Mrejesho: Baada ya Safari ya Dar kukutana na asiyejulikana

Mrejesho: Baada ya Safari ya Dar kukutana na asiyejulikana

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Wakati nipo ndani ya basi likichanja mbuga muda huo nikipata mawazo ya wadau mbalimbali ya wana-jf kuhusu kwenda kukutana na mwanamke kwa mara ya kwanza ambaye tulifahamiana kwenye mitandao ya kijamii,pia nilikuwa natafakari maoni ya wanajf hasa kukutana Lodge kwanza badala ya kujipeleka nyumbani kwake moja kwa moja

Hata hivyo nilikata shauri nikaamua niende moja kwa moja nyumbani kwake kama ni kufa ngoja nikafie kwenye papuchi,mbona wengine wanajiua kwa sababu ya papuchi

Muda wa SAA 4:30 usiku nilifika stendi kuu ya mabasi Ubungo,mwanamama alikuwa tayari alishafika nusu SAA kabla

Baada ya kushuka nilimpigia sim nikamwelekeza upande niliopo na nguo nilizovaa na nimesimama karibu na nini,mara nikaona mwanamke anaibuka,kwenye mawazo yangu nilikuwa nafikiria atakuwa mama mwenye age kidogo kumbe alikuwa ni mwanamke mdogo ndo ameingia 30,mwenye umbile la kuvutia na sura yenye mng'ao maji ya kunde isiyotumia mkorogo

Kwanza wakati ananipokea alinipokea kawaida,kwa sababu ya ile ugeni

Basi akanipeleka kwenye gari lake ,tukaingia tukaanza safari,ila mawazo ya napopelekwa na ni usiku yalikuwa yananisumbua na vile vituko vya wanamemba nikawa nawaza zaidi

Huku tukipiga stori kwa mbali kwa sababu ya ugeni na kujizuia kujionyesha kuwa unajua kuongea na usiye mjua

Baada ya nusu SAA tulifika kwake,akapiga honi,mlinzi wa geti kafungua ,ile nyumba yenye geti kubwa kiasi kile niliwaza" hapa itafika kesho nipo salama kweli" ila nikapiga moyo konde liwalo na liwe

Tulipoingia ndani tukashuka,akaniambia karibu ndani,tukaingia ndani,moja kwa moja sebuleni tukakaa,akaniletea kinywaji,nikaanza kunywa ila kwa tahadhari sana ingawa muda huo mwili ukawa kama jiwe kwa hali ile ya kuwa na wasi wasi

Muda mchache akaingia jikoni akapika baada ya muda akawa ameleta chakula,basi nikala,muda huo tunapiga stories moja mbili tatu

Nikataka nijue anaishi na nani kwenye ile nyumba ambayo inaonekana ni kubwa,akanambia" anakaa na Dada wa kazi na mwanae wa kike ana miaka 3 ila wamelala,nimeona sio vizkuri niwaamshe ,ila kesho mtaonana",nikasema sawa

Nikataka nijue baba wa mtoto vip au ana mpenzi ,ingawa alikuwa ameisha niambia awali,ili nipate uhakika zaidi
Akanambia"najua utakuwa na wasi wasi ila nakuhakikishia upo sehemu salama usiwe na wasi wasi hata kidogo,hayo mengine nitakuhadithia kesho," Sikutaka kumlazimisha sana kunambia kuhusu hizo stories

Baada ya kile chakula ni alinipeleka chumbani kwake akanambia karibu,nikasema asant,akanionyesha bafu niiingie nioge,kisha akanionyesha dressing table yake nikimaliza kuoga nikajipake mafuta baada ya hapo akatoka

Baada ya kutoka nikawa nimekaa kwenye kiti pale nawaza,hapa kuna usalama kweli,na anaenda wapi,

Ila baada ya dakika chache nikanyenyuka nikafunga mlango nikaingia bafuni nikaoga,nikamaliza nikajipaka mafuta ,nikamtumia SMS nimemaliza ,akaja akashusha net,akanambia karibu ulale,mara simu yake ikaita akapokea nikasikia mwitikio wake "Amefika salama,aya " akakata sim

