Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Hivi hili jina la saint kayumba lilianzia wapi
Umezaliwa mwaka gani? Kipindi cha uongozi wa Kikwete shirika la "hakielimu'(sijui ni la serikali au binafsi) walikuwa wanapublish matangazo kwenye redio na TV.
Matangazo hayo yalikuws na dhumuni moja tu la kukosoa mfumo na mazingira ya shule za serikali. Wahusika wakuu walikuwa vijana wawili wa kike( jina nimelisahau) huyu alikuwa anasoma shule ya private na wa kiume alikuwa anaitwa Kayumba alikuwa anasoma shule ya serikali.
 
Shule nzuri ni shule ambayo ina utilize uwezo wa mtoto.

St Kayumba sio good option kwa mtoto unless kipato sio kizuri. Nimesoma st kayumba from p' to o'level kwahiyo najua kitu nachokizungumza hapa so you better pay attention!

Watoto wanao excel shule za kayumba academically mostly wana biological advantage (wamezaliwa na uwezo mkubwa wa akili wa kuhifadhi kumbukumbu vizuri). Na wachache sana wanafaulu kwa jitihada binafsi za wazazi kama kuwapeleka tuition na ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya mtoto shuleni (kuangalia kama anafanya homework vizuri n.k). Ila watoto wengi wa Kayumba wapo kwenye hatari kubwa sana ya kuharibikiwa. Nina mifano hai ya kutosha, so you better listen careful.

Anyday of the week, nitapigia kura International/English Medium over Kayumba kwa sababu ya utofauti mkubwa wa mifumo yao ya uendeshaji. Yes you heard me well, SYSTEM!

Mdogo wangu alibahatika kusomeshwa English medium, wakati yupo std 6 nilikua napiga naye story za hapa na pale nikagundua anajua vitu vingi ambavyo laiti angesimamishwa na hawa form four wengi wa kata kwenye debate, kwa kweli ingekua ni aibu.

Sasa shida iko wapi?

Kayumba hakuna ufuatiliaji wa karibu kwa watoto. At least hata English Medium za mchongo wanamrudisha mtoto mpaka nyumbani na wanampitia tena Ahsubuhi. Kila siku mtoto lazima aachiwe homework za kutosha kumpunguzia muda wa kucheza mtaani hovyo (Aliyocheza shuleni inatosha!).

Ila Kayumba mzazi huna uhakika kama mtoto kafika shule, huna uhakika kama mtoto atarudi nyumbani salama, huna uhakika kama muda aliofika nyumbani ndio wenyewe au kuna mahali kapitia, huna uhakika kama hajaachiwa homework au kaachiwa, hujui marafiki zake ni kina nani, hujui kama anahudhuria vipindi vyote au lah... na ikitokea siku umeitwa Shule ujue kabisa kuna kosa kubwa sana kafanya maana haya mengine ya ufaulu walimu sio shida zao, utajua mwenyewe na mtoto wako!
Una program subconscious mind yake kuwa wa kusukumwa ,ama kuelekezwa kila kitu,yaani unamtengenezea behavior ya kusimamiwa ama kulishwa like spoon feeding.
Sasa njoo Hali halisi ya maisha ,he maisha yako Kama huko saint English ama Kama saint kayumba. Kuwa atasimamiwa na kuelekezwa how to fight in the jungle full if wolves, wild dogs, bulls and Black mamba. Binafsi napenda mwanangu afundishwe shule ya kijeshi,yaani Ni mchakamchaka baadaye akuja kuwa automatic kufanya Mambo ya kijeshi bila ya kusukumwa. Alime bustani,apapalie,atengeneze fanicha,ajenge nyumba,atengeneze gari,ajue kutengeneza sabuni etc,Kama anapena mchezo fulani akomae nayo,atoke huko anajua kuchora ramani za nyumba,anajua kutumia vifaa vya saveya,awe anajua vitu vingi ama awe na skills za maisha na sio eti kufaulu na kuongea English Basi kuwa ndio amefaulu maisha.

