Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Kweli kaka umepambana lakini naomba tuwasiliane namba 0629696362
 
Wakuu December hii nitaleta mrejesho wapi nimefika. Na mwisho kabisa ilikuwa kufikia levo ya kuwa dealer. Guys keep informed.... Kuna cha kujifunza kwenye safari yangu hii. Kwahiyo June ya 2022 utakuwa ni mrejesho wangu wa mwisho. Tuombe uzima kwa mola!!
 
Tunakushukuru sana kiongoz kwa mchango wako. Je vipimo vya kutambua purity ya dhahabu ni bei gan?

Sent from my SM-J810F using JamiiForums mobile app
 
Unachosema ni kweli kuna wachangiaji wachache kwenye NYUZI za aina hii, LAKINI mimi nadhani sababu mojawapo ya uchache wa uchangiaji ni UGUMU WA WALETA NYUZI kujibu maswali au kutoa maelezo kwa wana JF wanao uliza ili kujua nyendo zote ikiwa ni pamoja na mafanikio na changamoto alizokutana nazo mtoa UZI! Hali kama hii inakatisha tamaa kuchangia au kuuliza maswali kwa nia na lengo la kutaka kujua! Kwa mfano, kuna mwana JF kamuuliza mleta UZI yuko chimbo gani, na mkoa gani!? Yeye kanyamaza kimya. Katika hali hii wewe mwingine utauliza kweli!? TUJISAHIHISHE kama tunataka kusaidiana KIMAWAZO humu JF.
 
Mkuu nipo Chunya Mbeya.
mcrounmj hebu tupe details za mchakato wote hasa hasa kwenye ununuzi wa dhahabu wewe kama BROKER na uuzaji wake na pia ni masoko yapi unatumia na ikiwezekana tupe experience yako ya namna ulivyo tapeliwa na baadaye kuinuka kwani ulisema kuwa hadi unaingia machimboni ulikuwa na balance ya 2M/-! Je hiyo ndiyo ilikufikisha kwenye 20M/= ya sasa AU ILIKUWAJE!?
 
Yes, safi kabisa kwa maelezo ya KISOMI kutoka kwa MSOMI mpambanaji! Keep it up mcrounmj!
 
Ila Master Dealer anaweza kupeleka popote ikiwa ni pamoja na Kenya ingawa nadhani masharti ya hiyo leseni ni magumu kidogo au siyo Wangari Maathai?Saidia katika hili.
 
"DHAHABU ILIYOPEMBULIWA" una maana ni ile safi au ni ile ya wachimbaji wadogo wadogo ambayo haijasafishwa!? Nifafanulie Msomi wangu!
 
PENYE NIA PANA NJIA NA MUNGU AKIWA MBELE YA YOTE.
 
Hakika wewe umetema pointi za maana na zinazoonyesha uhalisia wa biashara tofauti na wengi wetu hupenda kusikia stori za vijiweni, maake kama faida ingekuwa kubwa sana tunavyoaminishwa basi wengi wangefanya.
Mimi nadhani HOJA hapa siyo faida ya hii biashara, nadhani HOJA hapa ni MTAJI na UDIRIKI. Hivi ni vitu au mambo muhimu sana kwa mtu yoyote kuingia kwenye hii biashara. Ukiwa na MTAJI mzuri unaweza kununua mzigo mkubwa na hivyo kupata faida kubwa bila kujali eti "biashara hii ina faida ndogo". Faida ndogo ndiyo inapelekea kupata faida kubwa kama una MZIGO mkubwa ambao utatokana na MTAJI na UDIRIKI wako wa kuwekeza.
 
Ila kuna maswali madogo madogo hujajibu! Kwa mfano, soko lako ni wapi? Ni hapo hapo Chunya au nje ya hapo? Na range ya selling price inakuwaje na mwisho nikitaka kuanza kazi kama Broker, nahitaji kuwa na VITENDEA KAZI gani muhimu ukiacha pesa? Wengine wanasema ni vizuri uwe na mzani na hata mashine ndogo ya kujua hii ni dhahabu au shaba n.k n.k. hii ikoje. Asante tena Msomi wangu.
 
Nimeshaweka kambi mkuu,kusubiri mrejesho😃
 
Soko langu ni chunya.... Porini tunanunua kuanzia themanini hadi tisini kwa gram, sokoni tunauza kwa laki mpaka laki na elfu tano kutegemea na asilimia ya dhahabu
 
Kuhusu vitendea kazi ni scale ya kupima uzito wa Dhahabu tu Basi. Kuhusu kuuziwa Dhahabu feki macho yataijua tu. Na saivi Dhahabu zinanunuliwa masokoni hivyo akileta mteja hautakuwa peke yako maana zipo ofisi nyingi hivyo unauliza wenzako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…