Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Daah... Haya mambo ya mtu kipato cha chini kujitutumua kusomesha watoto English medium yanachangamoto zake.
Jirani yangu hapa kafirisika kauza ardhi hadi mlangoni kisa watoto wasome private.
Matokeo wakwanza kamaliza form 4 yupo nyumbani wawili bado anapambana nao ila hali tete kwelikweli
 
Wewe tajiri networth yako ni how much Million Dollars ? Tuanzie hapo mkuu
Imegeuka me versus you sasa?

Wewe watoto wako wapo Kayumba kwa kukimbia ada ya 4mil mimi watoto wangu wapo shule hizo ulizokimbia,na sio ya 4mil ni multiple ya hiyo 4mil,yaani mara kadhaa za kutosha

Kwahilo tu sina haja ya kutaja networth...na wanaume hua hatutaji networth,unaona tu action then wewe mwenye kuuliza maswali unapiga hesabu kwenye ubongo wako mwenyewe!
 
Daah... Haya mambo ya mtu kipato cha chini kujitutumua kusomesha watoto English medium yanachangamoto zake.
Jirani yangu hapa kafirisika kauza ardhi hadi mlangoni kisa watoto wasome private.
Matokeo wakwanza kamaliza form 4 yupo nyumbani wawili bado anapambana nao ila hali tete kwelikweli
This is what I was talking about
 
Tatizo la kusoma st kayumba unakuwa huna strong connections unless ziwe zile special schools. Yaani utajikuta unamaliza lakini marafiki zako wengi watakuwa katika positions ambazo hazimsaidii mtu kati yenu kuondoka katika poverty circle

Yaani circle nzima ya marafiki si ajabu ukakuta huna contact ya kukuambia kuna nchi flani ulata ina fursa flani
Kuna shule mtu anamaliza wote wanakuwa bodaboda
 
Imegeuka me versus you sasa?

Wewe watoto wako wapo Kayumba kwa kukimbia ada ya 4mil mimi watoto wangu wapo shule hizo ulizokimbia,na sio ya 4mil ni multiple ya hiyo 4mil,yaani mara kadhaa za kutosha

Kwahilo tu sina haja ya kutaja networth...na wanaume hua hatutaji networth,unaona tu action then wewe mwenye kuuliza maswali unapiga hesabu kwenye ubongo wako mwenyewe!
Basi kumbe wewe ni mbumbumbu wa pesa. Huna elimu ya pesa. Huna mahusiano mazuri na hela...

Ngoja nikusanue kitu ndugu yangu. Nikupe elimu ya mtaani kidogo kuhusu pesa..

Mjanja sio yule anae tumia ( spend) pesa nyingi ila ni yule anae ( tunza) pesa nyingi.

Mfano; kama Mimi mshahara wangu ni shilingi milioni tatu kwa mwezi ila matumizi yangu ni sh laki TANO kwa mwezi halafu natunza benki milioni mbili na laki tano kila mwezi.

Ila wewe mshahara wako ni shilingi milioni kumi kwa mwezi ila matumizi yako ni sh milioni tisa na laki nane kwa mwezi.

Baada ya miaka kumi Mimi nitakuwa tajiri wewe utakuwa masikini. Nktakuajjri Mimi.

So wewe kuspend milioni nane kwa mwaka kulipia kitu ambacho unaweza kukipata kwa sh laki moja kwa mwaka ni shobo zako tu na.umbumbumbu/ulimbukeni wako kwenye pesa.

Huna mahusiano mazuri na pesa. Pesa haitumiki kizembe namna hiyo.
Ungeniambia hiyo milioni nane unaitunza kila mwaka ninge ona unafanya kitu ila kumbe una spend? Khaaa

Hapo mjanja ni huyo ambae unaweka hela kwenye akaunti yake na sio wewe
 
Nilisimamisha ujenzi kwa takribani miaka 6,tokea nimechukua maamuzi magumu ya kumpeleka mtoto wangu kayumba ujenzi unaenda kwa kasi ya ajabu,hili kwa wale wazee wa kukwapua nadhani hawatanielewa,ila kwa sisi tunaotegemea mshahara wa mwezi watajua naongea nini.Kizuri zaidi mwanangu ni kicwa na huku aliko bado anawapelekesha,kwa hiyo na mshukuru Mungu kwa kunipa maamuzi sahihi...
Sasa huoni we ni masikini?
Unafanyaje ujenzi kwa miaka yote hiyo?
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakao nipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa lako tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Kusomesha English Medium ni ushamba tu.