Yaani when mental and physical are trained or exposed under stress and pressure then they grow stronger than how they were before.
Ikiwekazana atembee kwenda shule, what I trust Ni kuwa binadamu huwa haihangaiki Kama hapati any hardship.
Am a student of mind and brain. Yaani we're always driven by either pleasure or pains.
Yaani mtu anafanya kitu kukwepa maumivu ama kupata Raha Basi. Na ubongo kazi yake Ni kukwepesha kutoka kwenye habari ama kitu ambacho kinakupa maumivu ya kimwili na mentally
 
Ni kawaida ya brain kutafuta faults, errors,mistakes, blunders etc. Sikuoni Kama una kosa Bali Ni nature ilichokuzawadia sema inatakiwa upambane ufanye recoding Kama sio reprogramming ili uweze kuushinda ubongo wako dhiidi ya reptile brain,tumia cortex achana na limbic and amygdaly brains zitakupoteza
Hakuna namna unayoweza kujitetea wakati ushahidi uko wazi. Saa nyingine kuwa muungwana kwa kurekebisha ulipoteleza. Unaweza ukawa umepata B au A ila kwenye kuongea ukawa hovyo tu. Unajitutumua wakati ni wewe uliyeandika sentensi yenye makosa.
 
Hongera sana.

Mtoto akilelewa vizuri na akapata mahitaji ya lazima kwa binadamu basic needs kwa wakati na mental health nzuri, usimamizi wa kimasomo mzuri, Hata akisoma kayumba lazima afanye vizuri

Chuo kikuu cha dsm, ama Udsm best students wao kwenye graduations kila mwaka mara nyingi ni waliosoma kayumba primary.
Best students wengi ni mabingwa wa kukariri wala hawana maajabu
 
Huo ndo ukweli kwamba mtu kafika kiwango ambacho vipaumbele vinashindana (apeleke mtoto shule nzuri ya ada kubwa au apeleke ya kawaida na pesa inayobaki afanyie mengine) maana kipato cha familia kidogo. Kingine kilicho wazi ni maandaliz kwa mzazi ambaye alijiandaa toka hajapata watoto na akatafuta kipato kizuri toka mapema ina maana uchumi wake unaweza kuhimili kupeleka watoto hizo shule, kufanya uwekezaji, n.k kifupi kujikuna kunaendana na urefu wa mkono. Haya mengine ni ya kujipa moyo tu!
Huo ndo ukweli watu wengi wanaanza familia pasipo kuwa na mpango mkakati wa kiuchumi wa miaka isiyopungua 30

Shule ya za serekali kidogo zaman sasa hivi zinahali mbaya sana
 
Kwa dunia ya leo hakuna sehemu salama kwa watoto ila kusema kweli Kayumba ni hatari zaidi jamani.
Kwanza shule nyingi za Kayumba zina watoto wengi kiasi kwamba kuna watoto wanatoa makwao ila wanaishia vyooni na njiani darasani hawafiki na mwalimu hajui.Mtoto anaweza kaa mwaka hajaingia class.
Kayumba watoto wanafanyana vitu vibaya chooni na njiani.

Kayumba mwanao anacheza na watoto wanaotembea umbali mrefu kwenda na kurudi shule na huko njiani wanajifunza mambo mengi mabaya.

Kayumba tupeleke watoto ikiwa hakuna namna ila kama ka uwezo kapo tafuta shule nzuri ya kulipia fanyia research tabia za watoto wa hapo ukiridhika mtoto asome hapo.
Kuna shule mbagala ina wanafunzi elfu 7000 hapo kuna elimu sasa
 
Hakuna namna unayoweza kujitetea wakati ushahidi uko wazi. Saa nyingine kuwa muungwana kwa kurekebisha ulipoteleza. Unaweza ukawa umepata B au A ila kwenye kuongea ukawa hovyo tu. Unajitutumua wakati ni wewe uliyeandika sentensi yenye makosa.
Kuongea naongea vizuri mno yaani nikiwa chuoni nilikuwa naongea English muda wote ,hata kutongoza kwangu urahisi Ni English mpaka watu Wana doubt kuwa ivi kweli mie Ni mtanzania na wananiuliza the way navyo flow mkuu.
Na uelewe nimeingia la kwanza sijui kiswahili,kidato Cha Pili naongea English,nikiwa chuoni nikasoma kwa kirusi natongoza demu wa kirashia anavua chupi kwa Russian na lugha ambayo nimejifunza Niko above 23.
Ishu kuwa kwenye maisha nayoiheshimu na ambayo inatakiwa uombe mwanao awe nayo Ni Ile desire , willingness, commitment, discipline,courage, warrior mindset,greed and determination of Successful, kuwa mtu fulani. Hii huwa haina kuwa upo wapi,unaongea lugha gani,ama wewe kabila ,dini,rangi gani

Kwa maneno ya Greek or Roman empiror philosophy ngoja nikupe alisemaje.
Screenshot_20230603-104544.png
Screenshot_20230515-153625.png
 
Wengine pesa wanazo kuna sehemu nilikaa nikashangaa mzazi ana hela anasomesha mtoto kayumba kisa anasema anataka mwisho wa siku mtoto akimaliza form six aje apate mkopo bodi ya elimu ya juu bila shida

