Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

hapana mimi namuona yuko sahihi, inaonesha mwanamke wake anataka kumpanda juu bila kumshirikisha yupo sahihi kabisa baba unatakiwa uwe na sauti yenye mamlaka wanawake tuna manyanyaso sana hapo akimpa hio ruhusa ya kujiandika jina la mwanamke bas wakigombana kidogo utasikia toka kwenye nyumba yangu yan hawa bila huyo mwanaume kua na sauti kama hivo atanyanyasika


unasema akajenge kwengine awaachie hii pia naipinga mwanamke ana kiwanja baba amejenga, baba ametaka anunue kiwanja ili amiliki vyote kihalali bila kunyanyaswa yupo sahihi tena akimpa hizo hela ampe kwa maandishi na mbele ya shahidi huyo mwanamke au wakiona wameshindwa kama inawezekana wawaandikishe watoti wao umiliki
Zingatia hili
 
Mkeo mbinafsi. Inaonekana anapata ushauri toka nje yenu. Inaweza ikawa ndugu au rafiki ambaye kwake amefanikiwa kufanya atakavyo.. Nakushauri yafuatayo;

1. Jina lazima liandikwe lako. Kama ambavyo ametamka anajuta kuolewa na wewe, siku moja atakutimua akiwa na hasira kama ambavyo ametamka hayo.

2. Hasira hazina mwisho. Na wenzetu hawa wanawake, wakipatwa na hasira lolote linaweza kuwatoka mdomoni. Na akiwa anamiliki vitu vyake ndani ya familia, kwa asiye na heshima na mumewe, atavitumia hivyo kukunyanyasa navyo. Hivyo piga ua, jina liandikwe lako.

3. Kwa familia za kiafrika zenye baba ndani, mara nyingi kama si zote mali huandikwa kwa jina la mume. Likiandikwa jina la mume maana yake ni mali za familia. Lakini zikiandikwa majina ya mke, mara nyingi, kama si zote mali huwa ni za mke. Nakumbuka kuna nyumba moja, Baba akinunua TV, mama naye ananunua. Baba akinunua hiki, mama ananunua kile. Kuna siku mama alisafiri. Wakati anawaaga watoto wake, akawaambia, nasafiri, lakini humu ndani TV fulani, Friji etc ni vyangu. Hata kama ntakufa huko hivyo ni vyangu, hence ni vyenu. Nikajiuliza vingi sana. Liwe jua iwe mvua andika jina lako.

4. Kitendo cha kusema apewe muda wa kufikiria, maana yake, hataki jina lao lionekane kwenye umiliki..!! Hapo anahitaji tu muda wa kupata ushauri toka anakopewaga ushauri. Ndoa yoyote ile, kama inaendeshwa na watu toka nje yenu (nje ya mke na mume), lazima ipitie matatizo mengi. Fuatilia kwa makini nani mshauri wake mkuu. Kama ni ndugu, basi itisha kikao cha familia, kamchane wazi. Ila kama mshauri huyo siyo ndugu, mtafute kamchane wazi mkiwa wawili wewe na yeye au ikibidi tengeneza mazingira ya kiurafiki then jifanye kama unamtoa out mkeo na huyo mshauri wake, yhen kamchane wazi wote wawili wakiwemo.

5. Tegemea kupewa majibu ambayo hutayapenda, yaani aandike jina lake kwenye umiliki. Jiandae kwa vurugu na matusi. Najua mwanaume kutukanwa unaweza ukafanya jambo kubwa baya. Lakini ukijiandaa kuwa kuna uwezekano wa jambo hilo kutokea, maana yake athari zinaweza zikapungua. Ukifanya kosa hapa mtaishia polisi. Ambako inaweza ikala kwako kwa namna yoyote ile, iwe kuhonga, kufungwa, kupoteza muda etc. Handle with care

6. Option ya mwisho wanayokuwa nayo wanawake ni kuondoka au kuvunja ndoa. Jua kuwa, huko anakoenda kupewa ushauri hatakuja na jibu la moja kwa moja. Ataanza kwanza kupima upepo au kutikisa kiberiti. Kwenye kutikisa kiberiti, njia moja wapo na kukuambia amechoka anarudi kwao..!! HAPA SIKUPI JIBU LA MOJA KWA MOJA, ILA JIANDAE NA HILO PIA.

