Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

[emoji23][emoji23][emoji23]
Dah. Ila wazazi wengi ni wafanya biashara
Sema kuna wale wadada wadangaji pia nao huwa hawataki kubaki nyuma kwenye hilo. Kama nakuelewa hivi. Unakuja kuja[emoji23][emoji23]
🤣🤣🤣 usinielewe kwanini sasa
 
2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mkuu hapa ndo pa kukazania zaidi,kama hauna muda unaweza tafuta hata mwl wa kiingereza wa 100,000 kwa mwezi kila siku akawa anawapigisha kitabu wanapokuwa nyumbani
 
Wewe kama wewe lazima upate Faida Kwa sababu umepunguza matumizi

Ila Kwa watoto wako ni maumivu na hayo maumivu watakutanayo pale watakapoingia katika soko la ajira na kuitwa katika interview tena kama sector binafsi ndio kabisa lazima wawapishe walioyosoma private school

Mimi nimesoma kayumba kuanzia primary Hadi form six nilipoingia chuo ndio nikaanza kuona tofauti kati ya tuliyotoka kayumba na wale private school

Pia nilipoingia katika ajira sector binafsi ndio kabisa Kuna tofauti kubwa sana

Broo believe me usiwaone hao akina Joket au akina Babra ukazania walifika walipofika Kwa bahati mbaya sio kweli ila ukweli ni kwamba wazazi wao wali invest

Mimi binafsi nimeapa watoto wangu hawatasoma kayumba labda niwe Sina pesa

hizo English Medium walimu wake :
1. Wamesoma kayumba.

2. English sio lugha yao ya kwanza

3. English sio lugha yao ya mawasiliano ya kila siku ( kwa maana ni watanzania ambao huwasiliana kwa kiswahili)


Unaweza vipi kulipa mamilioni ili mtoto wako afundishwe kwa KIINGEREZA na mtu ambae KIINGEREZA sio lugha yake ya kwanza? Wala sio lugha yake ya mawasiliano?
 
2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mkuu hapa ndo pa kukazania zaidi,kama hauna muda unaweza tafuta hata mwl wa kiingereza wa 100,000 kwa mwezi kila siku akawa anawapigisha kitabu wanapokuwa nyumbani
Nakazia . Na walimu wapo wengi sana...
 
Safi sana dada ake. Very inspiring. Suala la malezi ya kitanzania kwenye English Medium wamefeli sana. Yani wanataka kuwalea watoto kama wazungu eti.

Wakati mtoto wangu wa kike yupo darasa la saba kwenye shule ya KIINGEREZA kuna siku nilienda shulenj kwao . Sehemu ya wageni kusubiria ilikuwa karibu na darasa la saba. Nikasikia mwalimu anamuomba msamaha dogo wa kiume anampa na chocolate . Jioni namuuliza dogo ananiambia eti jana yake mwalimu alimfokea dogo, dogo akakskrika ndio maana siku hiyo ticha akawa anamuomba msamaha. Say what?
Kama asingekuwa la saba ningemuhamisha shule siku hiyo hiyo ningemrudisha kayumba
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] huyo mwalimu siyo mseng* kweli? Asije kuwa analawiti watoto. Kwann anampa chocolate. Katika vitu sipendi ni hizi vitu za kula kula za kutoka viwandani. Aisee. Naimba umakini uzidishwe hapo. Nimepata hofu na hiyo mwalimu. Hakuna wa kumuamini hata kidogo.

Namshukuru Mungu hakika kwa experience nilizopitia. Hizo shule 2 kamwe sitokaa nijutie. Hiyo ya primary kuna shamba liko Mandaka huko. Basi tulikua tunachaguliwa wale wa grades 5 mpk 7 tunaambiwa tuvae tracksuit zetu, tunakwea fuso na wafanyakazi mpk shamba kuvuna mahindi na kurudi. Tunawashwaaa[emoji23][emoji23] sema sisi tulikua tunaenjoy. Hatukuwahi kuona shida.
It was superb kwa kweli.

