Mrejesho: Kilichotokea baada ya mke wangu kurudi saa sita usiku

Mrejesho: Kilichotokea baada ya mke wangu kurudi saa sita usiku

Ndoa zina mambo mengi sana ya kupitia na nyakati nyingi tofauti, ukute ata uyo anayeshauri anaishi na mkewe uku kukiwa na rumours baadhi ya watoto sio wake lakini hana mpango wa kuachana na mkewe, wengi wanakurupuka na ushauri wa kuachana bila kuangalia pande zote mbili na watoto walionao wataishi katika hali gani, nafikiri ata wakisameheana wakaishi watakuwa na mwanzo mzuri wa amani ndani ya ndoa yao adi kuzeeka pamoja
Moja kati ya ushauri bora kabisa!
 
Achana na hiyo kondoo kifuatacho atakuua, mwanamke akifikia kuvua chupi kwa mwanaume mwingine huyo sio wako, jitenge na shetani man au komaa utazikwa
 
Mungu akubariki mkuu nakutabiria ustahimilivu ktk ndoa mda ukifika
Amina mkuu mengine tunayaexperience wenyewe afu watu wanakuja kubomoa ndoa za wenzao, na yeye afikirie mbona kama si mchepuko kumpotezea asingefika nyumbani kwake siku iyo? Na kwa vyovyote mchep naye alikuwa kwa mpenzi wake uko 😜😜😜
 
Pima watoto dna .kama kuna asiye wako aondoke naye piga chini milele
 
Baada ya mimi kurudi home siku ambayo wife hakutarajia ntarudi ,sikumkuta nyumbani na nilipompigia simu yy alijibu yupo home anaangalia tamthilia.

Nimekaa kuanzia saa moja usiku mpka saa sita usiku ndio anatokea,
Alipatwa na kama bumbuwaz hiv hakuamin km nipo home nilimnasa vibao akadondoka chin na kuomba nimsamehe haja fanya chochote kibaya

Nilimsikiliza lakin hakuwa na hoja yeyote ambayo inarizisha ukamwelewa yeye alisimamia msimamo wake huo alikuwa kwa shoga yake walikuwa wanaangalia muvi ndio maana kachelewa.

Alivyofika tu chakwanza kawahi kuchukua ndoo aende bafun akaoge niliamin kweli tayar kashaliwa
Sikumkagua huko chin sikuona km kuna haja ya kufanya hivo maana ni km uzalilishaji jibu linaonyesha tu ametoka kuliwa,alivyo maliza kuoga ,

Nikachukua simu yake na kumwambia toa password akawa hataki nikapiga ngumi ya uso akatoa password niliyo yakuta humo unaeza kuzimia,

Moja nikaenda kwny calls nikakutana na calls za jamaa za saa kumi na mbili kamili jion

Pili hamna calls hata moja inayo husisha rafiki yake inayo onyesha jana waliwasiliana kukutana

Tatu kwny whasp msg nikakutana na zajamaa pia na waliplan toka saa tano asubuh nilitaka niziweke humu but nimeshindwa kuweka ila ilikuwa km hivi

Jamaa:hey beautiful missed you

Mke: hey baby missing you more

Jamaa: missed your voice sana

Mke : thanks uko free leo?
Jamaa: yes tuonane bas please
Mke😱k ntakwambia.

Hiyo ilikuwa mida ya saa tano hivi asubuh hapa nakumbuka wife alipiga simu km mara 3 nikawa sikupokea nilikuwa kwny bus narud Dar na nililala nikakuta tu msg anasema
Hey baby nataka kujua unaendeleaje na unarudi lin? hapo nilimjibu Jmos usiku hiv akasema poa

Kwny saa kumi na mbili alimtafuta jamaa tena

Mke : hey uko wap tunakutana wap?
Jamaa:maaeneo ya studio kuna sehem inaitwa garden nini sijui..
Mke😛oa

Mke mida hiyo ndio kaenda na calls za jamaa ni kama saa 1830hrs nafikir alikuwa akimwelekeza

Yote hayo na msg zote hizo bado wife hajakubali km alikuwa kwa jamaa amekataa katakata

Msela aliye kutana nae kamsave LivingStone nakumbuka wakati tunakaa kijitonyama tulipanga nyumba moja na rafiki zake Mallow walikuwa wakiimba hapo na kuvuta bangi tu ile nyumba tulikuja kuhama hata kodi haijaisha na sikujua haswa tatizo nini pale ila alisistiza tu tuhame maji ni shida , nikasema poa nilitafta sehem nyingine nikalipa

Pale tukapangisha mwingine, mke alikuwa akiwasifia sifia anasema wajua kuimba ila bado hawajatoka kimziki but sikumzingatia ila namba
Wamepeana huko na ukichek jamaa ni yupo yupo anahaso na mziki mambo ya gym Bangibangi tu

Ila ndio hivo kila kitu kinamwisho wakuu akili kwangu kichwani wife kaliwa na and aground wa mziki sijui kwann wanawake wanapenda masela tu mambo ya gym nashangaa sana mtu kama huyo kuvunja ndoa yangu nipo nae toka 2016,

Wakuu ambo mko kwny ndoa mnanishaur nini?
hapa itabidi kutumia busara sana nmefanya nae vitu vingi na huyu manzi leo huu analiwa kimasihara tu inauma sana,

Cha kushangaza alimpigia simu jamaa ,alivyopokea tu jamaa inaonyesha ni wapenz na jamaa alikana ndio ww sio mpenz wangu but sio lazima niwe mpenz wako ndio ufanye .

Watoto wangu wawili mdogo ana 2years na mkubwa 4years wataishi bila Baba na mama pamoja inauma ila ndio itabid iwe hivo

Sintafanya haraka ntamwacha hapa kwny hii nyumba mimi ntaenda kupanga kwingine but watoto wangu atabaki nao yeye bado ni wadogo na ntafocus kuwahudumia na kuwasomeshe but
Itakuwa ngum sana kuwa nae tena wife haswa unapojua ameliwa na mtu wa dizan gan

Usaliti ni kitu kibaya sana wakuu leo hii Livingstone anavunja ndoa yangu hivhiv naona na katika kuchepuka kote sijawahi toka na mke wa mtu Kwann lkn imetokea kwangu?

Story hii ni ya kweli Mungu shahid hakuna nilipo ongeza japo sijaweza kuongea yote yalio tokea sintomaliza,

Hoja zake kubwa
1/ alifanya hivo kujifrahisha nafsi na haimaanishi alienda kwa jamaa
2/Kanitajia wanawake ambao yeye anahis mimi natoka nao katika hao mmoja niyule mchepuko wangu which is true
3/ jana alitoka kwenda kwarafiki yake kwa kuwa aliboreka home alikuwa alone

Hapaameamka na kwenda zake kazin na ubaya tunafanya sehem mmoja kaz,

Imeniuma sana wakuu sijalala kabisa leo hii iskie tu kwa mtu

Nawasilisha mtanisamehe kwa uandish nimevurugwa sana.

Unashauriwa kusoma kisa kilichotangulia: Leo nahisi mke wangu anachepuka huko alipoenda
Ndoa ndoana.... msamehe
 
Mwanaume anaathirika sana kisaikolojia, sema hawa wadada hawajui tu.

Nadhani ndo maana hata biblia imeruhusu kumuacha mke kwa habari ya uzinzi
Ni kweli mkuu, ni vile tu wanawake hawajui..
Tena huyu mleta uzi namsifu kwa ujasiri wa kuandika uzi, hiki ndiyo kimemsaidia ku "withstand" situation anayooitia.

Angekaa tu kimya bila kutoa la moyoni, angeweza kudondoka au kuua/kujiua
 
Umeongea vizuri ila hapo kusema hutaoa mmm
Mkuu nimeshuhudia marafiki baadhi waliachana na wake zao, wakaoa tena...
Maisha yao yakaenda vibaya zaidi.....basi ile hali ikawa kama imeniathiri.....nikajisema mfano itakee sioi....
Na nikioa labda uzeeni nitafute mzew mwenzangu wa kuzikana..
Maisha haya..[emoji119][emoji119][emoji26][emoji26][emoji119][emoji119]
 
Sijaoa ila principles ni hizi.

Mke akikukosa risasi, ama akakupiga lakini isikuue ama akakupiga panga ya shingo lakini bahati nzuri ukapona, msamehe na ongeza upendo kua zaidi ya ule wa mwanzo.

Lakini mke akichepuka kwa sababu yoyote ile usimsamehe.

Madhara ya mwanamke kuamua kuchepuka ni makubwa hatari zaidi kwenye maisha ya mume kuliko hata angempiga risasi.

Take it or leave it.
Kwa hiyo wanaume ndo wachepuke?
 
Tunaishi kwenye nyakati ambazo ni ngumu kuwatofautisha machangudoa na wanandoa......

Kuendelea kuishi na huyo mwanamke kutakusababishia sononeko la nafsi lisiloisha.......hilo sononeko litazalisha msongo wa mawazo utakaokufanya uwe Karibu na magonjwa yasiyoambukiza na kuyaweka hatarini maisha yako.....tiba pekee ni kukaa mbali na huyo mwanamke........pole sana kwa huo mtihani ndugu........
Napenda busara zako
 
Ni kweli mkuu, ni vile tu wanawake hawajui..
Tena huyu mleta uzi namsifu kwa ujasiri wa kuandika uzi, hiki ndiyo kimemsaidia ku "withstand" situation anayooitia.

Angekaa tu kimya bila kutoa la moyoni, angeweza kudondoka au kuua/kujiua

Ngoja waje wanawake nao waseme vile wanajisikia wakichitiwa [emoji3], sijui wao hawaathiriki kisaikolojia, wanaona poa tu kina baba mjengo wakiwa na mpango wa kando
 
Amina mkuu mengine tunayaexperience wenyewe afu watu wanakuja kubomoa ndoa za wenzao, na yeye afikirie mbona kama si mchepuko kumpotezea asingefika nyumbani kwake siku iyo? Na kwa vyovyote mchep naye alikuwa kwa mpenzi wake uko [emoji12][emoji12][emoji12]
Hongera mkuu binafsi ilishanitokea nikaangalia mdada wakuoa nikaona kizunguzungu nikamrudisha wife kwasasa heshima ipo watoto wanafuraha nahatua zamaisha kidogo zipo sikatai kama bado yapo lakini sijaona dalili
 
Mkuu nimeshuhudia marafiki baadhi waliachana na wake zao, wakaoa tena...
Maisha yao yakaenda vibaya zaidi.....basi ile hali ikawa kama imeniathiri.....nikajisema mfano itakee sioi....
Na nikioa labda uzeeni nitafute mzew mwenzangu wa kuzikana..
Maisha haya..[emoji119][emoji119][emoji26][emoji26][emoji119][emoji119]
Baba hii dunia ningumu nikujiandaa kukabiliana nayo tu wapo walioacha wake kwamazingira haya halafu wakaoa yaliyowakuta mwisho wakatamani bora hata kule mwanzo yani hawa watu kunamwingine anachepuka ila usimamizi wafamilia namipango ya maisha kila mtu anatamani kuwa nae
 
That's nature. Mwanaume akichepuka wanawake mnajisikia normal na kusamehe ni rahhsi, but kwa mwanaume haijawahi kuwa normal this is the reason why wanaume wana-react sn pale wake zao wakichepuka na ni ngumu sn kusamehe ukigundua umechapiwa.

Wewe ni me au ke? Kama ni mwanaume umejuaje kama wanawake wanajisikia normal tu wakichepukiwa? Umewahi kuwa mwanamke ukaiona hiyo hali vile inakuwa ukichepukiwa? Au mna assume tu mwanaume akichepuka mwanamke anajisikia normal tu [emoji848][emoji848]. Msiwasemee wanawake, na wao wanavurugukiwa mno wakisalitiwa. Usaliti unauma pande zote jamani [emoji42][emoji42]
 
Ni maamuzi yako Mkuu. Si kila ushauri lazima uufanyie kazi. Jana tumeona humu mchepuko anadai June 5, 2021 watakuwa wanasherehekea 15 years anniversary wamechoropoa mimba tatu na mtoto wa mwisho mchepuko anahisi yeye ni Baba.
Ushauri.kama huu
 
Back
Top Bottom