KAZI KWAKO
Zingatia haya
 
Yafuatayo wanaume tubadilike

1---mtoto watoto hawana Chao kwetu wazazi(Mali zetu tunazochuma sisi sio zawatoto nizetu sisi wazazi wao). Kivuli hicho kiondolewe na ni ujinga wa hali ya juu


2---mwanume unajengaje katika kiwanja Cha mwanamke au mwanamke unajengaje kwenye kiwanja Cha mwanaume
**Kwenye SHERIA kunakitu kinaitwa kuchumwa Mali pamoja unapokuja kujenga nyumba kwenye kiwanja alijinunulia mtu kabla ya ndoa huo ni ujuha mkubwa Sana ,kwakweli TUBADILIKe

Mleta mada ,bomoa tofali zako kwenye hiyo nyumba uza maisha yaendelee kabla hamjua MSIISHIE kuPima UKIMwI tu , Jaribuni kusoma SHERIA ya ndoa na mchakato wa TALAKa kupata ufumbuzi wa mambo
 
Kwanza nikupe pole ingawa ni jambo jepesi kwa mwanaume aliekamilika na kujitambua. It's a very minor case.

Pili usitegemee km utapata majibu muafaka kutoka kwa jinsia ya KE maana muda wote lao huwa moja na kuona km wanaume wanawaonea.

Tatu, nimesoma msitari kwa mstari, neno kwa neno, kuna sentensi umesema mkeo aliwahi kukutamkia kuwa "anajuta kuolewa na wewe". Hapo wewe km kidume huoni maneno hayo yana maanisha zaidi ya yale yaliyopo moyoni mwake usio yaona? Ukizingatia inaonesha wewe unaishi mbali na familia yako kwa namna ulivyoelezea humu. Hapo mzee ukiona manyoa jua keshaliwa, na dalili za mvua ni mawingu lakini heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta.

USHAURI
Simamia hapohapo ulipo hivi sasa vinginevyo utajikuta siku moja unatupiwa virago km ambavyo wewe mwenyewe tayari umeshitukia.

Akikataa wazo lako la kumrudishia pesa za kiwanja, basi wewe pindua meza, mwambie yeye akurudishie pesa za ujenzi ulizotumia ili ukanunue kiwanja kingine na kujenga nyumba ya familia. Hiyo ya kwake atajua mwenyewe km atapangisha, kuuza, kumilikisha watoto au kuhonga.

Mwisho, kwa maelezo yako mkeo ni mbinafisi sana na anapenda kuwa juu Yako, na kuna watu wamemshikia akili ndio maana akasema ngoja akae ajifikirie juu ya maamuzi yako. Hivi ukimtongoza mwanamke akakwambia "ngoja nikajifikirie nitakupa jibu" hapo unadhani anaenda kufanya nini km sio kuulizia na kusimulia marafiki.

Kaza Jamba wewe ni mtoto wa kiume hata akienda kushitaki kwa ndugu zako kushitaki, wewe baki na msimamo wako maana familia ni yako na future ya watoto Iko mikononi mwako kwa sasa ambapo bado upo hai.
 
Mkuu Mbona unaongea Kama mtoto mdogo, hivi wewe kweli una Hata chumba kimoja kweli, yaani unasema muachie aandike jina lake na yeye ajenge Nyumba nyingine, hivi ujenzi Ni wa siku moja au? Unajua kipato Cha mleta hoja? Je Kama kastaafu na Sasa ndo kajenga!!?


Utakuwa unaishia kwa Shemeji yako wewe
Kiwanja na hati ni chake mwanamke, anakaa na watoto wako humo ndani na anaonekana selfish, nyumba ni vyumba viwili tuu (sio madharau), na watoto wako salama inaonekana, vitu vingine kama mwanaume unaachia tuu ili maisha yaendelee, labda mwenzetu unataka kuvunja nyumba uchukue tofali maana kiwanja sio chako
 
Yafuatayo wanaume tubadilike

1---mtoto watoto hawana Chao kwetu wazazi(Mali zetu tunazochuma sisi sio zawatoto nizetu sisi wazazi wao). Kivuli hicho kiondolewe na ni ujinga wa hali ya juu