Mtoto akamsomesha shule ya msingi ya kayumba Darasa zima wakafaulu kwenda shule ya kata ya Kayumba Form one

Form four shule haikuwa na division one wala two wote waliishia division three ,four na zero na hakuna ambaye combination ya kwenda Form five ilikubali

Ndoto za mwanae za ohh akasome high.school ya serikali form five iliishia mwisho cha ohh apate mkopo bodi ya mikopo zikayeyuka hewani.Sababu hata hiyo form five hakuiona

Mzazi kama kipo usiwe na vi theory vya kiajabu ajabu utaumiza mtoto.Somesha shule nzuri
Mzazi mwenye hela huitaji kuangaika na maswala ya bodi ya mikopo unaweza ukawa una hela ila ukawa na mentality za kimaskini
 
Hakuna namna unayoweza kujitetea wakati ushahidi uko wazi. Saa nyingine kuwa muungwana kwa kurekebisha ulipoteleza. Unaweza ukawa umepata B au A ila kwenye kuongea ukawa hovyo tu. Unajitutumua wakati ni wewe uliyeandika sentensi yenye makosa.
Yaani nimeingia la kwanza naongea my mother tongue pekee Sasa shangaa tunaingia la Pili nakuwa wa kwanza na shule nimetoka bush nikaenda kusomea town ,yaani lugha is of immaterial linapokuja suala la kichwa kuelewa kitu. Unaweza ukafundishwa kwa kabila yako ukawa daktari mzuri mno. Yaani wachina wanasoma kwa lugha yao Ni Engineers na leo nilikuwa nao wanaseti foundation ya road underpass,yaani technical drawings anaisoma na anaweka vipimo. Yaani hufanyi kazi kwa kuongea Bali kwa vitendo na uelewa wako
 
Dunia nzima matajiri wenye lengo la uendelezaji wa mali lazima wasomeshe kwenye shule kubwa na za ghali ili kujenga connection.

Matajiri wote Tz watoto wao wapo IST, hapo hutamkosa mtoto wa MO, GSM, Azam, Cello, Camel
umeongea bonge la point ambayo ni wachache sana wanaweza iona
Connection na exposure ni muhimu zaid hata ya cheti kizuri
 
Kuongea naongea vizuri mno yaani nikiwa chuoni nilikuwa naongea English muda wote ,hata kutongoza kwangu urahisi Ni English mpaka watu Wana doubt kuwa ivi kweli mie Ni mtanzania na wananiuliza the way navyo flow mkuu.
Na uelewe nimeingia la kwanza sijui kiswahili,kidato Cha Pili naongea English,nikiwa chuoni nikasoma kwa kirusi natongoza demu wa kirashia anavua chupi kwa Russian na lugha ambayo nimejifunza Niko above 23.
Ishu kuwa kwenye maisha nayoiheshimu na ambayo inatakiwa uombe mwanao awe nayo Ni Ile desire , willingness, commitment, discipline,courage, warrior mindset,greed and determination of Successful, kuwa mtu fulani. Hii huwa haina kuwa upo wapi,unaongea lugha gani,ama wewe kabila ,dini,rangi gani

Kwa maneno ya Greek or Roman empiror philosophy ngoja nikupe alisemaje.
View attachment 2711383View attachment 2711389
Mkuu ur the true son of ur father. Asante kwa madini. Nimejifunza kitu kikubwa sana kaka
 
Ruka ruka lakini hii elimu yetu ya awali Hadi form 4 inatosha mtoto kuingia katika fani aitakayo awe kayumba au ushuani! Hizi form 5 & 6 ni kupoteza muda. Muhimu ni determination ya mtoto mwenyewe bila kujali ukayumba au ushua
 
Ruka ruka lakini hii elimu yetu ya awali Hadi form 4 inatosha mtoto kuingia katika fani aitakayo awe kayumba au ushuani! Hizi form 5 & 6 ni kupoteza muda. Muhimu ni determination ya mtoto mwenyewe bila kujali ukayumba au ushua
mkuu big up umeongea point kubwa sana
 
Hakuna cha mambo ya dad mommy halafu Toto la kiume
Daddy & Mummy maana yake ni baba na mama. Sasa shida ipo wapi? Hivi unajua ya kuwa asilimia kubwa ya tabia za hovyo mtoto anajifunza katika hizi shule za Swahili medium? Mimi ninashauri kila mmoja afanye jambo kulingana na hali yake ya uchumi.
 
Back
Top Bottom