Tambua kwamba mwalimu wa kwanza na mwalimu mkuu wa mwanao ni wewe mzazi.

Kama mzazi umesoma na ulikuwa unayamudu masomo hakikisha unakuwa mwalimu kwa mwanao.

Akiwa shule ya msingi ndo msingi wa yote.

Elimu ya Tanzania imesimama katika nguzo kuu mbili. Nguzo hizo ni Hisabati na Kiingereza.

Mwanao akiwa shule ya msingi hakikisha unakagua madaftari yake ya Hisabati na Kiingereza. Hakikisha unampa mazoezi (homework) za hisabati na kiingereza na kwamba hakikisha muda wote yuko sura za mbele kwenye mtaala wa hisabati na kiingereza ili akienda darasani iwe ni marudio.

Akihitimu darasa la saba na alama A ya hisabati na A ya kiingereza hapo kazi umeshamaliza katika suala zima la masomo. Ataelewa masomo mpaka chuo kikuu. Hapo sasa utabaki na shughuli ya kukabiliana na changamoto za balehe.
 
hata English Medium hakuna connection. Connection unazo zizungumzia wewe zipo international kama IST. Hata hivyo kiuhalisia hazipo kwa sababu wanao soma huko wengi wametoka familia zinazo ishi kizungu ( kibepari) na ubinafsi.

St. Kayumba utapata network kubwa kwa sababu mnasoma watu wengi. Unlike English Medium darasa moja watu wanane hakuna connection yoyote ya maana.

Usisahau mkuu asilimia kubwa ya wazazi wanao somesha watoto wao hizo English Medium ni mahohehahe tu wenye hela za mawazo ambao hufuata mkumbo na kujionyesha kwamba na wao wanaweza kusomesha watoto English Medium lakini kiuhakika hawana lolote la maana kwenye maisha yao..

Wanaosomesha watoto English Medium ni masikini tu ambao wameamua kujipa matumizi ya sio ya lazima sawa na mfanyakazi mwenye mshahara wa laki nne ambae amenunua iPhone ya milioni mbili baada ya kujibana kwa miezi mitano.

English Medium ni Kayumba ambazo zinafundisha kwa KIINGEREZA.
Medium nyingi ada haivuki 3mil kwa mwaka, ambazo ni sawa na 300,000 kila mwezi
 
But the evidence says no. Uhalisia unaonyesha watoto walio soma kayumba ndio wanajiamini zaidi kwenye maisha kuliko hao wa st. English Medium.

Akina Diamond, Konde Boy, Shilole wote wamesoma kayumba ila wana confidence kuliko.

Halafu hivi sio nyie mnaosemaga watu ambao hawajasoma kabisa ndio wana uthubutu kuliko wasomi?
Unachukualia sampo space ya watu 3 kwenye kundi la wanafunzi zaidi ya milioni 14 walio mashuleni mwaka huu
 
Kusomesha English Medium ni ushamba tu.

Tambua kwamba mwalimu wa kwanza na mwalimu mkuu wa mwanao ni wewe mzazi.

Kama mzazi umesoma na ulikuwa unayamudu masomo hakikisha unakuwa mwalimu kwa mwanao.

Akiwa shule ya msingi ndo msingi wa yote.

Elimu ya Tanzania imesimama katika nguzo kuu mbili. Nguzo hizo ni Hisabati na Kiingereza.

Mwanao akiwa shule ya msingi hakikisha unakagua madaftari yake ya Hisabati na Kiingereza. Hakikisha unampa mazoezi (homework) za hisabati na kiingereza na kwamba hakikisha muda wote yuko sura za mbele kwenye mtaala wa hisabati na kiingereza ili akienda darasani iwe ni marudio.

Akihitimu darasa la saba na alama A ya hisabati na A ya kiingereza hapo kazi umeshamaliza katika suala zima la masomo. Ataelewa masomo mpaka chuo kikuu. Hapo sasa utabaki na shughuli ya kukabiliana na changamoto za balehe.

Barikiwa sana mkuu.

Wyatt Mathewson soma hiyo
 
Back
Top Bottom