharimu kiasi gani?
 
Ahsante kwa nondo hizi... kifanyike nini kuwezesha ng'ombe chotara aongeze uzalishaji... na mmoja anaweza kugharimu kiasi gani?
Ili waongeze uzalishaji ni kuwalisha balanced diet. Kama huko uliko upo karibu na mtu aliyesoma BSc. Animal Science atakushauri vizuri sana namna ya kutengeneza mchanganyiko wa chakula chenye kulingana na kiasi cha maziwa unachotaka kizalishwe. Au kama uko karibu na SUA jaribu kutembelea idara ya sayansi ya wanyama, viumbe vya majini na nyanda za malisho hapo utakutana na maprofesa waliobobea katika maswala ya uzalishaji maziwa. Mara ya mwisho (2010) bei ya mtamba aliyepandishwa ilikuwa kati ya laki 9 mpaka 1m. Kwa sasa hivi sina bei sahihi!!
 
Niko kahama shy
Kwa vile uko Kahama nakushauri uende Mabuki Misungwi, hapo utapata ng'ombe wa kukufaa kabisa. Utapata mtamba mwenye mimba kabisa (kama utapenda). Epuka hawa wa kuuziwa mitaani utakamatishwa tasa!!
 
Asante mkuu kwa uzoefu wako huyo mwenye mimba anaweza kupeleka kama sh ngapi?
 
Hili somo ni zuri sana, lakini naona watanzania wengi tunapenda hizi kazi za show off kuvaa matai na masuti ili tuonekane vema lakini kazi kama hizi mhmh tunaona sio hadhi yetu hasa ukiwa na tu degree ndio kabisaaa....mwisho wa siku tunaishi chini ya kiwango....
 
Sio kwa mtu pekee hii ni kasumba ya waafrika uwe na mastaz halafu useme unaenda kufuga ng'ombe utachukiwa mpaka na dada wa bibi yako achilia mbali ndg wengine
 
Ili waongeze uzalishaji ni kuwalisha balanced diet. Kama huko uliko upo karibu na mtu aliyesoma BSc. Animal Science atakushauri vizuri sana namna ya kutengeneza mchanganyiko wa chakula chenye kulingana na kiasi cha maziwa unachotaka kizalishwe. Au kama uko karibu na SUA jaribu kutembelea idara ya sayansi ya wanyama, viumbe vya majini na nyanda za malisho hapo utakutana na maprofesa waliobobea katika maswala ya uzalishaji maziwa. Mara ya mwisho (2010) bei ya mtamba aliyepandishwa ilikuwa kati ya laki 9 mpaka 1m. Kwa sasa hivi sina bei sahihi!!
Shukrani mkuu... huku Wilaya hadi bwan mifugo akutembelee... ni hadi maombi ya upako...
 
Kwa vile uko Kahama nakushauri uende Mabuki Misungwi, hapo utapata ng'ombe wa kukufaa kabisa. Utapata mtamba mwenye mimba kabisa (kama utapenda). Epuka hawa wa kuuziwa mitaani utakamatishwa tasa!!
Nipo Buhongwa Mwanza,nimeuelewa vizuri ushaur nitakwenda mabuki
 
Habari wanajukwaa,
Nataka nianze mradi wa ufugaji wa ng'ombe wa kisasa wa maziwa kwaajili ya biashara,naomba wenye uzoefu wa ufugaji huu wanisaidie kupata somo na mambo ya kuzingatia wakati wa ufugaji.

Pia naomba kujuzwa mbegu bora ni ipi,upatikanaji wake na soko la maziwa likoje.niko Dar es salaam.
Asanteni
 
Habari wanajukwaa,nataka nianze mradi wa ufugaji wa ng'ombe wa kisasa wa maziwa kwaajili ya biashara,naomba wenye uzoefu wa ufugaji huu wanisaidie kupata somo na mambo ya kuzingatia wakati wa ufugaji.Pia naomba kujuzwa mbegu bora ni ipi,upatikanaji wake na soko la maziwa likoje.niko Dar es salaam. Asanteni
Mm pia naplan hii mkuu.hii biashara ukipata breed nzuri ya ngombe umaskini kwa kheri mkuu na unaweza ukafungua hata MILK POINT yako ukaauza milkshake na vitu vingine vya maziwa ya ngombe.
 
Mm pia naplan hii mkuu.hii biashara ukipata breed nzuri ya ngombe umaskini kwa kheri mkuu na unaweza ukafungua hata MILK POINT yako ukaauza milkshake na vitu vingine vya maziwa ya ngombe.
Ngoja tupate information kwa kina kutoka kwa wajuzi zitatusaidia sana
 
Ukitaka Pure breeds za Ng'ombe ni kuagiza Kenya. kule ndo kuna Pure za aina zote za breeds unazo zijua. Bongo magumash mengi mno
 
Habari wanajukwaa,nataka nianze mradi wa ufugaji wa ng'ombe wa kisasa wa maziwa kwaajili ya biashara,naomba wenye uzoefu wa ufugaji huu wanisaidie kupata somo na mambo ya kuzingatia wakati wa ufugaji.Pia naomba kujuzwa mbegu bora ni ipi,upatikanaji wake na soko la maziwa likoje.niko Dar es salaam. Asanteni
Sasa soko tena uambiwe likoje? Kwa nini kwanza unataka kufuga Ng'ombe na si Kuku au si Mbuzi au si mfugo wa aina nyingine ile?
Maana yake lazima uwe umeona kuna uhitaji wa kufuga Ng'ombe.

So swala la Soko nazani unapaswa wewe mwenyewe kufanya utafiti, Jenga mazoea ya kutafuta taarifa ambazo sio second hand.

Ishu ya Breeds bora na pure Kenya ndo zipo unaweza pata make wale wana breeds si chini ya 9 za Ng'ombe wa maziwa.
 
Habari wanajamvi,
ningetaka kufahamu kuhusu ufugaji wa ng'ombe chotara wa Biashara,
[emoji815]Eneo linalohitajika kwa ng'ombe 50,
[emoji815]Muda wa ukuaji wake,
[emoji815]ng'ombe wapi wa
Kuanza nao
[emoji815]changamoto zao kwa ujumla

Asanteni!
 
Back
Top Bottom