Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Nilivyosoma stori aisee,nimependa namna unavyoweka waz majibu ya mke...umepata mke mwenye hekima sana...ana majibu yenye busara na upole....nikirudi kwako....embu rahisisha tu mambo... Mwache aandike kwa jina lake maana hata
Wanawake nawapenda sana! Nyumba hii aiandike jina la mke; apambane ajenge na kiwanja chake ndicho aandike majina ya Watoto.
 
Usingemuambia kuhusu kumlipa hela, ungemueleza tu kuwa hiyo nyumba ya hapo ni mnaandika majina yenu. Kisha pesa ya kumlipa ukawekeza sehemu bila kumwambia, hiyo nyumba hata akiruhusu uandike jina lako kwa tamaa zake atakusumbua.

Sitisha maendelezo fanya yako ki jay mo.
 
Moja ya ushauri mbovu kabisa ni kuwaandika watoto kwenye nyumba au mali unazotafuta baba/mama...

Mali zote zinapaswa kuandikwa majina ya baba/mama, watoto wana nafasi yao lakini kamwe,kamwe kamweeee, usifanye makosa ya kuandika resources zako kwa majina yao, they are growing and they have their own roles to play kutengeneza maisha yao, wajibu wa wazazi ni kuwatengenezea watoto mazingira wezeshi kujiandalia kesho yao!

Mali zote ni za mke na mume, mpaka watakapofariki wote, then watoto warithi mali za wazazi wao, muhimu ni kuandika wosia tu na kuuhifadhi mahali salama bila watoto kujua wosia wako mpaka utakapojiridhisha kwamba wamejitengenezea maisha yao!

Narudia usithibutu kuwapenda watoto wako kwa kiwango cha kuwaandika kwenye kila resource yako, utawaharibu na watakuua kwa pressure...!
 

Ni ulimbukeni mwanaume kufikiri yeye ni kichwa na mmiliki, both you and your wife are selfish and uneducated..

Someni sheria. Hata ungeandika jina la nyau, Mali inayipatikana Mkiwa na Ndoa halali ni Mali yenu.

Kama mke wako alikuwa na kiwanja kabla ya ndoa, ujue anaweza kuwa na haki fulani kukizidi, umekosea kujenga.

Kama mwanaume na kichwa cha Familia. Achaneni na hizi harakati za kijinga ijengeni Familia.
 
Mkuu MBUZI kinachoendelea kwenye familia yako na kwangu kuko hivyo hivyo hapa nakaa kwenye nyumba ambayo kiwanja mke alikopa hela akanunua then tukaanza ujenzi tukahamia ila sikai nae hapa anakuja mara moja moja likizo na watoto kuna kipindi kulitokea mgogoro kidogo akadai anatafuta watu apauze( hati ya manunuzi ya kiwanja anayo yeye tena aliichukua kwa kuiiba na kule kuna jina lake) na hadi leo sijui kaificha wapi.

Hapa nimekaa mguu nje mguu ndani na nimeacha rasmi kufanya maendeleo yoyote kwenye hii nyumba. Najichanga nitafute kiwanja changu kimya kimya nijenge kimya kimya. Hawa wenzetu wana ubinafsi sana na hawafai kumiliki mali maana wana madharau flani hivi.

Aking'ang'ania kutaka umiliki mwachie mali zinatafutwa hizi.
 
Hivi kwanini wanawake hua wanakimbilia kusema mali ni za watoto?, kwanini wasi wajengee watoto wao maarifa ya kupambana na kupata vyao?

Binafsi,watoto wangu hawagusi mali yangu zaidi ya kuwajengea maarifa na akili za kutafuta chao.pia kuhusu mwamnake kuandika jina katika mali zako unakua umejiroga na kujijengea kaburi mwenyewe.

