Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

T
Yes angalau sio hizi za leo yani mtoto afundishwa English kwa kiswahili.

"Watoto leo tunajifunza kuhusu tense.
Zipo tense za aina tatu. Kuna past tense, present tense na future tense"
Ndo nikalipe milioni hivi kweli? Tuheshimiane tafadhal
Tafuta hela uache makasiriko.
Maskini mnafarijiana au sio. Waza madogo upate kidogo waza makubwa upate makubwa. Somesheni watoto shule bora ni haki yao ya msingi.

Sitaki povu
Yani mzazi ni mjinga anataka na vizazi vyake vibaki kwenye ujinga.
 
Tofauti kubwa kati ya Kayumba na Shule binafsi, wale wa Kayumba wanaenda shule kukua wakati wenzao wanaenda shule kusoma.
 
CHAI
 
upo sawa watoto wangu wa kwanza na wapili kayumba mpaka chuo kikuu. wa tatu mwezi huu form 5 kayumba huko huko.. wa nne yupo la 7 anamaliza muda mfupi ujao maendeleo yake sio mabaya na inshallah atafaulu. huko medium sitaki hata kusikia!
"Ukiona Elimu ni gharama basi jaribu ujinga"
 
Mkuu ungesema umewatoa boarding school na kuwaleta nyumbani hapo ningekupongeza sana kwakua mtoto kukaa Karibu na wazazi wake hata katika age ya 0-14 ni muhimu sana kwa ustawi wa akili ya mtoto,ukakamavu n.k
Lakini ww unajisifu kuwatoa kwenye mwanga na kuwaleta kwenye Giza kwa faida za kiuchumi tuu hapo umefeli
 
Na amefeli pakubwa sana
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kutwa/wiki watoto wanacheza tu, eti kisa mwl kaenda kwenye mwenge, mara kuna shughuli za vyeti vya kuzaliwa, mara kuna chanjo, mtoto mpaka anamaliza miezi 6 daftari halijafika hata nusu.Jamaa eti hizo ndio shule.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ndio ila sio kwa wote kama una uwezo ni bora waanze English medium ili wapate mwanzo mzuri wa lugha huko sekondari fresh tu hata st.kayumba wanapeta maana lugha ile ile.
Lugha watoto wanaweza kujifunza hata bila kwenda English medium.

Kwanini nyinyi wazazi kama mnafahamu kingereza kwanini msigeuza language of communication nyumbani kwenu for the benefits of your kids.?
 
Hivi inawezekana mtoto kumtoa shule za private na kwenda government?, ninavyojua ni mtoto kumtoa government kwenda private inawezekana.
Kwa shule ya msingi inawezekana ila kwa sekondari kidogo kuna changamoto sana na mlolongo huwa ni mrefu sana.
 
Ni wazo zuri kabisa
Nafikiri watoto wanajua lugha kwa urahisi zaidi kama ikiwa localized kama lugha ya mazungumzo ya kawaida ya kuwasiliana.

Kumpeleka mtoto English medium kwajili ya kujua english pekee sidhani kama iko sawa kwa sababu lugha yoyote mtu anaweza kujifunza hata nje ya shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…