Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Ukishasema kutumia kizembe hasa inapokuja swala la Elimu ni kwamba hauna hela.
Tafuta hela itosheleze mahitaji siyo ujibane bane ili mahitaji yafit kwenye hela [emoji23][emoji23]

Elimu ni nini?.Tuanzie hapo kwanza. Kwa sababu ninacho jua Tanzania hakuna 'elimu' iwe English Medium iwe Swahili medium.
 
Msisahau pia kila mtu ana destiny yake kwenye maisha bila kujali alisoma wapi. Mfano Paula Kajala alisoma English Medium kuanzia darasa la kwanza hadi la 7 then akaenda Tusiime form one hadi Six. Now look at what she is doing. Hicho anacho kifanya ndicho ambacho kilimpeleka shule?
Humpangii mtu maisha, mpe haki yake ikiwemo elimu bora, mengineyo ni maamuzi yake.
 
Kufikiri kwamba ukisoma shule ya kishua utapata connection na watoto wa kishua ni sawa na kuamini kwamba ukienda kwenye bar ya kishua wanakouza bia elfu kumi basi wale washua wanao kunywa kwenye hiyo bar watakuwa rafiki zako kwa sababu unakunywa nao bar moja wakati wenzako wanakuona mwizi tu.

Wakishua wanawadharau sana watoto wa kimasikini. Na hawapendi kuchangamana nao.

Mfano mzuri ni pale Shaaban Roberts, ngozi nyeusi wana baguliwa sana. Sio wanafunzi tu bali hata walimu. The same as Agha Khan.

Hata USA ndivyo inavyo kuwaga mara nyingi. Mtoto mweusi akipelekwa kwenye shule ya wazungu tu atabaguliwa mpaka maka.

Kuna mitaa mingine Marekani akihamia mtu mweusi hata mmoja wazungu wanauza nyumba zao wanahamia mitaa mingine.

Njoo kwenye mpira, Konde Boy kaenda Ahly hapo kaishia kubaguliwa kwa sababu anatoka nchi ya kimasikini.


Ukiwa mtoto a shule ya kishua, kampani yako watakuwa
naona unachanganya race na economic status.
 
naona unachanganya race na economic status.

Katika maeneo mengi huwezi kuvitofautisha. Mifano mizuri ni hapa hapa bongo. Mitaa wanayo ishi wenye kipato kikubwa inaitwa uzunguni, uhindini. Mitaa wanayo ishi masikini huitwa" uswahilini "
 
Katika maeneo mengi huwezi kuvitofautisha. Mifano mizuri ni hapa hapa bongo. Mitaa wanayo ishi wenye kipato kikubwa inaitwa uzunguni, uhindini. Mitaa wanayo ishi masikini huitwa" uswahilini "

comment yako inataka kusema kwamba majority ya watoto weusi waliopo shule za gharama ni maskini. Unadhani ni sahihi?
 
Wewe unaonaje?

comment yako ilikuwa inaongelea kuhusu ubaguzi wa tajiri kwa maskini lakini mifano yako inaongelea ubaguzi wa race.

That is to say weusi wote walioshule za gharama ni maskini which is absolutely not true.
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa JF wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakaonipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (Huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.


MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa laki tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Endelea kujifariji
Hata Madudu ya DP world yanawahusu product ya kayumba
 
Hata yule bodaboda alielawitiwa na Mzungu alisoma English Medium.

Malezi ya mtoto sio kumfundisha kuongea kiingereza tu mkuu anatakiwa pia aandaliwe na kufundishwa namna ya kuishi kwa kuyatawala mazingira yake
Hapo kwenye malezi nakuunga mkono hizo English Medium wanalelewa kimama mno, mbu akiingia darasani mtoto yote inaanza kulia. Na hap no darasa la saba ujue
 
Back
Top Bottom