Mrejesho kuhusu vijana nane niliowasaidia

Mrejesho kuhusu vijana nane niliowasaidia

Learn Or perish
EVioXflXQAIjsQU.jpg
 
Wale vijana niliowasaidia kwa kuwapeleka site wakaungane na mafundi wangu(japo hawana ujuzi wa ufundi)

Baada ya kutangaza kwamba vijana wasio na ujuzi ila wanahitaji walau kutoboa kimaisha kwa kujifunza ujuzi wowote niliwachagua hawa nane kwa sababu zangu flani na usiriaz walioonyesha

Vijana wote nane niliwapokea nikawapeleka site Kibaha kiukweli wako serious sana na washaanza kujifunza na kujua vitu mbalimbali Kama vile :-

Kuskimu kuta & kupiga plasta
Kufunga system za maji (bomba)
Kupiga rangi

Wanajifunza na posho yao wanapata, nimemwambia msimamizi mpaka site hii inaisha anisaidie wawe wamejua vizuri kabisa na ana moyo wa kipekee anatumia muda mwingi kuwafundisha nadhani ujuzi huu utawasaidia kupata chochote kitu.

Najivunia kuona vijana wenye moyo wa kupambana.

Kama wewe ni kijana acha Kushinda ndani umelala na kuchat tu

Amka anza kufikiria kuhusu ugumu wa maisha yako na utatoboaje.

Toka nje tembea utafte koneksheni

Fanya kitu kwa ajili ya hatma ya maisha yako sio kulalamika maisha hayako fair au serikali haikujali

Acha Kushinda ndani unabet na kupiga nyeto tu.

Usiwe looser

Amsha akili yako acha ubwege

Endelea kufanikiwa. Tanzania tunayoitaka!!
 
Back
Top Bottom