Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Nakwambia kwa uzoefu kama unaamua mke wako kila.kitu uandike kwa jina lake umejiroga.bora ungeandika kwa majina ya watoto.

Kama una hela tafuta na mali zako za siri lakini usisahau ilitokea la kutokea mnagawana pasu.

Aisee ndoa ni majanga.
😅😅😅 Wacha tu nicheke ,ila Mwenyezi Mungu anijaalie maisha marefu angalau watoto-wakue na kujitegemea.
 
Hivi mwanamke mwenye mali na utajiri huwa wanafuata nini kwa Mwanaume?

Kwanini mwanamke tajiri naye huolewa?

Maana kama vile Kuna tatizo kwa mwanamke masikini akipata kitu kwenye mapenzi/mahusiano/ndoa.
 
Kaka mkubwa, naelewa hisia zako na naturally inafaa iwe hivyo, ila amini kitu kimoja siku utakuja gundua kwamba uliishi katika denial ya kumuamini mkeo kwa asilimia zote hizo hiyo disappointment utakayopata kama siyo jasiri unaweza pata msongo wa mawazo au maradhi yasiyoambikiza na pengine kufa kabisa .

Ishi kwa sheria moja kuu itakusadia sana " don't trust no fu&@#n body". Ndoa zina mauzauza pengine ambayo hukuwahi fikiria kama ungekutana nayo. Wanawake nowadays wamekuwa waki embrace sana issue za "freedom", wanahisi wanaweza ishi bila mwanaume, ile traditional life ya mume na mke haipo tena. Wanaume wengi tunapambana na kuishi kulea familia na maisha ya ndoa, while asilimia kadhaa ya wanawake wanaishi kwenye ndoa wakiwa na mission maalumu.
Shukrani sana mkuu kwa uzoefu. Labda nikupe tu sababu chache za kumuamini.
1. Namfahamu tokea kitambo kidogo (2006). Sijawahi sikia skandali.

2. Wakati namuoa seven years nilimkuta akiwa bado sealed. Hope you understand

3. Hana mambo mengi. Anaweza akakuachia simu yake ukakaa nayo hata siku nzima. Akikosea akaelekezwa, huwa anakiri makosa na kuomba msamaha, maisha yanaendelea.

4. Ana hofu kidogo ya Mungu. Huwa anajitahidi kufunga na kuomba.

5. She has brains you can trust. Siyo elimu ya darasani tu (PhD) lakini ana akili ya maisha pia.

6. Ni mpole na mkimya sana.
7. She has her own salary na sio mara moja au mbili alishaniboost project zangu zilipogoma.

Sio kwamba hana madhaifu, anayo, ila tokea nimemuoa mpaka sasa yanavumilika. Siwezi sema hatobadilika, I'm not a prophet. Will deal with the future kadri itakavyokuja.
 
Mfumo dume bado upo na utaendelea kiwepo, kuna nchi tendo ya ndoa mwanamke ndio anaamua akipe au asikupe na ukim force akienda police umekwisha
 
Mkuu, pole. Hope mtapata ufumbuzi mujarabu wa hiyo kadhia. Mimi baada ya kuona jinsi wife anavyowapenda wanae (tuna watoto 2, mmoja miaka 5 mwingine miaka 2), nikaona sio kesi akiandika jina lake kwenye umiliki wa kiwanja.

Mungu jaalia, tunaweza anza ujenzi mwakani, lakini hata nyumba nataka iwe Kwa majina yake. Sababu ni zipi?
1. Najua hawezi watelekeza watoto (labda apigwe ndumba), so pale patakuwa pa watoto. Hata likitokea la kutokea, siombei, watoto watakuwa na kwao.

2. Nimeshuhudia issues za mirathi, ndugu wamechukua mirathi ya watoto,(ilikuwa 19M). Yaani baba na mama wamekufa, mjomba akapewa zoezi la kusimamia mirathi ya marehemu dada yake, ndo mirathi ya wadogo wawili waliokuwa chini ya 18 ikapigwa.

Nilijifunza kuwa mzazi, baba au mama atakuwa na uchungu zaidi na mali za watoto kuliko mtu wa nje. Labda nakosea, labda sijui, kikubwa fuata moyo wako
Watu mnajiamini aisee.

Kwanini basi msiandike majina ya watoto!??
 
Mpe pesa yenye thamani ya kiwanja chake ndiyo heshima itafuata mkondo wake,wanawake akili zetu tunazijua wenyewe
 
Sasa nimeongea na mke wangu kuhusu nyumba ambayo nimejenga kwenye kiwanja chake kuhusu umiliki kwasababu yeye alitaka kuandika jina lake tena kwa siri. Nimemuuliza kwanza kwamba tangu tuoane hatujawahi kuongelea kuhusu hicho kiwanja chake.

