Jamaa kuna kitu anataka kukitengeneza hasa ni kitu positive hasa ila tatizo tumechanganyikiwa na usimba na uyanga ni ngumu sana kumuelewa. Ila hii ndio ilikuwa ni fursa kwa wapenzi wa soka la haki kuungana na huyu mwamba aliyeamua kujitolea muda wake. Maamuzi mabaya hayakuanzia jana tu bali tokea muda mrefu tu, na haikufaidisha Simba pekee hata timu zingine zimenufaika ikiwepo Yanga. Ni swala la kushirikiana nae kwa kumpa vielezo kwa kuanzia tukio la jana kisha kurudi nyuma na kuonesha matukio mengine kwa timu zinginezo pia. Hilo litasaidia kuonesha kuwa hayo matukio hayakuanzia jana na wala hakuanzia kwa timu moja
Ila kuna ugumu nauona mahali, hizi tuhuma zinatakiwa kutolewa na ushahidi wa nje wa uwanja. Mfano mawasiliano ya baina hao wapangaji matokeo, video zao za hao wapangaji wakiwa wanajadiliana kuhusu kupanga, na vielezo vingine. Ishu tuliona jana ni ya ndani ya uwanja ni ngumu sana wao kuhitimisha kuwa ni match fixing kwasababu hayo yanaonekana kama makosa ya mwamuzi jambo ambalo sio jipya kwenye mpira wa miguu hata huko ulaya tunayashuhudia.