2---mwanume unajengaje katika kiwanja Cha mwanamke au mwanamke unajengaje kwenye kiwanja Cha mwanaume
**Kwenye SHERIA kunakitu kinaitwa kuchumwa Mali pamoja unapokuja kujenga nyumba kwenye kiwanja alijinunulia mtu kabla ya ndoa huo ni ujuha mkubwa Sana ,kwakweli TUBADILIKe

Mleta mada ,bomoa tofali zako kwenye hiyo nyumba uza maisha yaendelee kabla hamjua MSIISHIE kuPima UKIMwI tu , Jaribuni kusoma SHERIA ya ndoa na mchakato wa TALAKa kupata ufumbuzi wa mambo
Aisee we jamaa mbona Kama umepiga vitu vikali mchana kweupe
 
Sasa nimeongea na mke wangu kuhusu nyumba ambayo nimejenga kwenye kiwanja chake kuhusu umiliki kwasababu yeye alitaka kuandika jina lake tena kwa Siri.

Nimemuuliza kwanza kwamba tangu tuoane hatujawahi kuongelea kuhusu hicho kiwanja chake.

Akanikumbusha kwamba wakati tunaoana Mimi nilimshauri akiuze na ilituletea mtafaruku kweli. Na ni kweli nilisita sana kujenga kwenye kiwanja cha mke wangu kwasababu nilishaona ni mtu mpenda vyake na asiye na muda na vyangu ilihali tayari sisi ni mke na mme.

Na niwarudishe kidogo kilichonifanya nimuona wa tofauti kidogo baada ya kuhamia pale siku moja mwisho wa mwezi nilienda kuitembelea familia.

Asubuhi tukiwa Mimi na watoto akaleta mada kwamba Joyce (sio jina halisi) ambaye yeye ni shangazi kwa Joyce. Joyce ameniomba Jack (sio jina halisi) yaani mtoto wa Joyce aje aishi hapa na aende shule akikaa kwetu.

Sasa Joyce tuliwahi kukaa naye kama ndugu yake mke wangu akawa anatusaidia kazi lakini alikuja kuondoka kwa ugomvi na mke wangu.

Aliponipa hizo histori akili yangu iliyafanya mrejeo haraka sana nikakumbuka jinsi Joyce alivyoondoka kwa shangazi yake kwa maneno.

Nikamwambia wife hilo kwasasa haitawezekana na sababu niliyompa ni kwamba mtoto wetu kwasasa anasoma English medium halafu huyu Jack akija aende shule ya kawaida ( serikali) Mimi sitajisikia vizuri na haitakuwa sawa hata kwa tafsiri za watu wengi. Nikamshauri kwamba kama ni kwa ajili ya kwenda shule basi aende kwa Shemeji ( kaka yake wife) ambaye kimsingi yupo karibu na shule hiyo ya serikali na ni baba mdogo wake Joyce. Mke wangu alikuja juu sana na kuzua ugomvi kidogo nimpige. Lakini maneno yaliyonikera sana ni kwamba Mimi siwataki ndugu zake na huwa nakuja hapa kuleta vurugu na kwamba anajuta kuolewa na mimi na akakimbilia nje baadae nilimuita akaje tukaongea nikaamua kutulia ili nione maisha yanaendaje baada ya pale.

Na hapa wiki moja kabla alinijulisha swala la kuwekewa bcone kwenye like eneo kwamba inahitahijika 100,000 akanipa na time limit sikutaka maneno nikampa ile hela akalipa niliporudi akanionesha risiti nikamwambia wafuatilie waweke. Wiki inayofuata akanitaarifu kwamba wameshaweka bcone lakini wanahitaji passport 7 kwa maandalizi ya hati nikamwambia sawa.
Nilipoenda nikamwambia ebu nenda idara ya maji ukaulizie utaratibu wa kupata maji kwa bomba binafsi yaani kufungiwa mita ya maji kwenye hiyo nyumba.

Alienda baadae akaniambia wanahitaji tujaze fomu na passport mbili na fomu hurusiwi kuchukua unajazia kule idara ya maji nikamwambia sawa. Jioni akaniambia kesho nataka nikapige zile picha ajaze hizo fomu na kupeleka zile picha 7 kwa ajili ya hati Mimi nikaitikia sawa. Asubuhi kulipokucha nikamwambia simamisha Hilo zoezi hadi nije. Lakini nilimpigia simu jamaa yangu ambaye naye amejaza hiyo fomu nikamuulizi hivi hizi fomu hurusiwi kutokana nazo ukajazie nyumbani? Jamaa akasema mbona Mimi nilijazie nyumbani nikarudisha!