Akanikumbusha kwamba wakati tunaoana mimi nilimshauri akiuze na ilituletea mtafaruku kweli. Na ni kweli nilisita sana kujenga kwenye kiwanja cha mke wangu kwasababu nilishaona ni mtu mpenda vyake na asiye na muda na vyangu ilihali tayari sisi ni mke na mume.

Na niwarudishe kidogo kilichonifanya nimuone wa tofauti kidogo baada ya kuhamia pale, siku moja mwisho wa mwezi nilienda kuitembelea familia. Asubuhi tukiwa mimi na watoto akaleta mada kwamba Joyce (siyo jina halisi) ambaye yeye ni shangazi kwa Joyce. Joyce ameniomba Jack (siyo jina halisi) yaani mtoto wa Joyce aje aishi hapa na aende shule akikaa kwetu.

Sasa Joyce tuliwahi kukaa naye kama ndugu yake mke wangu, akawa anatusaidia kazi lakini alikuja kuondoka kwa ugomvi na mke wangu. Aliponipa hizo stori akili yangu iliyafanya mrejeo haraka sana nikakumbuka jinsi Joyce alivyoondoka kwa shangazi yake kwa maneno.

Nikamwambia mke hilo kwasasa haitawezekana na sababu niliyompa ni kwamba mtoto wetu kwasasa anasoma 'English Medium' halafu huyu Jack akija aende shule ya kawaida (serikali) mimi sitajisikia vizuri na haitakuwa sawa hata kwa tafsiri za watu wengi.

Nikamshauri kwamba, kama ni kwa ajili ya kwenda shule basi aende kwa shemeji (kaka yake mke) ambaye kimsingi yupo karibu na shule hiyo ya serikali na ni baba mdogo wake Joyce. Mke wangu alikuja juu sana na kuzua ugomvi kidogo nimpige.

Lakini maneno yaliyonikera sana ni kwamba, mimi siwataki ndugu zake na huwa nakuja hapa kuleta vurugu na kwamba anajuta kuolewa na mimi na akakimbilia nje. Baadaye nilimuita, akaja tukaongea, nikaamua kutulia ili nione maisha yanaendaje baada ya pale.

Na hapa wiki moja kabla alinijulisha swala la kuwekewa 'bcone' kwenye like eneo, kwamba inahitahijika 100,000 akanipa na ukomo wa muda, sikutaka maneno nikampa ile hela akalipa. Niliporudi akanionesha risiti, nikamwambia wafuatilie waweke.

Wiki inayofuata akanitaarifu kwamba wameshaweka 'bcone' lakini wanahitaji paspoti saba kwa maandalizi ya hati nikamwambia sawa. Nilipoenda nikamwambia ebu nenda idara ya maji ukaulizie utaratibu wa kupata maji kwa bomba binafsi, yaani kufungiwa mita ya maji kwenye hiyo nyumba.

Alienda baadaye akaniambia wanahitaji tujaze fomu na paspoti mbili, na fomu hurusiwi kuchukua unajazia kule idara ya maji, nikamwambia sawa. Jioni akaniambia kesho nataka nikapige zile picha ajaze hizo fomu na kupeleka zile picha saba kwa ajili ya hati, mimi nikaitikia sawa.

Asubuhi kulipokucha nikamwambia simamisha hilo zoezi hadi nije. Lakini nilimpigia simu jamaa yangu ambaye naye amejaza hiyo fomu, nikamuulizi hivi hizi fomu hurusiwi kutokana nazo ukajazie nyumbani? Jamaa akasema mbona mimi nilijazie nyumbani nikarudisha?!

Nikamwambia sawa, mimi nilikuwa naendelea kukusanya taarifa zangu. Jana nikafanya ziara ya kustukiza, nikafika nyumba lakini nikiwa njiani niliandika ujumbe kumjulia hali yeye na watoto nikamwambia nipo njiani nakuja huko.

Basi nikafika yeye alikuwa ametoka na watoto, nikafungua nikaingia nikampigia akasema anakuja na kweli wakawasili na watoto, watoto wangu wananipenda sana wakafurahi stori mbili tatu.

Mimi sikutaka kikao kichukue muda, nikaanza kikao na yeye nikamwambia mimi nimekuja kwa mazungumzo na wewe, akastuka sana. Nikamwambia mazungumzo ni ya kawaida ya kifamilia. Tukaongea nikamwambia hiki kiwanja si unajua ni chako, akasema ndiyo.

Nikamwambia lakini bahati nzuri tumejaliwa kujenga nyumba ya familia, akasema ndiyo. Nikamwambia kuna vitu tusipoviweka sawa huko mbeleni vitatuletea shida, akashangaa. Nikamwambia kwasasa tunaelekea kwenye swala la umiliki sasa tuamue mimi na wewe mmliki wa nyumba ya familia yetu kwenye kiwanja chako kitakuwa na umiliki wa nani? Hana jibu!

