Mrakibu Msaidizi wa Polisi Fatuma Kigondo afunguliwa shtaka la kutuma vijana kufanya ukatili kwa binti wa Yombo

Kwani hawa watu hawako smart kiasi cha kufanya mambo kizembe kizembe namna hii ilhali mara zote askari huwa wako smart zaidi kuliko raia?

Yaani sisi raia tunataka kujifanya ndiyo smart kuliko watu ambao ni professional?

Hili tukio limefanywa makusudi. Askari ni watu smart mno hawawezi kufanya kitu kizembe kizembe namna hii.

Mbali na hayo, kwa ujumla wao, fact ni kwamba askari huwa ni waadilifu kuliko raia
 
Ameshawakana, but if kuna evidence zimebaki including mawasiliani au miamala ya pesa kwenda kwa hao jamaa amekwisha
 
Askari wa Tanzania ni smart ??

Hebu elezea huo usmart uko katika nyanja ipi.

Pia huo uadilifu ni upi , pengine leo nijifunze maana tofauti ya uadilifu kutokana na kauli yako kuwa askari wa Tanzania ni waadilifu kuliko raia.
 
Askari wa Tanzania ni smart ??

Hebu elezea huo usmart uko katika nyanja ipi.

Pia huo uadilifu ni upi , pengine leo nijifunze maana tofauti ya uadilifu kutokana na kauli yako kuwa askari wa Tanzania ni waadilifu kuliko raia.
Hapo kabla, ulishawahi kukuta wamefanya tukio la kizembe namna hii? Je, ungekuwa wewe raia, ungefweza kuanya hivi? Na kama wewe raia usingeweza, je unadhani askari anaweza kufanya hivi? Kwa nini askari afanye hivi? Changanya na za kwako; be smart!
 
Unadhani kukana shitaka pekee ndiyo kutakuepusha na mkono wa sheria?

Kila mtuhumiwa akisomewa shitaka huwa anakana lakini kadri mwenendo wa kesi unavyoenda na ushahidi kutolewa mahakamani ndipo watuhumiwa wanapokuwa karibu zaidi na uhusika wa kosa husika.

Shahidi namba moja ni mwathiriwa wa tukio hivyo yeye ndiye atakayetoa ushahidi mzuri ikiwemo kumtambua mtuhumiwa kizimbani.
 
Hapo kabla, ulishawahi kukuta wamefanya tukio la kizembe namna hii?
Yale masanduku ya kura kuibiwa wakati wa uchaguzi huwa yanakwenda wapi?

Wale wafanyabiashara wa madini Mtwara waliouliwa na polisi kesi yao ilishia wapi??

Wanaotajwa kuhujumu miradi na fedha kwenye ripoti za CAG walikamatwa lini na kufikishwa mahakamani?

Nimetaja chache tu.
Je, ungekuwa wewe raia, ungefweza kuanya hivi?
Hili ni swali ?
Na kama wewe raia usingeweza, je unadhani askari anaweza kufanya hivi? Kwa nini askari afanye hivi?
Hujajibu swali.
Changanya na za kwako; be smart!
Hili ndio hitimisho la askari kuwa ni smart kuliko raia?

Ok, waliomshambulia Tundu Lissu 2017 wako wapi,?

Waliomteka Mohamed Dewji wako wapi?

Mimi naomba hao walio smart watueleze raia anaewezaje kupigwa risadi 16 kwenye ardhi yake na waliomshambulia wasipatikane hata miaka 7 mbele.

Tajiri namba moja kutekwa na watekaji wasipatikane hadi leo.

Ben Saanane kapotea mwaka wa 8 leo walio smart kushinda sie raia nao hawajui alipo.

Nimechanganya zangu nimeishia hapo.
 
sasa mkuu mbona hiyo document inaonyesha mshtaki sio jamhuri bali ni mtu binafsi huyo Paul kwani sheria zetu zinaruhusu mtu binafsi kufungua mashtaka ya jinai? hiyo si kazi ya DPP kupitia polisi kwa ajili ya upelelezi au.!
Umesoma hiyo Moving section ambayo ameitumia??

Ndo maana watu wanasomea sheria miaka 4-5 kuja kufanya hayo.
 
Ukisikia jina Fatma....basi matatizo
 
Kwani Kesi hiyo imefunguliwa na DPP hadi afikie hatua ya yeye kusema kwamba hana Nia ya kuendelea na Kesi?
Mtu aliyefungua Kesi Mahakamani ndiye mwenye mamlaka ya kusema kwamba Hana Nia ya kuendelea na Kesi.
Hivi kisheria imekaaje ikiwa shtaka linafungulia kwa mtu ambaye hakuwepo kwenye tukio na wala hakutajwa jina??

Waliofanya hilotukio bado hawajakubali kama walitenda kosa husika je kumtaja huyo ASP hawaoni kua ni kupoteza mda ??

Naomba hili swala lisepelekwe kimhemko tutapoteza.
 
Je, unajua sababu ya kufanya Upelelezi au Uchunguzi wa kijinai??
Nini hasa lengo la Kufanya Upelelezi??

Nakushauri uende shule angalau ukasomee kuhusu suala la CRIMINOLOGY au Criminal Investigation, hata kwa level ya Basic Foundation Course tu inatosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…