Mrejesho: Kilichonipata Malta ni zaidi ya Ukraine, siku 18 za kufa na kupona

Ulitoa mzigo
 
Ungesubiri upone kabisa ndo uje na mrejesho full
 
Pole sana. Ila huko nje yanawapataga makubwa sana. Nina ndugu yangu alikutana na maswahiba Japan baada ya kujihusisha na biashara ya magari na wajapan toka kule kuleta nchini.

Walianza na magari machache, yakaisha trip ya pili yakaongezeka zaidi biashara ikaenda vizuri , trip ya tatu mzigo ukaja kupotea mazima bandarini. Wajapan hawakumwelewa kabisa wakahisi kawapiga tukio ila wakasema wanafatilia wenyewe wajue mzigo ulipoenda. Wakati wanachunguza wakamwalika aende Japan kupoteza mawazo.

Sasa sijui yaliyompata amerudi kavurugwa anaeleza vitu havieleweki mara walitaka kumkata mikono, mara kaingizwa chumba miili ya watu imening'inizwa. Kwa sasa yupo milembe kichwa imeruka kabisa na hatujui vizuri yaliyomsibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…