Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

T
Yes angalau sio hizi za leo yani mtoto afundishwa English kwa kiswahili.

"Watoto leo tunajifunza kuhusu tense.
Zipo tense za aina tatu. Kuna past tense, present tense na future tense"
Ndo nikalipe milioni hivi kweli? Tuheshimiane tafadhal
Tafuta hela uache makasiriko.
Maskini mnafarijiana au sio. Waza madogo upate kidogo waza makubwa upate makubwa. Somesheni watoto shule bora ni haki yao ya msingi.

Sitaki povu
Yani mzazi ni mjinga anataka na vizazi vyake vibaki kwenye ujinga.
 
Kama pesa hipo muwache mtoto anasomea kwenye shule wanayo keti darasani wanafunzi 45 na kila mtoto na kiti chake na meza

Kila choo kina bomba la mja na bafu safi uji wa ulezi asubuhi kila mala mtoto yuko safi kila likizo mzazi unamfuata mwanao na gali safi na baada ya likizo unamludisha hiyo ndio kazi ya pesa

Kama huna kama mimi muwache mtoto asome kayumba darasa 1 wanafunzi 100 wanaketi chini njaa yake kila siku saa 4 foleni ya mihogo ya kukaanga na kachri

Shule yenye watoto 800 matundu 10 ya vioo kabla ya mtoto kulifikia tundu anaanza kukutana na mkojo mita 5 na vinyesi kuta zote zime tapakaa vinyesi maji hakuna kila asubuhi mtoto lazima aende na kudumu cha lita 3 za maji na ufagio jua lake mvua yake kulala kwake saa 3 kuamka saa 11 kuwai daladala akipata bahati konda anampakia au anasalia kituoni mpaka saa 2 kufika shuleni 3 asubuhi kwa wakazi wa dar sisi mikoani mtoto yeye na baisikeli kila kukicha kilometa 5 mpaka 3


Wakitoa mchango wa unga na mchele na maharagwe hili wale shuleni chakula chote wanakula walimu chagua wewe mtoto wako umpeleke wapi
Tofauti kubwa kati ya Kayumba na Shule binafsi, wale wa Kayumba wanaenda shule kukua wakati wenzao wanaenda shule kusoma.
 
Mkuu ni a nice story,kama wewe ni mtu wa kujifunza unaweza kujifunza kitu.My own story kwa watoto wangu is as follows:
1.STD I-VII-Shule za kawaida.
2.Form I-IV -Private Schools
3.Form V-VI-Government Schools
4.Katika watoto wangu ambao nimewapitisha Shule hizo,Wawili wamemaliza MSc.Mmoja Mzumbe University yuko Bank,na mwingine UDSM naye yupo Bank.Mtoto mwingine
amemaliza Muhimbili ni Surgeon.Watoto wengine wawili wamemaliza SUA wana BSc.Agri.Business na wote ni employed,mmoja yuko Bank,mwingine yupo World Vision.Mtoto mwingine amemaliza Second Year IFM anakwenda Third Year,huyu anachukua Economics and Finance.Wa mwisho amefaulu kwenda Form V atachukua CBG(Chemistry,Biology and Geography).So you see,obviously kutopitia Shule za English Medium haijawaathiri kabisa,na wameniambia categorically,baba,it is wastage of resources kuwapeleka watoto English Medium Schools,na nime-prove it first hand.
CHAI
 
upo sawa watoto wangu wa kwanza na wapili kayumba mpaka chuo kikuu. wa tatu mwezi huu form 5 kayumba huko huko.. wa nne yupo la 7 anamaliza muda mfupi ujao maendeleo yake sio mabaya na inshallah atafaulu. huko medium sitaki hata kusikia!
"Ukiona Elimu ni gharama basi jaribu ujinga"
 
Mkuu ungesema umewatoa boarding school na kuwaleta nyumbani hapo ningekupongeza sana kwakua mtoto kukaa Karibu na wazazi wake hata katika age ya 0-14 ni muhimu sana kwa ustawi wa akili ya mtoto,ukakamavu n.k
Lakini ww unajisifu kuwatoa kwenye mwanga na kuwaleta kwenye Giza kwa faida za kiuchumi tuu hapo umefeli
 
Mkuu ungesema umewatoa boarding school na kuwaleta nyumbani hapo ningekupongeza sana kwakua mtoto kukaa Karibu na wazazi wake hata katika age ya 0-14 ni muhimu sana kwa ustawi wa akili ya mtoto,ukakamavu n.k
Lakini ww unajisifu kuwatoa kwenye mwanga na kuwaleta kwenye Giza kwa faida za kiuchumi tuu hapo umefeli
Na amefeli pakubwa sana
 
Kipindi naanza maisha, nilimshirikisha jamaa yangu nilitaka kununua kisabufa. Bajeti ilikuwa 150k. Akaniambia acha kupoteza hela nunua sabufa ya 60k tu inatosha. Hakuna shida
Tv basi nikawaambia nataka nchi 32, akaniambia acha kupoteza hela, chukua ya nchi 15 au 21 tu inatosha.
Kuna baadhi ya marafiki ukiwa nao ndiyo kinakuwa chanzo chako cha umasikini. Nishakoma kushirikisha marafiki wenye mawazo ya kimasikini. Nilitegemea angeniambia, tatafuta hela uchukue muziki wa 800k. Ule maisha
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kutwa/wiki watoto wanacheza tu, eti kisa mwl kaenda kwenye mwenge, mara kuna shughuli za vyeti vya kuzaliwa, mara kuna chanjo, mtoto mpaka anamaliza miezi 6 daftari halijafika hata nusu.Jamaa eti hizo ndio shule.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Ndio ila sio kwa wote kama una uwezo ni bora waanze English medium ili wapate mwanzo mzuri wa lugha huko sekondari fresh tu hata st.kayumba wanapeta maana lugha ile ile.
Lugha watoto wanaweza kujifunza hata bila kwenda English medium.

Kwanini nyinyi wazazi kama mnafahamu kingereza kwanini msigeuza language of communication nyumbani kwenu for the benefits of your kids.?
 
Hivi inawezekana mtoto kumtoa shule za private na kwenda government?, ninavyojua ni mtoto kumtoa government kwenda private inawezekana.
Kwa shule ya msingi inawezekana ila kwa sekondari kidogo kuna changamoto sana na mlolongo huwa ni mrefu sana.
 
Ni wazo zuri kabisa
Nafikiri watoto wanajua lugha kwa urahisi zaidi kama ikiwa localized kama lugha ya mazungumzo ya kawaida ya kuwasiliana.

Kumpeleka mtoto English medium kwajili ya kujua english pekee sidhani kama iko sawa kwa sababu lugha yoyote mtu anaweza kujifunza hata nje ya shule.
 
Back
Top Bottom