Kuhusiana na hii story, mkuu wewe ni mwanaume na kama mwanaume lazima ukubali kupambana, acha kufanya mambo kua magumu, jipange anza ujenzi katika kiwanja chako na kila kitu kitakua chako mengine funika kombe maana ulishayakanyaga mwenyewe kwa kuamua kwa kutumia hisia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Makosa yapo kwenye mazungumzo kulazisha jina la Kiwanja kuwa la Mwamme ni Dhambi na Dhuruma.

Ni bora jina la Kiwanja muamdika majina ya watoto wenu.

Huyo ni mwanamke mawazo yake tofauti ataanza kuuliza na kuomba ushauri kwa wengine, ushauri akipewa Mbaya ni tatizo
 
Hakuna haja ya kukimbizana na mke wako. Trust baina yenu is not there and it will not there. Primary concern should be the well being of your children and their. Embark on plan B. Anza kujenga upya maisha yako na watoto.

Don't expect that things will be the same again. Allow her to do whatever she thinks is OK. Fanya yako and you may or may not tell her.
 
Maamuzi yako yapo sawa kama mkeo anatoka kwa bwana, ila issue ya wewe kutangulia mbele za haki sio kitu ikiwa kwa sasa unaweza kuandikisha mali zako kama mirathi kabla halijatokea la kutokea... hapo sasa ndo uandike nani atabaki kuwa mmiliki wa nini.

Huwezi kusema unaogopa kuandika mirathi mapema na unahisi kama kujiombea kifo ilihali una hofu ya familia yako kuja kudhulumiwa yakitokea ya kutokea...

Note: kama mkeo hajatoka kwa bwana ukiandikisha jina lake umeisha issue ipo utajuaje maana binadamu hubadilika.
 
Limbwata tayari limeshafanya kazi😀
 
Mkuu
Nimesoma habari hii ya mrejesho kwa kituo lakini nilipogundua unatuhusisha masuala ya ndani kabisa ya familia yako nje ya mada kuu nimegundua kuwa unapitia wakati mgumu sana kwenye hiyo familia ambayo mkeo ndiye kiongozi wa familia huku wewe ukiwa ni wa pili yake.

Pia nimegundua kuwa hauna mshauri mzuri kutoka kwenye familia uliyozaliwa yaani kimsingi ukoo wenu hakuna wa kukushauri kama wapo basi kuna jambo umefanya wamekutenga au kukususa

Jambo la tatu, kapime DNA ya mwanao kisha kaa kiume kuamua future ya familia iweje.

Mambo mengine yanahitaji umri na kifua. Sisi wengine tunapitia misukosuko ya kifamilia lakini hautuoni kuja kuwaanika wenza wetu humu kwa sababu ni kweli tunatofautiana namna ya kumudu msongo lakini tunalinda staha za wenza hata kama wana upumbavu andamizi kama GENTAMYCINE🤣

Nakushauri,
Achana na hiyo project maana huyo mkeo hana muda mrefu na wewe. AshaanA kukuonesha namna usivyokuwa ndani ya nafsi yake. Wewe ni mpitanjia na kila dalili umeiweka kwenye huu uzi.

Ishi kwa akili
 
Nakwambia kwa uzoefu kama unaamua mke wako kila.kitu uandike kwa jina lake umejiroga.bora ungeandika kwa majina ya watoto.

Kama una hela tafuta na mali zako za siri lakini usisahau ilitokea la kutokea mnagawana pasu.

Aisee ndoa ni majanga.
Mm nimemuachia kila kitu hadi nimeanza upya mambo ya kesi siwezi nimechukua begi niko shamba NAJUA WANAUME HAWANIELEWA MAISHA NI MAPFUPI SANA HAKUNA ANAYEJUA KESHO YAKE MNAGOMBANIA UMILIKI WA PROPERTIES MNAISHIA KUUANA Yanini mie
 
Labda nakosea, labda sijui, kikubwa fuata moyo wako
Hapana, hukosei, uko sahihi, wazazi katika mipango yetu tunapaswa kwanza kuweka maslahi mbele ya watoto, kwa kuzingatia kuna kesho huenda mzazi mmoja au wote wasiwepo duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…