Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Daah... Haya mambo ya mtu kipato cha chini kujitutumua kusomesha watoto English medium yanachangamoto zake.
Jirani yangu hapa kafirisika kauza ardhi hadi mlangoni kisa watoto wasome private.
Matokeo wakwanza kamaliza form 4 yupo nyumbani wawili bado anapambana nao ila hali tete kwelikweli
 
Wewe tajiri networth yako ni how much Million Dollars ? Tuanzie hapo mkuu
Imegeuka me versus you sasa?

Wewe watoto wako wapo Kayumba kwa kukimbia ada ya 4mil mimi watoto wangu wapo shule hizo ulizokimbia,na sio ya 4mil ni multiple ya hiyo 4mil,yaani mara kadhaa za kutosha

Kwahilo tu sina haja ya kutaja networth...na wanaume hua hatutaji networth,unaona tu action then wewe mwenye kuuliza maswali unapiga hesabu kwenye ubongo wako mwenyewe!
 
This is what I was talking about
 
Kuna shule mtu anamaliza wote wanakuwa bodaboda
 
Basi kumbe wewe ni mbumbumbu wa pesa. Huna elimu ya pesa. Huna mahusiano mazuri na hela...

Ngoja nikusanue kitu ndugu yangu. Nikupe elimu ya mtaani kidogo kuhusu pesa..

Mjanja sio yule anae tumia ( spend) pesa nyingi ila ni yule anae ( tunza) pesa nyingi.

Mfano; kama Mimi mshahara wangu ni shilingi milioni tatu kwa mwezi ila matumizi yangu ni sh laki TANO kwa mwezi halafu natunza benki milioni mbili na laki tano kila mwezi.


Ila wewe mshahara wako ni shilingi milioni kumi kwa mwezi ila matumizi yako ni sh milioni tisa na laki nane kwa mwezi.


Baada ya miaka kumi Mimi nitakuwa tajiri wewe utakuwa masikini. Nktakuajjri Mimi.

So wewe kuspend milioni nane kwa mwaka kulipia kitu ambacho unaweza kukipata kwa sh laki moja kwa mwaka ni shobo zako tu na.umbumbumbu/ulimbukeni wako kwenye pesa.

Huna mahusiano mazuri na pesa. Pesa haitumiki kizembe namna hiyo.
Ungeniambia hiyo milioni nane unaitunza kila mwaka ninge ona unafanya kitu ila kumbe una spend? Khaaa

Hapo mjanja ni huyo ambae unaweka hela kwenye akaunti yake na sio wewe
 
Sasa huoni we ni masikini?
Unafanyaje ujenzi kwa miaka yote hiyo?
 
Kusomesha English Medium ni ushamba tu.

Tambua kwamba mwalimu wa kwanza na mwalimu mkuu wa mwanao ni wewe mzazi.

Kama mzazi umesoma na ulikuwa unayamudu masomo hakikisha unakuwa mwalimu kwa mwanao.

Akiwa shule ya msingi ndo msingi wa yote.

Elimu ya Tanzania imesimama katika nguzo kuu mbili. Nguzo hizo ni Hisabati na Kiingereza.

Mwanao akiwa shule ya msingi hakikisha unakagua madaftari yake ya Hisabati na Kiingereza. Hakikisha unampa mazoezi (homework) za hisabati na kiingereza na kwamba hakikisha muda wote yuko sura za mbele kwenye mtaala wa hisabati na kiingereza ili akienda darasani iwe ni marudio.

Akihitimu darasa la saba na alama A ya hisabati na A ya kiingereza hapo kazi umeshamaliza katika suala zima la masomo. Ataelewa masomo mpaka chuo kikuu. Hapo sasa utabaki na shughuli ya kukabiliana na changamoto za balehe.
 
Medium nyingi ada haivuki 3mil kwa mwaka, ambazo ni sawa na 300,000 kila mwezi
 
Unachukualia sampo space ya watu 3 kwenye kundi la wanafunzi zaidi ya milioni 14 walio mashuleni mwaka huu
 

Barikiwa sana mkuu.

Wyatt Mathewson soma hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…