Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,962
- 70,576
Macho mdiliko na wangari naomba kuwajibu kwa namna ambavyo mmetafsiri ninyi na nilitakiwa nisiwajibu chochote kwa sababu ya ufinyu wa mawazo yenu ila kwa sababu leo ni jumapili nimepoz ngoja nipoteze mda kuwajibu hili.
Kwanza kabisa mdau aliweka uzi kutoa ushuhuda wa kile anachokifanya naweza kusema uzi huu haukuwa na lengo la kumpiga mtu kwa sababu tayari aliwahi omba kupata utaratibu namna ya yeye kwenda huko kufanya biashara hii,
Biashara hii kwa wale walioko maeneo ya migodin wataelewa nini naongea na hasa kwa upande wa dhahabu ni biashara ambayo ukiwa makini na ukabahatika kulenga eneo lina dhahabu unaweza amka kwenda chimbo huna hata mia na ukarudi una mamilioni hili sio hadithi na tumeshudia wengi, lakini biashara hii ukiingia kichwa kichwa hata kama ungekuwa unamiliki ndege sita unaweza poteza zote na ukabaki masikini.
Kwa maelezo ya mleta uzi kuwa yeye ananunua tayari ikiwa imechomwa na kuiuza kwa makota na wao wanapeleka sokoni hili lipo wazi kuna faida tena ya wazi bila kificho ila ni mbaya kununua ile haijachomwa hapo unaweza nunua udongo.
Hivyo kwa mtaji wake wa milioni tano na kusema kwa mwezi kaingiza faida ya milioni moja mbona ni ndogo sana hiyo kwa biashara ya dhahabu tena hapo anaenda taratibu na kwa umakini mkubwa asije kupigwa.
Kuhusu mimi ndama dume kuomba mtu mwenye machine na sio pesa hili kwa akili yenu fupi mkadhani mtu atapigiwa wapi labda kwa sababu sisi hatuendi kuchimba sisi tunaenda kuwapimia watu maeneo na kulipwa chetu,
Pili unaweza kujiuliza kuwa kma machine hii ingekuwa na faida kiasi hicho watu wengi si wangekuwa nayo? Naomba nikujibu hivi kuwa asilimia kubwa ya wachimbaji hawana shule hapa nazungumzia wachimbaji wadogo na hivi vifaa kwao hawana utaalamu navyo hivyo wanachimba kwa kubuni na kudhani lakini hawana uhakika na kile kilichopo so hapa ndio sehemu geologist hupiga pesa ukipima eneo na mchimbaji akaja kuchimba kapata kitu basi juwa wote watahamia kwako kwa gharama yeyote ili ukawapimie maeneo.
Lakini kama hujui mazingira ya migodin yakoje na hukawahi kufika na kuona na haiba ya watu au wachimbaji wadogo wanahitaji nini basi unaweza dhani ni uongo ila ukweli ni kwamba watu wametoka na kunawiri zaidi nyie endeeleeni kucheza forex tu .
Nadhani umejimix...mie sijamsema mtu tapeli...! Nioneshe wapi nimesema Kuna utapeli ..kila la heri mkuu...! ..