Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Tatizo la kusoma st kayumba unakuwa huna strong connections unless ziwe zile special schools. Yaani utajikuta unamaliza lakini marafiki zako wengi watakuwa katika positions ambazo hazimsaidii mtu kati yenu kuondoka katika poverty circle

Yaani circle nzima ya marafiki si ajabu ukakuta huna contact ya kukuambia kuna nchi flani ulata ina fursa flani

hata English Medium hakuna connection. Connection unazo zizungumzia wewe zipo international kama IST. Hata hivyo kiuhalisia hazipo kwa sababu wanao soma huko wengi wametoka familia zinazo ishi kizungu ( kibepari) na ubinafsi.

St. Kayumba utapata network kubwa kwa sababu mnasoma watu wengi. Unlike English Medium darasa moja watu wanane hakuna connection yoyote ya maana.

Usisahau mkuu asilimia kubwa ya wazazi wanao somesha watoto wao hizo English Medium ni mahohehahe tu wenye hela za mawazo ambao hufuata mkumbo na kujionyesha kwamba na wao wanaweza kusomesha watoto English Medium lakini kiuhakika hawana lolote la maana kwenye maisha yao..

Wanaosomesha watoto English Medium ni masikini tu ambao wameamua kujipa matumizi ya sio ya lazima sawa na mfanyakazi mwenye mshahara wa laki nne ambae amenunua iPhone ya milioni mbili baada ya kujibana kwa miezi mitano.

English Medium ni Kayumba ambazo zinafundisha kwa KIINGEREZA.
 
Tatizo la kusoma st kayumba unakuwa huna strong connections unless ziwe zile special schools. Yaani utajikuta unamaliza lakini marafiki zako wengi watakuwa katika positions ambazo hazimsaidii mtu kati yenu kuondoka katika poverty circle

Yaani circle nzima ya marafiki si ajabu ukakuta huna contact ya kukuambia kuna nchi flani ulata ina fursa flani
Conection zako zote zipo zina fanya kazi kwenye viwanda na Makampuni yaliopo Pugu Road😂
 
Wow... very inspiring.

Niseme tu, primary nilisoma bweni, nikapangiwa shule ya serikali mbali. Nilipataga bendel memmorial na Mary Gorethy lkn sikwenda kwakua aunty yangu alisoma hiyo shule ya serikali miaka ya 90s. Ilikua bora sana kielimu miaka hiyo. Basi nikaenda. Sikua natumia sana nguvu kusoma. Wapo waliotoka shule za kayumba hata majina yao kuandika hawakua wakijua. Ilinishangaza sana. Lakini wapo wa kayumba waliokua wakikimbiza snaa. Wapo pia waliotoka shule za english mediums wengine moshi na arusha. Walifanya vizuri hawa wote. Mimi sikua natumia msuli wala
Kwa kweli nilikua natumia kingereza changi vizuri[emoji28][emoji23][emoji23]
Ila nilikua naumwa umwa maana sijazoea mazingira. Ila shule ni nzuri kwa kweli. Iko mazingira rafiki. Baada ya form 1 mzazi akataka nirudisha private. Kwakweli nilikataa. Niligoma. Unapata wapi maisha ya kisela kama haya[emoji23] yaan kusema kweli, kama hujasoma shule ya bweni ya serikali hujaenjoy. Kwanza nilikua kiongozi toka naanza mpaka namaliza form four. Na shule ina shamba kubwa tu. Sema sikuwahi lima. Kuna viwanja vya kufyekaaa. Yaan kila kazi inajitegemea. Kwakweli ulikua msingi mzuri sanaa. Na sijawahi jutia sema wengi niliosoma nao wa mikoa tofauti wana roho za uchoyo wala siyo bajeti mpaka ukubwani huku.
Nadhani ni nature ya mazingira yao. They dont wanna spend big to get bigger. Simaanishi starehe hapa hapana.

