Kerosine Bal
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 247
- 231
Hii kitu ipo na watu wanapiga hela... Mdogo angu awali aliniambia nikamkatalia nkamwambia forex ni utapeli tuu. Alisisitiza anaomba laki 5 kama sehemu ya msaada wangu kwake, nilimkatalia kwa macho makavu nilitamani hata kumfukuza kwangu. Baada ya kama mwezi hivi alinambia amepata wazo la biashara na jamaa yake ila mtaji mdogo. Nkamsaidia laki 700 dogo akaniaga anakwenda kufuata mzigo kama wiki 2 hakuonekana. Sikuwahi kumfuatilia sana kwe hiyo biashara yake. Baada ya kama miezi 3 hivi(mwezi oktoba sasa) dogo alikuja na kabegi kadogo ilikuwa usiku tunakula akachomoa 1.5 M akanipa zen akanambia asante kaka kwa kunilea leo naondoka kwako sasa naweza kujitegea. Nkamwuliza hela umepata wapi zote hizi akanjibu FOREX nilikuwa naogopa kukwambia kama nafanya forex. Forex is real.