Nikamwambia sawa. Mimi nilikuwa naendelea kukusanya data zangu. Jana nikafanya ziara ya kustukiza nikafika nyumba lakini nikiwa njiani niliandika sms kumjulia hali yeye na watoto nikamwambia nipo njiani nakuja huko. Basi nikafika yeye alikuwa ametoka na watoto nikafungua nikaingia nikampigia akasema anakuja na kweli wakawasili na watoto, watoto wangu wananipenda sana wakafurahi stori mbili tatu.
Mimi sitaka kikao kichukue muda nikaanza kikao na yeye nikamwambia Mimi nimekuja kwa mazungumzo na wewe akastuka sana. Nikamwambia mazungumzo ni ya kawaida ya kifamilia. Tukaongea nikamwambia hiki kiwanja si unajua ni chako akasema ndio. Nikamwambia lakini bahati nzuri tumejaliwa kujenga nyumba ya familia, akasema ndio. Nikamwambia kuna vitu tusipoyaweka sawa huko mbeleni vitatuletea shida akashangaa. Nikamwambia kwasasa tunaelekea kwenye swala la umiliki sasa tuamue Mimi na wewe mmliki wa nyumba ya familia yetu kwenye kiwanja chako kitakuwa na umiliki wa nani? Hana jibu! Nikamuuliza je maji na hilo suala la picha za hati miliki ungeandika? Akasema Mimi nilijua ni vitu vya kawaida Wala sikufikiria yote hayo! Nikamuuliza kwa mkuu wa familia ni nani akasema ni wewe ( Mimi). Nikamuuliza Sasa mbona siku ile ulifanya tu kunipa taarifa tu unataka kwenda kupiga picha bila kuuliza tuandike jina la nani? Akasema Mimi niliona hata nikiandika jina langu ni sawa tu na kwasababu nilikupa taarifa niliona hakuna shida.

Nikamwambia sasa Mimi natambua kwamba kiwanja ni chako lakini nimejenga nyumba ya familia yangu ambayo ni sisi sote. Nimekuja tupate mwafaka wa hicho kiwanja na Mimi nipo kwa ajili kuidhamini familia yangu na katika hii familia tunao jielewa kwasasa ni Mimi na wewe vijana wetu bado wadogo. Nikamwambia Mimi nina majibu yangu lakini nahitaji majibu yako juu ya kiwanja hiki. Nikamkumbusha; kwamba siku ile ulivyoongea maneno ya kwamba Mimi huwa nakuja kukuletea vurugu na kwamba unajuta kuolewa na mimi nilizingatia na hivyo sitakubaki kuiweka rehani familia kwa kuruhusu mambo yaende kiholela. Akahamaki na kudai kwanini namkumbusha mambo ya zamani nikamwambia haikuwa sehemu ya mada lakini nimeona nikukumbushe ili ujirekebishe kimawazo, kauli na kimtazamo na ufahamu mipaka yake kama mke. Akasema Yale alitamka kwa hasira kwasababu ulinikemea mbele ya watoto n.k nikamwambia Mimi uliniletea mada yako mbele ya watoto na nilipopinga wewe ndo ukaleta ugomvi. Akasema tuyamalize kwanza haya ndo tuje swala la umiliki wa nyumba. Ila nikamwambia Mimi siwezi tena kukuruhusu kumiliki hii nyumba kwasababu hutahili utashindwa kuzuia hisia zako na utaendelea kuropoka zaidi na huenda hata kuna siku utamleta mwanaume humu na sitaweza kuzuia. Naye akasema na wewe unaweza kumleta mwanamke halafu unitoe Mimi.

Mwisho akasema nimpe muda atafakari swala la umiliki wa hii nyumba halafu atanipa jibu kwamba hawezi kupata jibu la haraka. Lakini nimemwambia Mimi ndiye nina wajibu na jukumu la kulinda, kuhifadhi na kutunza mali za familia hivyo yeye ni mtu wa pili kutoka kwangu na akaona ugumu nipo tayari kumpa pesa yenye thamani ya kiwanja chake yeye atajua atazifanyaje hizo hela lakini kiwanja kiwe chini ya familia na chini yangu kama mwenyewe dhamana ya familia namba moja.

