Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Nilisoma shule ya kupitia kwenye umande halafu dawati mnakaa watoto wanne. Kabla ya kuingia darasani ilikuwa kila mtu afagie mraba wake ambao prefect atapita kukagua kuwa mraba umefagiliwa vizuri ndipo mtoto anaingia darsani. Zaidi ya nusu ya darasa walikuwa hawana viatu.
 
Pole sana mkuu, fanya kile kiko ndani ya uwezo wako. Watoto wangu wanasoma private kwani nazijua changamoto lukuki za public school.
 
Tatizo ni kutaka kuwapangia wengine cha kufanya, haiitaji kuwa milionea kumpeleka mtoto wako shule nzuri, ambazo nyingi ni around 3M kwa mwaka. Wengine tunaishi maisha tuliyonayo kwa sababu wazazi wetu walitusomesha. Watoto wangu wanasoma na watasoma shule zinazoeleweka. Wewe pambana na hali yako tu mkuu, huku mikoani matajiri wenye elimu ndogo ndio wanainvest sana kwenye elimu ya watoto wao.
 
Safi sana mkuu hizi English Medium ni ubabaishaji tu. . Wanao wapeleka watoto huko acha waendelee kupigwa
Mara nyingi makuzi ya mtu uamua maisha atakayoishi, ndio maana hekima ya kawaida kuna mambo huwezi pangia watu wayafanyeje. Huna haja ya kushupaza shingo kutetea hicho unachokiamini kwani maisha halisi hayatakuwa hivyo unavyofikiri kamwe. Heshimu wanaopeleka watoto wao shule wanazoona ni sahihi kwa future yao.
 
Huku ni kuyumba kiuchumi tu hakuna kingine.
Ndomaana akasema tuje tufarijiane. Mara zote mtu mwenye matatizo au majanga anapewa faraja.
Your browser is not able to display this video.
 
Umasikini ni tatizo na Watanzania wanafurahi kuwa masikini na wanautukuza
 
safi sana mkuu coz ulijifunza changamoto za maisha at that tender age
 
Diamond alisoma Feza?.. Konde Boy?. Connection ni akili na ujanja wa mtu mwenyewe binafsi wala haina uhusiano wowote na lugha aliyo tumia kusoma shule.


Wema alisoma Academy ila company yake ni kina Aunty Ezekiel na Gigy Money walioishia form two Kayumba.


Hamisa Mobetto kasoma st.kayumba tena form four leaver lakini ana connection na viongozi wakubwa nchini plus Artists wakubwa duniani akina Rick Ross etc.

Mange Kimambi kasoma Arusha school plus international schools ila kazi yake ni umbea ambao ulitakiwq kufanywa na akina Mwajuma wa Tandale pale.

Usiishi kwa kukariri mkuu.

Ishi kulingana na uhalisia wa nyakati zilizopo
 
Wacha tujifariji tu.

Hela ya ada ya mtoto wangu
Zamani nilikuwa napiga mahesabu nikipata kiasi kadhaa tu nafanya biashara.

Eti sasa hivi ndio pesa ya ada ya mtoto...Kum*nyok ELIMU.✍🏻
 
Primary sio eneo la kucheza nalo uko sahihi
Ndio.maana inaitwa elimu ya msingi

Msingi ukiwa mbovu huko mbele kilio
Kweli kabisa Mkuu mimi mwenyewe shahidi , ninao uwezo Mkubwa sana kwa hilo Sina shaka ila elimu ya msingi nilipiga kayumba na niseme ukweli lugha ilikuwa kikwazo kikubwa sana ata baada ya kumaliza chuo kikuuu na kuajiliwa , unakuta kwa uwezo ulionao unaaminiwa na kupewa majukumu makubwa Kuna wakati unapangiwa vikao na board of directors wengine wazungu unapima maji unaona kabisa hapa - hiki ni kina kirefu , ilinisumbua sana ikabidi niende British school pale mwenge kujipiga msasa , si haba kwa sasa Niko vzr naweza nikapiga umbea kwa ung'eng'e , kwahiyo guys msipuuzie msingi ni kitu cha kuzingatia sana kwa mtoto.
 
Kama uwezo wa kipato ni mzuri, private school ni mahali sahihi kupeleka mtoto, shule za uma haswa kwa primary na olevel changamoto ni nyingi sana sana

Hizo unazo ziita changamoto ndio zinazo wafanya wazazi wengine wawapeleke watoto wao kwenye shule hizo ili waanze kujifunza kuhusu changamoto za maisha tangu wakiwa wadogo.

Hizo changamoto ni sehemu ya makuzi kwa mtoto pia.


Binafsi siwezi mpeleka mtoto wangu sehemu ambayo haina changamoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…