Duh, nikahisi mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi, hapa leo sijui,akanambia "Ni rafiki yangu ananiulizia kama umefika maana nilimwambia kuna mgeni atakuja kunisalimia" Nikasema sawa

Akanambia "Hapa ni kwako ,kuwa free,ingia ulale mi tutaonana kesho asubuhi" Nikasema Duh,mama unaenda wapi tena,akasema ",No nipo siende popote ila naenda kulala na mwanangu,asubuhi nitakuja kukuona,sikubisha sana ila mawazo yakawa yananijia sasa ,hapa ni kwa nani,na mwanae analala kwa nani,hapa kuna usalama mweli ,au kafuata majamaa yaje kunimaliza,niliwaza bila kupata jibu

Alipotoka nikanyenyuka nikaenda nikafunga mlango,nikavaa nguo kama nilivyokuja,nikazima taa,nikaingia kulala,hamna cha usingizi,ni kuwaza what will happen in this night,na sasa ni SAA saba na 37

Sikulala kwa kweli niliwaza huku nikiperuzi mitandao mbalimbali ya kijamii

SAA 12 na 30 hivi kausingizi kakaanza kuja,nikasikia mlango unagongwa,kuangalia saa ni SAA 12 nikasema kumbe kumekucha,ile hali ya usalama nikahisi kuwepo ila sio sana ,ila nikajipa matumaini

Nikaamka nikafungua mlango,alikuwa ni mwanamama,akiwa kwenye night dress yake akaingia,akanisalimia ,tukakaa pale kitandani,pole na uchovu na nk

Tukapiga story za hapa na pale ila ,tukaja kwenye hili,akanambia" Dear samahani kwa kutolala na wewe kwa usiku wa jana,kwa sababu mbili,1,ulikuwa umechoka na safari maana ulikuwa umetoka mbali sana
2, Mimi na wewe hatujuani,hatuna kipindi kirefu tangu tufahamiane,na pia hujui historia ya maisha yangu na wewe hujui nimewahi kukutana na nani na wapi na yukoje,hivyo naomba baada ya kunywa chai kwa ridhaa yako,kwa moyo wako wa hiari twende kituo kimoja cha afya tukacheki afya zetu ili tujue hali zetu

Nikasema poa,nikaingia kwenye dimbwi lingine la mawazo ,Duh hapa nimekubali je nipo salama? Nikapiga picha ya niliowahi kudate nao ila nikasema basi liwalo na liwe

Baada ya dakika 10 akaniita kunywa chai,muda huo na Dada wa kazi na mwanae wakawa wameisha amka,mama yao akawambia msalimie baba yenu,salam za shikamoo baba zikatua kwangu nikaitikia

Tulipomaliza tukaenda kituo kimoja cha afya ,tukacheki afya zetu,sikuamini kuwa wote tulikuwa salama,ila kama alinitega huenda yey e alikuwa hayupo salama huenda alihonga majibu na alikuwa amepanga mchezo sijui,ni mengineyo,

Badae tukarudi home,hadi chumbani,tukavunja amri ya mungu ,mwanamama akaenjoy kazi ya mwanaume wa mkoani,na sasa nipo njiani naelekea kwangu,na wiki ijayo kaniahidi kuja kwangu

Kuhusu na ex wake alinieleza full story huku nikifanya Diagnosis ya nguvu ya maelezo yake basi kwa aslimia 70 nikakubaliana na maelezo yake ,30 nitendelea kuzifanyia uchunguzi

Sikupata dhoruba yoyote,nashukuru kwa maombi yenu
 
mwanamama akaenjoy kazi ya mwanaume wa mkoani
hadiii hapoo sina la kusema umetuwakilisha vyema wanaume wa mkoani inabidi siku ukifuata mwingine Kigoma nitaarifu nikuandaliee mihogo na mafuta ya mawese kwa ajili ya kazi kakaa
 
Back
Top Bottom