Mrejesho: Maboresho ya ramani ya nyumba yangu

Mrejesho: Maboresho ya ramani ya nyumba yangu

1. Madirisha yapo kwenye kila chumba, naona alisahau kuyaweka kwenye hii draft.

2. Office na laundry kwa life style yangu ni muhimu. Sijui kwa nini umeshauri niviondoe!!!

3. Umesema niongeze ukubwa wa sitting room. Sitting room ya 4*6 meters ni ndogo? Mbona naona kama inatosha kabisa?

4. Nitaongeza kidogo dining, ila Jiko la 3*3 ni dogo?

Ofisi kwa life la sasa hivi ni muhimu, hata isipokuwa ofisi inaweza kuwa bedroom tu, so kwangu ni sawa kuwa na ofisi. Kuna careers zinahitaji ofisi home.

Sitting room sio ndogo, ila uwiano unaweza usiwe sawa, 4x6 ni bora ikawa 5x5 au 6x5 ndio muonekano utakuwa mzuri zaidi...hapa tunaangalia uwiano tu.

Jiko la 3x3 pia sio dogo na sio kubwa. Siku hizi wanasema, angalia wapi utakuwa unatumia mda wako mwingi and make it spacious, kuna wanaotumia mda wao mwingi chooni, so choo kinakuwa spacious, wapo wanaokaa sana chumbani, wengine jiko linakuwa kubwa as wanapika mahanjumat sana. So, kufanya sehemu ya nyumba kuwa kubwa/ndogo unaangalia mda wako mwingi utatumia wapi.

Ingekuwa mimi ningefanya open kitchen, dining na jiko viungane, kutenganishwe na "breakfast table" tu.
 
Sebule Itakuwa na Giza...na hewa hafifu...halo kwenye ofisi ndo pangekuwa na sebule...then hiyo ofisi ndo uiweke uswekeni..
 
Ni kweli mkuu, kwenye ramani nyingi huwa haipo hivyo.... lakini ramani nyingi ni majiko ya kujitenga na Dining (closed kitchen).

Hii hapa ya open kitchen, si jiko na Dining ni chumba kimoja kirefu kilichoshikana? Kuweka mlango kwenye makutano ya jiko na dining (zinapokutana), si sawa tu? Ili jiko liwe na space ya makabati.

Au mimi ndio naona isivyo sahihi?
Open kitchen inawafaa wazungu ambao vyakula vyao vinginni vya kupasha kwenye oven na microwave msosi unakuwa tayari...mapishi ya bongo complicated mara wabandike maarage, mara nyama, .mAra makande, mara kitimito hapo sebuleni makochi yote yatakaa shombo...na hizo ceiling zitaota fungus kutokana na condensation zisizoeleweka..na hizo harufu za misosi mpaka iive unakuwa umeshiba harufu
 
Unakuwa na jiko la nje kwa ajili ya kuchemsha maharage na dagaa.
 
Back
Top Bottom