Pole sana. Ila huko nje yanawataga makubwa sanai. Nina ndugu yangu alikutana na maswaiba Japan baada ya kujihisisha na biashara ya magari na wajapan toka kule kuleta nchini. Walianza na magari machache, yakaisha trip ya pili yakaongezeka zaidi biashara ikaenda vizuri , trip ya tatu mzigo ukaja kupotea mazima bandarini. Wajapan hawakumwelewa kabisa wakahisi kawapiga tukio ila wakasema wafatilia wenyewe wajue mzigo ulipoenda. Wakati wanachunguza wakamwalika aende Japan kupoteza mawazo. Sasa sijui yaliyompata amerudi kavurugwa anaeleza vitu havieleweki mara walitaka kumkata mikono, mara kaingizwa chumba miili ya watu imening'inizwa. Kwa sasa yupo milembe kichwa imeruka kabisa na hatujui vizuri yaliyomsibu