Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Wakuu naomba kuuliza swali. Ng'ombe dume anahasiwa ili iweje? Mimi nilidhani ananunuliwa ili azalishe?

Ivi nyama ya ng'ombe aliye asiwa inakuwa sawa na ambaye ajaasiwa msaada apo kwenye tuta
 
Sasa soko tena uambiwe likoje? Kwa nini kwanza unataka kufuga Ng'ombe na si Kuku au si Mbuzi au si mfugo wa aina nyingine ile?
Maana yake lazima uwe umeona kuna uhitaji wa kufuga Ng'ombe.

So swala la Soko nazani unapaswa wewe mwenyewe kufanya utafiti, Jenga mazoea ya kutafuta taarifa ambazo sio second hand.

Ishu ya Breeds bora na pure Kenya ndo zipo unaweza pata make wale wana breeds si chini ya 9 za Ng'ombe wa maziwa.
Kenya wapo vizuri sana katika technology ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na nyama.
Wana mbegu walizitoa Germany. Wanaitwa Fleckvieh cattle [emoji202]. Wapo vizuri sana na awashambuliwi sana na magonjwa kama wale Fresian cattle
 
TZ hakuna hii mbegu?
kwa wadau-- ni namna gani uzalishaji wa maziwa kwa mbegu chotara unaweza kuboreshwa..
Nawakilisha
 
Nilisikia South Africa [emoji288] wanauza ng'ombe dume wa fleckvieh anauza $ 15,000 ambayo ni sawa na kama Tshs 35,000,000 za kitanzania. Wale ng'ombe ni dual purpose na wanaimili sana maisha ya baridi kali na Joto kali pia na ulaji wao sio mkubwa
 
Sasa soko tena uambiwe likoje? Kwa nini kwanza unataka kufuga Ng'ombe na si Kuku au si Mbuzi au si mfugo wa aina nyingine ile?
Maana yake lazima uwe umeona kuna uhitaji wa kufuga Ng'ombe.

So swala la Soko nazani unapaswa wewe mwenyewe kufanya utafiti, Jenga mazoea ya kutafuta taarifa ambazo sio second hand.

Ishu ya Breeds bora na pure Kenya ndo zipo unaweza pata make wale wana breeds si chini ya 9 za Ng'ombe wa maziwa.
Mkuu SUA hawawezi kuwa na ng'ombe wazuri wa maziwa?
 
Habari wandugu nina M5 ninataka kuingiza katika biashara ya kununua ng'ombe mnadani huko mikoani halafu napeleka Dar kwenye mnada wa Pugu.

Mwenye ushauri juu ya biashara hii naomba anishauri, anayejua changamoto zake naye anakaribishwa ili nijipange.
 
Habari wandugu nina M5 ninataka kuingiza katika biashara ya kununua ng'ombe mnadani huko mikoani alafu napeleka dar kwenye mnada wa wa pugu,mwenye ushauri juu ya biashara hii naomba anishauri,anayejua changamoto zake naye anakaribishwa ili nijipange.

WAZO ZURI HILO.......Ngoja waje wajuvi.
 
Watu wengi hatujafanikiwa kwa sababu waliofanikiwa hawapo tayar kueleza ni jins gan wao wamefanikiwa sasa cha msingi wewe jalibu ukisubr kujua hayo hakuna wa kukuambia ndg yangu
 
Habari wandugu nina M5 ninataka kuingiza katika biashara ya kununua ng'ombe mnadani huko mikoani alafu napeleka dar kwenye mnada wa wa pugu,mwenye ushauri juu ya biashara hii naomba anishauri,anayejua changamoto zake naye anakaribishwa ili nijipange.
Nenda minada ya huko sehemu ambazo wanatimuliwa kwenye mapori ya hifadhi utapata ng'ombe kwa bei nafuu, mfano mnada wa LUSAHUNGA Biharamulo
 
Nenda minada ya huko sehemu ambazo wanatimuliwa kwenye mapori ya hifadhi utapata ng'ombe kwa bei nafuu, mfano mnada wa LUSAHUNGA Biharamulo
Yap pia nilitaka kujuazaidi kuhusu soko hapa Dar kwani nisije leta bidhaa ikakaa miezi miwili.
 
Pesa ndogo sana hio kwa biashara ya Ng'ombe
 
Milioni 5 ufanye biashara ya ng'ombe! Hiyo pesa kidogo sana!

Badala yake fanya biashara ya mbuzi. Hiyo kidogo inaweza kukusaidia kukuza mtaji wako.

Maana, hao ng'ombe ukiwanunua mikoani utahitaji usafiri wa kuwalete Dar. Sasa gharama ya usafiri peke yake kwa hiyo pesa yako haitoshi.

Mbuzi unaweza kupata faida. Japo inahitaji ubunifu na uvumilivu mkubwa sana. Mfano, unachotakiwa ili kufanikiwa kwa hiyo pesa yako. Kwanza, nenda maeneo kama Sinza, fanya makubaliano na wauza supu na wachoma nyama ya mbuzi wapatao kumi wa kuaminika na ambao wanauwezo wa kuchinja mbuzi zaidi ya watano kwa siku kila mmoja. Kwa watu kumi utakuwa na hesabu ya wastani wa mbuzi 50 kila siku.

Weka bei shindani! Kwa maana ya pungufu kidogo na bei inayotolewa kwenye mnada wa mbuzi vingunguti. Lete bidhaa baada ya makubaliano kwa kuwasambazia wateja wako kwenye maeneo uao ya biashara. Utapata matokeo mazuri kama utaifanya kwa umakini na faida kubwa utaipata.
 
Back
Top Bottom