Kwa hiyo namsubiri aamue then nami nitaweka msimamo wa kiti. Japo sasa amenuna lakini mgonjwa haulizwi dawa. Mimi kiukweli sina plan B ya hilo nahitaji heshima iwepo kwangu kama mwenye nyumba na siwezi kuwa mtalii kwenye familia yangu. Lazima kiti kiheshimiwe bila hivyo panya watatawala.

Naomba kuwasilisha kwa ajili yenu kujifunza na kutoa ushauri.

Asanteni

Pia soma:
Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga
Daah
 
Mkuu, pole. Hope mtapata ufumbuzi mujarabu wa hiyo kadhia.
Mimi baada ya kuona jinsi wife anavyowapenda wanae (tuna watoto 2, mmoja miaka 5 mwingine miaka 2), nikaona sio kesi akiandika jina lake kwenye umiliki wa kiwanja. Mungu jaalia, tunaweza anza ujenzi mwakani, lakini hata nyumba nataka iwe Kwa majina yake. Sababu ni zipi?
1. Najua hawezi watelekeza watoto (labda apigwe ndumba), so pale patakuwa pa watoto. Hata likitokea la kutokea, siombei, watoto watakuwa na kwao.
2. Nimeshuhudia issues za mirathi, ndugu wamechukua mirathi ya watoto,(ilikuwa 19M). Yaani baba na mama wamekufa, mjomba akapewa zoezi la kusimamia mirathi ya marehemu dada yake, ndo mirathi ya wadogo wawili waliokuwa chini ya 18 ikapigwa. Nilijifunza kuwa mzazi, baba au mama atakuwa na uchungu zaidi na mali za watoto kuliko mtu wa nje.
Labda nakosea, labda sijui, kikubwa fuata moyo wako
Thubutuu

Kuna wanawake ukifariki anapata basha
Huyo basha anamdanganya danganya mwisho ana badili umiliki anakua anasomeka basha wake

Wanawake akili zao unazijua au unazisikia?

Au basha linamdanganya tuuze hapa tujenge pengne

Na huko wanakojenga basha anajiandika yeye
 
Unless nina miaka juu ya 45, ila kama ni below 45 siwezi kaa hapo nagombana na mwanamke kisa alinunua kiwanja nikajenga. Ntajenga tu nyingine, ya pili na ikiwezekana ya tatu. Na viwanja vilivyo vingi mpaka unanunua na kulipa kwa mafungu fungu nikae nabishana? Huo muda bora nitafute rejesho la kiwanja kipya. Halafu mwanamke ambaye hatuelewani kuhusu mali huyo hanifai. Tutalea tu watoto. Mambo ya kulogana na kuuana nani anataka.
 
Kama kweli una nia nzuri kwa mkeo na watoto basi fanya yafuatayo:-
1. Usilazimishe kuandika jina lako peke yako kwani hautakuwa tofauti na huyo mkeo anayetaka kuandika jina lake peke yake hata kwenye suala dogo tu la kuunganishiwa maji
2. Andikeni majina yenu wote wawili kwenye umiliki wa nyumba ili likitokea la kutokea msiisumbue mahakama bali mali igawanywe 50/50 fasta kila mtu afe na chake.
3. Ikishindikana ya kundika majina yenu wote wawili basi jilipuwe andika majina ya watoto wenu kama ambavyo umeshasema mwenyewe kuwa wewe huna shida sana na hiyo nyumba bali unapambania watoto wako wasije dhulumiwa jasho lako..
4. Usije kuachia hiyo nyumba kwa hasira kwani huyo mwanamke namna anavyokujibu ni kama tayari kashapata mwanaume mwenzio. Mbaya zaidi kama kashampenda hachelewi kumzawadia hiyo nyumba au hata akashauriwa kuiuza kama mchangiaji mmoja alivyoeleza hapo juu halafu waende wakajenge upya nyingine ili huyo mwanaume mwingine awe na umiliki au sehemu ya umiliki.
5. Tafuteni muda mkae wawili tu muulizane mlioana kwa ajili ya kujenga familia au mlioana ili mjenge nyumba halafu hiyo nyumba iiangukie ndoa yenu isambaratike. Jibu mtakalopata hapo kwa pamoja ndio litakalotoa mwelekeo wa ndoa yenu. Na hapo ndio kila mmoja wenu atachagua kusuka au kunyoa.

