carter
JF-Expert Member
- Jan 23, 2009
- 3,664
- 4,259
Mwaka 2017 nilienda Moshi Marangu. Lodge self-contained ilikuwa Tshs. 5000 per night.Malazi hiyo 50k kwa siku ngapi mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwaka 2017 nilienda Moshi Marangu. Lodge self-contained ilikuwa Tshs. 5000 per night.Malazi hiyo 50k kwa siku ngapi mkuu
Those were good all daysMwaka 2017 nilienda Moshi Marangu. Lodge self-contained ilikuwa Tshs. 5000 per night.
Bakuli iyo inaitwa KIDEWAToka napata akili naskia sana neno Kilimanjaro, katika utafiti pia ni vitu vingi sana vina majina hayo. Toka niingie JF watu wanaotoka Kilimanjaro wanatajwa kwa ubaya kwa mazuri pia. Kutokana na mabishano ambayo nimeshuhudia kwenye majukwaa humu kuhusu wachaga na mkoa mzima nikatamani sana ipo siku nitaenda.
TRC warahisiha ndoto:
Nikakumbuka pia kuna usafiri unasifiwa sana kwa bei ndogo na uzuri wake. Nilikuwa free kama siku 7 hivi nikaamua wacha niende Kilimanjaro sina ndugu nitalala guest tu mpaka nione ukweli mana sio kwa misifa hiyo. Wachagga wamekuwa wakijitamba sana kwao kuzuri,makazi bora, nyumba nzuri,[emoji1658] la kutosha hususa mwisho wa mwaka.
Nikachukua Deluxe yangu tar 30 ilikua j5 nauli 23,500 tu. Kwanza pongezi kwa JPM na pole kwa wanaobeza juhudi zake. Ila jamaa anapambana sana, anakosolewa sana kaskazini lakini kawapunguzia sana shida.
View attachment 1674239
Sikuwahi kusafiri na treni umbali mrefu ila niliipenda safari. Nje mandhari nzuri ya kupendeza nchi yetu mradi wa SGR ulivyofikia n.k
Balaa linaanza kwenye treni: nilichoona kwenye treni unaweza kuhisi ndio sherehe au bata la mwaka mpya wenyewe. Watu wa pande zote TZ wamo sikujua kama labda nao wanaenda Moshi mwisho wa mwaka ama la. Watu wanajua kutumia pesa bana,full shangwe kujiachia unaweza kutamani kusikuche. Uzuri wa kwenye treni naamini unaweza kuamua kula mwisho wa mwaka huko tu kwa kusafiri na kurudi nalo.
Baada ya watu kujidunga ifaavyo(kupiga maji) mzozo ukatoke watu wakataka kushikana,kuna jamaa mmoja alikua anaongea lafudhi ya kisukuma alipandisha na madem flan hivi kama machotara. Ile watu kushika na kuita polisi cha kushangaza jamaa alijigamba hakuna mtu wa kumwambia lolote humo ndani. Alikuja polisi lakini jamaa alimdharau sana na kutaka kugombana nae ile dhana ya "unanijua mimi ni nani" yule jamaa aliitumia vizuri na yule polisi kuogopa kweli. Wengi walihisi labda ni usalama wa taifa.
Nafika Moshi saa 12 asubuhi mapema kabisa, stesheni kuna mishe mishe za hapa na pale lakini kwa muda huo maeneo mengine kumepoa.
Nilizunguka baadhi ya mitaa ili kuvuta muda.
Kulipokucha nikaacha kutembea sasa kwenda nje ya mji kidogo japo sikuzunguka wilaya zote ila nitaweka picha na maeneo niliyotembelea tu.
Nilitamani sana kwenda kupanda mlima lakini bajeti yangu haikuruhusu ukizingatia safari sikupanga mapema.
View attachment 1674242
Stendi Moshi asubuhi, kusafi sana.
View attachment 1674244
Karibu na chuo cha Mwenge kwa Dar ni kama Kijichi Mtoni hiyo mijengo.
View attachment 1674245
Barabara ya kwenda Chuo cha Manyamapori Mweka.
View attachment 1674247
Marangu
View attachment 1674248
Kibosho
View attachment 1674254
Maeneo ya Boro.
Ukweli ni kwamba japo hakuna gorofa nyingi, lakini sehemu za watu kuishi zimejengwa vizuri. Nyumba za matope niliona chache sana ila hakuna nyumba isiyo na njia.