Ila this kayumba had the best experience.
Primary shule ya masista walikua wanatubebesha mawe mtoni na kulima juu. Sema ni kupanda karanga[emoji23] kufua pia tulikua tunawafulia hadi wadogo wa madarasa. Still was a good experience too. Imenifaa kimaisha kwakweli japo wazazi walipojua masista wanatupa hizo kazi ilikua hekaheka kubwa sana. Wazazi wetu wa dar kasoro wazazi wangu tuu nahisi walitaka watoa watoto wao kwa hasira ile shule kwa aina ya kazi tuluzopewa[emoji23]
Wazazi wangu hawana malezi ya kudekadeka. Na usiombe uwe na kesi.
Nimekuja enda baobab advance ni upumbavu tu. Huko ni daddy na mammy. Adhabu unapewa mopper na squeezer usukume maji kwenye verandah mtu analia mpk kamasi anataka mzazi amuhamishe shule anateseka. Mtu anakuja na pafyumu 5 tofauti za bei tofauti tena za bei ya ndege. Kwakweli mimi nilishindwa kama ilivyo ada kwa wagumu wenzangu. Watu mnakula soseji, makuku, samaki etc mchuzi mtaam kbs wanalalamikia principal wazazi wao wanalipa ada kubwa sana wanataka fanya mgomo wakati o level yangu huo ni msosi wa 5 star hotel[emoji23][emoji23][emoji23] aaah ujinga kbs.

Nakubaliana na ambao wanasema kama uwezo upo peleka mtoto English Medium hizi za kawaida ili mtoto awe na base ya Lugha vizuri halafu baada ya hapo tupa kayumba tu kwa kweli. Ila kayumba yenyewe inategemea pia. Kuna kayumba ni kilio. Hazifai. Ila niliona serikali ilifanya ukarabati baadhi ya shule za serikali zile kubwa. Hata yangu imependeza kweli. Rai yangu wakarabati zote aisee. Ni shule nzuri mno. Zaidi wajitahidi kwa waalimu waliopo katika hizi shule kubwa walau wawe degree holders.

Mimi nadhani Elimu bora iwe kwa vitendo zaidi. Na kama mzazi una biashara zako basi wanao wawe wanafika pia na wanapractice hasa wakati wa likizo. Haya mashule ya gharama yapogi tu. Ila kayumba experience was the best for me kwa kweli.
Numeipenda hii comment. miss pablo ila walimu wenye bora bachelor hapo no. ujue Walimu wa diploma before 2010 wako vzr kuliko bachelor 10 wa leo
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakao nipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa lako tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Acha blaa blaa wewe sema umefikisika.

Kuwatoa huko means unawaandaa kuwa wapiga kura tuu sio zaidi ya hapo maana hata Nje wataogopa kwenda Kwa sababu za lugha nk.
 
Ni kweli mkuu ila Nina watoto wanasoma shule moja jijini 2M per each, Kwa mwaka 4.M yaani mkuu inanisononeshansana kuona wanakaririshwa tu. Nimewaza sans baada ya kusoma Uzi huu.

Kibaya zaidi mkurugenz ameweka burser/mhasibu Hana huruma.

Naendelea kuwaza lkn elim ni Bora kuliko kiwanja. Lkn wapi Sasa tunakwenda.

Mimi n mtumish wa imma. Serikalini ndio kumejaa walimu very professional. Lkn serikali inawakosea san na wao hawafanyi vema. Ila wapo vzr wakiwezeshwa.

Kwa Sasa naona si English Media Wala feza school hakuna lolote.

Huyu accountant ameniingiza kwenye matatizo makubwa mno.
Nakumbuka ilikuwa Januari nikiwa nimeandaa ada kama kawaida kianzio. Si akaikataa bana! Watoto wawili Kila mmoja laki Nne jumla laki nane, alidai Kila mmoja lazima owe 600K. Niliingia mkopo ambao unaniandama hadi sasa....

Mmiliki wa shule nilimuamini nikadamp wanangu lkn alitubadilia, alikataa hata end of Januari nikamilishe aligoma. Iliniuma Sana. Kwa hiyo mleta Uzi huu hili suala ni seriasi sana.
Pole sana mkuu,nimepita huko kote,mateso yake sio ya nchi hii,yani hawanaga huruma hata kidogo,nashukuru huyu wangu aliyebakia sasa hivi yuko A level na anapiga Kayumba vizuri tu...
 
Faida ya mtoto kusoma shule bora ni kumjengea kujiamini

But the evidence says no. Uhalisia unaonyesha watoto walio soma kayumba ndio wanajiamini zaidi kwenye maisha kuliko hao wa st. English Medium.

Akina Diamond, Konde Boy, Shilole wote wamesoma kayumba ila wana confidence kuliko.