Mwisho kuanzia sasa kuwa na tahadhari sana na huyo mkeo kwa sababu huko anakokwenda kuchukua ushauri akikutana na washauri wajinga wajinga wasioelewa maana na thamanai ya ndoa ni nini hachelewi kulishwa matango pori akija shtuka ndoa yenu imeishaparaganyika kwa suala dogo tu la kugombea umiliki wa nyumba.
 
Hakuna ndoa pale, wanaelekea kwenye divorce wasipokuwa makini
Hatuombei hilo mkuu. Sema kuna wakati busara ingekuwa inauza ungenunua tu. Mimi sio kwamba ni mwema sana au mwenye busara sana hapana. Na wadau wanaweza kuona ni mbinafsi sana ila hapana ninachotetea pia inaweza kuonekana cha kibabe lakini sina lengo hilo ila ninahitaji kulinda kwamba mke wangu aendelee kuwa mke na Mimi niendelee kuwa mume na tuwe wazazi wa watoto wetu tukielewana. Sasa nafahamu mapungufu ya mwenzangu kwa muda tuliyoishi wa miaka sita sasa vyake huwa vinampa kiburi na hivyo kuhatarisha mahusiano yetu kama wana ndoa. Umiliki hata ikowa wangu wala sitakuwa na usumbufu wowote kwake yeye na watoto lakini popote nitakapokuwa niweze kutoa maelekezo yakafuatwa na familia ijengeke kwenye umoja na amani. Sio Jambo dogo ila najaribu kulitatua kwa umakini sana na naamini sitaharibu bali nitaiwekea msingi imara. Ikitokea huo muda aliyoomba kutafakari ndio ametumia kufuatilia huo utaratibu wa umiliki kwangu haitakuwa mshangao na sitapanic bado nitakuwa imara na maisha yatasonga. Watu wanasema naanika mambo ya familia yangu hahaha kwani mnanijua? Na sijamhusisha hata ndugu yangu Jambo hili bado lipo katika level yetu Kama familia ila humu wengine pia watajiifunza nami nitajifunza kutoka kwenu lakini mwisho wa siku Mimi ndio nitaamua kwa busara nilizojaliwa na ushauri mzuri kutoka kwenu wadau. Nashukuru matusi sio mengi mbarikiwe lakini mtuombee pia
 
Mkeo mbinafsi. Inaonekana anapata ushauri toka nje yenu. Inaweza ikawa ndugu au rafiki ambaye kwake amefanikiwa kufanya atakavyo.. Nakushauri yafuatayo;

1. Jina lazima liandikwe lako. Kama ambavyo ametamka anajuta kuolewa na wewe, siku moja atakutimua akiwa na hasira kama ambavyo ametamka hayo.

2. Hasira hazina mwisho. Na wenzetu hawa wanawake, wakipatwa na hasira lolote linaweza kuwatoka mdomoni. Na akiwa anamiliki vitu vyake ndani ya familia, kwa asiye na heshima na mumewe, atavitumia hivyo kukunyanyasa navyo. Hivyo piga ua, jina liandikwe lako.

3. Kwa familia za kiafrika zenye baba ndani, mara nyingi kama si zote mali huandikwa kwa jina la mume. Likiandikwa jina la mume maana yake ni mali za familia. Lakini zikiandikwa majina ya mke, mara nyingi, kama si zote mali huwa ni za mke. Nakumbuka kuna nyumba moja, Baba akinunua TV, mama naye ananunua. Baba akinunua hiki, mama ananunua kile. Kuna siku mama alisafiri. Wakati anawaaga watoto wake, akawaambia, nasafiri, lakini humu ndani TV fulani, Friji etc ni vyangu. Hata kama ntakufa huko hivyo ni vyangu, hence ni vyenu. Nikajiuliza vingi sana. Liwe jua iwe mvua andika jina lako.

4. Kitendo cha kusema apewe muda wa kufikiria, maana yake, hataki jina lao lionekane kwenye umiliki..!! Hapo anahitaji tu muda wa kupata ushauri toka anakopewaga ushauri. Ndoa yoyote ile, kama inaendeshwa na watu toka nje yenu (nje ya mke na mume), lazima ipitie matatizo mengi. Fuatilia kwa makini nani mshauri wake mkuu. Kama ni ndugu, basi itisha kikao cha familia, kamchane wazi. Ila kama mshauri huyo siyo ndugu, mtafute kamchane wazi mkiwa wawili wewe na yeye au ikibidi tengeneza mazingira ya kiurafiki then jifanye kama unamtoa out mkeo na huyo mshauri wake, yhen kamchane wazi wote wawili wakiwemo.