Kama ni viatu vya watoto basi kuna kazi ya kuvibrash kama matron hayupo. Wale wa baby class na kinder kwa ujumla. Pia uniform zilikua tunanyoosha na maton. Zoote yaani. Usafi wa kudeki ni wafanyakazi ila kufagia daily ni wenyewe. Sema kipengele cha kuogesha watoto wa watu ndo sikukipenda na hata wazazi waligoma. Kuna vitoto vidogo vya mpk 2yrs jamani. Vingine havijatimiza. Kuna wamama wana moyo wa jiwe aisee.
Unakuta mzazi anaona sifa mwanae kula maprestige na masoseji na machips akidhani its health kisa yeye hakuzila udogoni kwa dhiki na umaskini basi anaona wanae wale unakuta mtoto wa kiume amenenepa mpaka makalio. Inashangaza sana. Hapo ni primary. Na wanabembelezewa na simu maaaninaa sana. Mtoto asipewe simu. Wazazi wanaharibu sana watoto. Mimi sitaki mazoea ya vitu kama hivyo na watoto. Tuanze nao hukuhuku chini. Kuanzia lishe, masomo, nidhamu, etc. English medium zilizo moderate ni kama akina diamond, olimpio etc. Ziko shule nzuri tu.
 
2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mkuu hapa ndo pa kukazania zaidi,kama hauna muda unaweza tafuta hata mwl wa kiingereza wa 100,000 kwa mwezi kila siku akawa anawapigisha kitabu wanapokuwa nyumbani
Word
 
Nilisimamisha ujenzi kwa takribani miaka 6,tokea nimechukua maamuzi magumu ya kumpeleka mtoto wangu kayumba ujenzi unaenda kwa kasi ya ajabu,hili kwa wale wazee wa kukwapua nadhani hawatanielewa,ila kwa sisi tunaotegemea mshahara wa mwezi watajua naongea nini.Kizuri zaidi mwanangu ni kicwa na huku aliko bado anawapelekesha,kwa hiyo na mshukuru Mungu kwa kunipa maamuzi sahihi...
Hongera sana mkuu
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakao nipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.


MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa lako tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Pale masikini wanapojifariji kwa umasikini wao,we have no choice but to let you dogs sleep!

Masikini hakosi sababu cha chochote kile alichoshindwa kuki-afford!

Hakosi sababu!
 
Hata kama una pesa lazima ujifunze kubana matumizi.
Sio busara kulipa milioni4 ili mtoto afundishwe A for Apple. Mwisho wa siku maisha ndo haya haya
Pale mzazi unapojitia unajua fani ya ualimu zaidi ya walimu wenyewe ndio haya unayoongea yanatokea

Masikini hutakosa sababu yeyote ile kutetea financial choices zako

Eti A for Apple,na ni kweli wanafundishwa hicho tu?

Yaani masikini wanajua ku sensationalize kitu ku justfy their choices!
 
Pale mzazi unapojitia unajua fani ya ualimu zaidi ya walimu wenyewe ndio haya unayoongea yanatokea

Masikini hutakosa sababu yeyote ile kutetea financial choices zako

Eti A for Apple,na ni kweli wanafundishwa hicho tu?

Yaani masikini wanajua ku sensationalize kitu ku justfy their choices!
Tuambie wanafundishwa nini mkuu?
 
Tuambie wanafundishwa nini mkuu?
Wewe uliona ni A for Apple tu?

Fact is,wanafundishwa vitu chungu nzima according to IB framework,wewe na matongotongo yako umeona A for Apple and ran away with it just to justify umasikini wako wa kutoweza hizo ada!

Wewe umeshindwa hizo ada,just admit,pangusa matako saka hela urudi hewani uwape watoto haki yao,hizi shenanigans hazisadii
 
Wewe uliona ni A for Apple tu?

Fact is,wanafundishwa vitu chungu nzima according to IB framework,wewe na matongotongo yako umeona A for Apple and ran away with it just to justify umasikini wako wa kutoweza hizo ada!

Wewe umeshindwa hizo ada,just admit,pangusa matako saka hela urudi hewani uwape watoto haki yao,hizi shenanigans hazisadii
Kwa mfano vitu gani hivyo wanavyo fundishwa. Ambayo vina justify mamilioni ya shilingi kama malipo ya ada.
 
Back
Top Bottom