Halafu hivi sio nyie mnaosemaga watu ambao hawajasoma kabisa ndio wana uthubutu kuliko wasomi?
 
Tatizo la kusoma st kayumba unakuwa huna strong connections unless ziwe zile special schools. Yaani utajikuta unamaliza lakini marafiki zako wengi watakuwa katika positions ambazo hazimsaidii mtu kati yenu kuondoka katika poverty circle

Yaani circle nzima ya marafiki si ajabu ukakuta huna contact ya kukuambia kuna nchi flani ulata ina fursa flani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119] say no more. Yaaan hapa ndo tatizo linapoanzia. Yaan hiyo kayumba yangu pumbavu sana. Wengi bado wana mawazo ya kimaskini. Kwanza wanapenda mambo elf 5 kwa rambi rambi. Na wengine wasitoe.
Haya, jamani, hebu tuwe na kikundi rasmi, haya mambo ya kutandika mikeka yamepitwa na wakati, wao hawako tayari. Na wanataka per month iwe elf 5. How are u gonna grow? Si kwamba labda wengine hawawezi hapana. Ila hawana mawazo mapana majority. Watu wa asili ya huo mkoa ni changamoto sana watani zangu. Wapo wachache sana wameamka. Inabidi mtumie ubabe kwenda sawa. Connections ndo kabisaaa hakunaa aisee. Hakunaa. Labda hizo special.schools. kwangu mimi walikuwepo japo wachache sana na si wa mkoa huo pia. Wengi watoto wa wakulima na wafugaji huko. Wanapiga jembe kama hawana akili nzuri. Lakini connection ya mazao unaipata mkuu[emoji23][emoji23] walikua wanaluja na pocket money mzigo umeshibaa
 
hata English Medium hakuna connection. Connection unazo zizungumzia wewe zipo international kama IST. Hata hivyo kiuhalisia hayupo kwa sababu wanao soma huko wengi wametoka familia zinazo ishi kizungu ( kibepari) na ubinafsi.

St. Kayumba utapata network kubwa kwa sababu mnasoma watu wengi. Unlike English Medium darasa moja watu wanane hakuna connection yoyote ya maana.

Usisahau mkuu asilimia kubwa ya wazazi wanao somesha watoto was hizo English Medium ni mahohehahe tu wenye hela za mawazo ambao hufuata mkumbo na kujionyesha kwamba na wao wanaweza kusomesha watoto English Medium lakini kiuhakika hawana lolote la maana kwenye maisha yao..

Wanaosomesha watoto English Medium ni masikini tu ambao wameamua kujipa matumizi ya sio ya lazima sawa na mfanyakazi mwenye mshahara wa laki nne ambae amenunua iPhone ya milioni mbili baada ya kujibana kwa miezi mitano.

English Medium ni Kayumba ambazo zinafundisha kwa KIINGEREZA.
[emoji23][emoji23][emoji23]
Dah. Ila wazazi wengi ni wafanya biashara
Sema kuna wale wadada wadangaji pia nao huwa hawataki kubaki nyuma kwenye hilo. Kama nakuelewa hivi. Unakuja kuja[emoji23][emoji23]
 
Numeipenda hii comment. miss pablo ila walimu wenye bora bachelor hapo no. ujue Walimu wa diploma before 2010 wako vzr kuliko bachelor 10 wa leo
Yawezekana kbs. Diploma wengi walisoma kwa vitendo. Na Elimu ilikua haijawa biashara sana kwa wakati huo. Siku hizi ni kichefuchefu. Na ndo maana serikali inawapenda sana diploma[emoji23][emoji23]
 
Wow... very inspiring.