5. Tegemea kupewa majibu ambayo hutayapenda, yaani aandike jina lake kwenye umiliki. Jiandae kwa vurugu na matusi. Najua mwanaume kutukanwa unaweza ukafanya jambo kubwa baya. Lakini ukijiandaa kuwa kuna uwezekano wa jambo hilo kutokea, maana yake athari zinaweza zikapungua. Ukifanya kosa hapa mtaishia polisi. Ambako inaweza ikala kwako kwa namna yoyote ile, iwe kuhonga, kufungwa, kupoteza muda etc. Handle with care

6. Option ya mwisho wanayokuwa nayo wanawake ni kuondoka au kuvunja ndoa. Jua kuwa, huko anakoenda kupewa ushauri hatakuja na jibu la moja kwa moja. Ataanza kwanza kupima upepo au kutikisa kiberiti. Kwenye kutikisa kiberiti, njia moja wapo na kukuambia amechoka anarudi kwao..!! HAPA SIKUPI JIBU LA MOJA KWA MOJA, ILA JIANDAE NA HILO PIA.

KAZI KWAKO
Asante mkuu. Kweli kazi ni kwangu ila nashukuru kwa muda wako na ushauri.
 
Kuna watu wapuuzi kweli. Mpaka sasa kiwanja sio chako wala huna haki ya kiwanja. Hapo sanasana unaweza kubargain aandike muwa wamiliki wa pamoja (joint occupiers).

Ubabe unaoleta ungekuwa na maana kama kiwanja ungenunua wewe.
 
Kiufupi huyo mwanmke kwanza.amekuheshimu sana

Yaani kiwanja changu

Hata ujenge ghorofa jina la kiwanja linakua langu, hakuna mjadala.
Jina lako.labda liwe kwenye luku
 
Kaka mkeo hawezi kuwatelekeza watoto ila anaweza kukutelekeza wewe, shwetani akutoke kichwani haraka sana. Amka ulikolala kumekucha
Nani kakuambia mwanamke hawezi telekeza watoto wake? Wapo wangi tu wanatelekeza watoto akiwemo wifi yangu. Mali zinatakiwa ziandikwe majina ya wanandoa . Hata mkiachana hakuna sijui mali za watoto au la maana hawakuchangia kuzitafuta hizo mali.
 
Shukrani kwa ushauri mkuu. Ingawa kuandika majina hakumaanishi kumiliki. Hata nikiandika Kwa majina yangu haitimaanisha nina umiliki wa 100%, kwenye kutengana kuna kugawana 50/50.
Kwa taarifa yako ,anaweza kubadili umiliki kinyemela akaansika jina la mama yake mzazi. Siku mkiachana umiliki unaonekana wa mama yake, ndio itajua hujui
 
Hata sijataka kusoma uzi wote, nimeishia tu kudoma hizo sehemu za kufuatilia mambo muhimu unaishia kumtuma mkeo ndio afuatilie...

Hadi hapo nimepata picha aina ya mwanaume ulivyo, na ukiendelea na tabia hiyo ya uvivu utapigwa kama ngoma...
 
MBUZI MWENYE BUSARA mkuu naona hapa baadhi ya watu wanazidi kukushambulia ni wapumbavu hao na wataka sifa na kujifanya wao ni hawana tatizo lolote kwenye familia zao

Hiki unachokipigania wewe hata kwangu ni vilevile ila nimekaa nimetafakari mkuu MBUZI ebu achana na hicho kitu jitahidi kajenge kwenye uwanja ulionunua wewe kaweka husia kwamba hiki kiwanja na nyumba hii nikifa ni mali ya watoto wangu hakikisha mtoto mmoja anakuwepo mbele ya wakili na shahidi atakaesahini huo wosia then endelea na ujenzi kwenye kiwanja chako usiumie kwenye kiwanja cha huyo mwanamke na acha acha kabisa kufanya maendeleo yoyote fanya kama umetoa sadaka kwa hivyo vitofali vya chumba mbili sijui na sebule, mkeo mbinafsi mpotezee anza upya kwenye kiwanja chako.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom