Mrejesho kuhusu vijana nane niliowasaidia

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
Wale vijana niliowasaidia kwa kuwapeleka site wakaungane na mafundi wangu(japo hawana ujuzi wa ufundi)

Baada ya kutangaza kwamba vijana wasio na ujuzi ila wanahitaji walau kutoboa kimaisha kwa kujifunza ujuzi wowote niliwachagua hawa nane kwa sababu zangu flani na usiriaz walioonyesha

Vijana wote nane niliwapokea nikawapeleka site Kibaha kiukweli wako serious sana na washaanza kujifunza na kujua vitu mbalimbali Kama vile :-

Kuskimu kuta & kupiga plasta
Kufunga system za maji (bomba)
Kupiga rangi

Wanajifunza na posho yao wanapata, nimemwambia msimamizi mpaka site hii inaisha anisaidie wawe wamejua vizuri kabisa na ana moyo wa kipekee anatumia muda mwingi kuwafundisha nadhani ujuzi huu utawasaidia kupata chochote kitu.

Najivunia kuona vijana wenye moyo wa kupambana.

Kama wewe ni kijana acha Kushinda ndani umelala na kuchat tu

Amka anza kufikiria kuhusu ugumu wa maisha yako na utatoboaje.

Toka nje tembea utafte koneksheni

Fanya kitu kwa ajili ya hatma ya maisha yako sio kulalamika maisha hayako fair au serikali haikujali

Acha Kushinda ndani unabet na kupiga nyeto tu.

Usiwe looser

Amsha akili yako acha ubwege
 
Mkuu tusomeshee ramani na sisi tulioajiriwa angalau tuweze kuingiza kipato kidogo tofauti na kusubiri mshahara
 
Ukipiga nyeto si unakuwa mvivumvivu pia huo mda ubao tumia kupiga nyeto ungeenda kutafuta kibarua usingekosa hata buku5 ya supu
Sasa mzee nyeto inahusiana vipi na mtu kukosa kazi.
 
Katika hao 8wangapi uliona wanajitambua🤔
 
Mkuu tusomeshee ramani na sisi tulioajiriwa angalau tuweze kuingiza kipato kidogo tofauti na kusubiri mshahara
Nitajitahidi nkipata muda kusaidiana ushauri na nini cha kufanya maana mi mwenyewe pamoja na hustle zangu lakini pia ni mtumishi wa serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…