Niseme tu, primary nilisoma bweni, nikapangiwa shule ya serikali mbali. Nilipataga bendel memmorial na Mary Gorethy lkn sikwenda kwakua aunty yangu alisoma hiyo shule ya serikali miaka ya 90s. Ilikua bora sana kielimu miaka hiyo. Basi nikaenda. Sikua natumia sana nguvu kusoma. Wapo waliotoka shule za kayumba hata majina yao kuandika hawakua wakijua. Ilinishangaza sana. Lakini wapo wa kayumba waliokua wakikimbiza snaa. Wapo pia waliotoka shule za english mediums wengine moshi na arusha. Walifanya vizuri hawa wote. Mimi sikua natumia msuli wala
Kwa kweli nilikua natumia kingereza changi vizuri[emoji28][emoji23][emoji23]
Ila nilikua naumwa umwa maana sijazoea mazingira. Ila shule ni nzuri kwa kweli. Iko mazingira rafiki. Baada ya form 1 mzazi akataka nirudisha private. Kwakweli nilikataa. Niligoma. Unapata wapi maisha ya kisela kama haya[emoji23] yaan kusema kweli, kama hujasoma shule ya bweni ya serikali hujaenjoy. Kwanza nilikua kiongozi toka naanza mpaka namaliza form four. Na shule ina shamba kubwa tu. Sema sikuwahi lima. Kuna viwanja vya kufyekaaa. Yaan kila kazi inajitegemea. Kwakweli ulikua msingi mzuri sanaa. Na sijawahi jutia sema wengi niliosoma nao wa mikoa tofauti wana roho za uchoyo wala siyo bajeti mpaka ukubwani huku.
Nadhani ni nature ya mazingira yao. They dont wanna spend big to get bigger. Simaanishi starehe hapa hapana.

Ila this kayumba had the best experience.
Primary shule ya masista walikua wanatubebesha mawe mtoni na kulima juu. Sema ni kupanda karanga[emoji23] kufua pia tulikua tunawafulia hadi wadogo wa madarasa. Still was a good experience too. Imenifaa kimaisha kwakweli japo wazazi walipojua masista wanatupa hizo kazi ilikua hekaheka kubwa sana. Wazazi wetu wa dar kasoro wazazi wangu tuu nahisi walitaka watoa watoto wao kwa hasira ile shule kwa aina ya kazi tuluzopewa[emoji23]
Wazazi wangu hawana malezi ya kudekadeka. Na usiombe uwe na kesi.
Nimekuja enda baobab advance ni upumbavu tu. Huko ni daddy na mammy. Adhabu unapewa mopper na squeezer usukume maji kwenye verandah mtu analia mpk kamasi anataka mzazi amuhamishe shule anateseka. Mtu anakuja na pafyumu 5 tofauti za bei tofauti tena za bei ya ndege. Kwakweli mimi nilishindwa kama ilivyo ada kwa wagumu wenzangu. Watu mnakula soseji, makuku, samaki etc mchuzi mtaam kbs wanalalamikia principal wazazi wao wanalipa ada kubwa sana wanataka fanya mgomo wakati o level yangu huo ni msosi wa 5 star hotel[emoji23][emoji23][emoji23] aaah ujinga kbs.

Nakubaliana na ambao wanasema kama uwezo upo peleka mtoto English Medium hizi za kawaida ili mtoto awe na base ya Lugha vizuri halafu baada ya hapo tupa kayumba tu kwa kweli. Ila kayumba yenyewe inategemea pia. Kuna kayumba ni kilio. Hazifai. Ila niliona serikali ilifanya ukarabati baadhi ya shule za serikali zile kubwa. Hata yangu imependeza kweli. Rai yangu wakarabati zote aisee. Ni shule nzuri mno. Zaidi wajitahidi kwa waalimu waliopo katika hizi shule kubwa walau wawe degree holders.

Mimi nadhani Elimu bora iwe kwa vitendo zaidi. Na kama mzazi una biashara zako basi wanao wawe wanafika pia na wanapractice hasa wakati wa likizo. Haya mashule ya gharama yapogi tu. Ila kayumba experience was the best for me kwa kweli.
Safi sana dada ake. Very inspiring. Suala la malezi ya kitanzania kwenye English Medium wamefeli sana. Yani wanataka kuwalea watoto kama wazungu eti.

Wakati mtoto wangu wa kike yupo darasa la saba kwenye shule ya KIINGEREZA kuna siku nilienda shulenj kwao . Sehemu ya wageni kusubiria ilikuwa karibu na darasa la saba. Nikasikia mwalimu anamuomba msamaha dogo wa kiume anampa na chocolate . Jioni namuuliza dogo ananiambia eti jana yake mwalimu alimfokea dogo, dogo akakskrika ndio maana siku hiyo ticha akawa anamuomba msamaha. Say what?
Kama asingekuwa la saba ningemrudisha kayumba siku hiyo hiyo
 
Back
Top Bottom