View attachment 1674266
Mtori mzuri sana Polisi mes, hii bakuli mpaka sijui inaitwaje(Wachagga mtanisaidia)
Redstone club maarufu na kubwa sana Moshi niliambiwa mwisho wa mwaka hujaa sana.
HITIMISHO: Nataka ikiwezekana nifanye utali wa ndani kila mwisho wa mwaka kwa kwenda mikoa tofauti kujionea mandhari za huko. Nikipata nauli ntaenda Dodoma mwaka huu mwishoni nikaone, ila Moshi ni pazuri japo sikumaliza mkoa mzima, nilitamani kupita kote bajeti yangu ikawa ndogo. Kongole kwa Wachagga, Wapare na Wasambaa mana ndio wengi wapo huko sana kujisifia kwenu sio bure nimeona angalau kidogo.
Kibosho ipi mankaEwaaaa hapo umetenda haki. Kibosho ndo kwetu karibu tena next time.
Nani anauza ardhi kule? Kutafyta bifu na ukoo tuSema kuna kitu nilishangaa luambo makiadi na Dilek mbona hakuna viwanja vya kununua? Niliuza kila sehemu lakini sikupata eneo linalouzwa afu nikaambiwa huko migombani bei ni kubwa sana kuliko hata maeneo mengine ya Dar ni kweli?
Kirima Juu,Kibosho ipi manka
Ooh jamani... nimepajua sana kwasababu ya marehemu Sr. Maria Antoni jamani. Napenda zile source zenu za majii. Rombo hatuna mpk kule juu msituniKirima Juu,
Sr. Maria? Kama namjua vile..kafariki mwaka jana?Ooh jamani... nimepajua sana kwasababu ya marehemu Sr. Maria Antoni jamani. Napenda zile source zenu za majii. Rombo hatuna mpk kule juu msituni
Nimemjibu Kama alivyouliza,na yeye kaleta dharauduuuuuh acha kudharau vijiji vya watu ww
Kajengeni nyumba nzuri kwanza huko dodoma kwenu achen kuishi vijumba vya tembe vya karne ya 12Kila sehemu na mazuri yake na mabaya pia. 2019 angalichungulia darini huko kibosho akaona hayo mafuvu si angalikuwa na story ingine? Sie wagogo tunaweza kuwa na yetu mazuri pamoja na madhambi ya tembele!!!
Walikufukua?Na angalikwenda kwa majirani zenu wa Uru akaona nao pia wanavyofukua si angalizimia?
Ni kweli kabisa ardhi ya UCHAGANI huwez kuinunua Ina bei kubwa,kiuchumi ukiona sehemu ardhi Ina bei kubwa ujue kuwa sehemu hiyo ilishaendelea tangu zamaniSema kuna kitu nilishangaa luambo makiadi na Dilek mbona hakuna viwanja vya kununua? Niliuza kila sehemu lakini sikupata eneo linalouzwa afu nikaambiwa huko migombani bei ni kubwa sana kuliko hata maeneo mengine ya Dar ni kweli?
Ni kweli ndio maana ripoti ya serikali inatuonyesha Kilimanjaro Ni mkoa wa pili watu wake kuishi maisha bora,makaz, miundombinu kwa 90%Hayo mambo yapo kwa makabila mengi. Ila uzuri wa mandhari vijiji vya Moshi huwezi linganisha na mikoa mingine. Ni ukweli usiopingika
Mkoa wa kwanza ni upi mkuu?Ni kweli ndio maana ripoti ya serikali inatuonyesha Kilimanjaro Ni mkoa wa pili watu wake kuishi maisha bora,makaz, miundombinu kwa 90%
Ripoti ya serikali inatuonyesha 90% ya watu wa killinanjaro wanaishi maisha boraTatizo kubwa tunapenda kugeneralise, si wote humu nyumbani ni bora vijijini au hata mijini. Asilimia kubwa hapa wanaotamba wanatambia za majirani pengine hata wewe mrembo
Usiwe na wivu hivyoSasa Mchaga kamzidi Mhaya misifa kila Mtu anajua wachaga ni watafutaji pia watu wa maendeleo punguzeni basi Misifa mkujimwambafa kumezidi tunajua uko mbali .
Mkoa wa kwanza ni Dar 92%Mkoa wa kwanza ni upi mkuu?