Nikamuuliza je maji na hilo suala la picha za hati mmiliki ungeandika? Akasema mimi nilijua ni vitu vya kawaida wala sikufikiria yote hayo! Nikamuuliza kwa mkuu wa familia ni nani akasema ni wewe (mimi). Nikamuuliza sasa mbona siku ile ulifanya tu kunipa taarifa tu unataka kwenda kupiga picha bila kuuliza tuandike jina la nani? Akasema mimi niliona hata nikiandika jina langu ni sawa tu na kwasababu nilikupa taarifa niliona hakuna shida.

Nikamwambia sasa mimi natambua kwamba kiwanja ni chako lakini nimejenga nyumba ya familia yangu ambayo ni sisi sote. Nimekuja tupate mwafaka wa hicho kiwanja na mimi nipo kwa ajili kuidhamini familia yangu na katika hii familia tunaojielewa kwasasa ni mimi na wewe vijana wetu bado wadogo.

Nikamwambia mimi nina majibu yangu lakini nahitaji majibu yako juu ya kiwanja hiki. Nikamkumbusha, kwamba siku ile ulivyoongea maneno ya kwamba mimi huwa nakuja kukuletea vurugu na kwamba unajuta kuolewa na mimi nilizingatia na hivyo sitakubaki kuiweka rehani familia kwa kuruhusu mambo yaende kiholela.

Akahamaki na kudai kwanini namkumbusha mambo ya zamani, nikamwambia haikuwa sehemu ya mada lakini nimeona nikukumbushe ili ujirekebishe kimawazo, kauli na kimtazamo na ufahamu mipaka yake kama mke. Akasema yale alitamka kwa hasira kwasababu ulinikemea mbele ya watoto n.k, nikamwambia mimi uliniletea mada yako mbele ya watoto na nilipopinga wewe ndiyo ukaleta ugomvi.

Akasema tuyamalize kwanza haya ndiyo tuje swala la umiliki wa nyumba. Ila nikamwambia mimi siwezi tena kukuruhusu kumiliki hii nyumba kwasababu hustahili, utashindwa kuzuia hisia zako na utaendelea kuropoka zaidi na huenda hata kuna siku utamleta mwanaume humu na sitaweza kuzuia. Naye akasema na wewe unaweza kumleta mwanamke halafu unitoe mimi.

Mwisho akasema nimpe muda atafakari swala la umiliki wa hii nyumba halafu atanipa jibu kwamba hawezi kupata jibu la haraka. Lakini nimemwambia mimi ndiye nina wajibu na jukumu la kulinda, kuhifadhi na kutunza mali za familia hivyo yeye ni mtu wa pili kutoka kwangu na akaona ugumu nipo tayari kumpa pesa yenye thamani ya kiwanja chake, yeye atajua atazifanyaje hizo hela lakini kiwanja kiwe chini ya familia na chini yangu kama mwenyewe dhamana ya familia namba moja.

Kwa hiyo namsubiri aamue halafu nami nitaweka msimamo wa kiti. Japo sasa amenuna lakini mgonjwa haulizwi dawa. Mimi kiukweli sina mpango B ya hilo, nahitaji heshima iwepo kwangu kama mwenye nyumba na siwezi kuwa mtalii kwenye familia yangu. Lazima kiti kiheshimiwe bila hivyo panya watatawala.

Naomba kuwasilisha kwa ajili yenu kujifunza na kutoa ushauri.

Asanteni.

Pia soma: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga
mi najua hati huwa ni ya kiwanja, mmiliki wa kiwanja ndo mwenye haki
sasa wewe jombaa unajengaje kwenye kiwanja cha mwanamke
 
Acha tu sikujua hizo changamoto zingetokea. Ila hili limenivuruga kabisa. Yaani aliposema sema tuandike Majina yetu wote akapendekeza pia na kile kiwanja changu tufanye hivyo hivyo pia. Aise ni mtihani mkubwa.
 
Akikubali ushauri wa kurejeshewa pesa aliyonunulia kiwanja, mpe haraka sana kabla hajabadili wazo, kisha muandikishane upya mauziano (ingawa ni mkeo). Hakawii kukugeuka. Nawasilisha
 
Nimeona michango mingi ya watu ila sijaona ushauri wa Kisheria
Kama kuna mwanasheria Mbobezi na mzoefu naomba atuletee ufafanuzi wa kisheria juu ya hili
(nimesema Mwanasheria Mbobezi na mzoefu ni kimaanisha, kuna baadhi ya sheria huhitaji uzoefu zaidi ya mistari mtu aliyokaririshwa darasani)
 
Fangs kymwachia hio nyumba

Kwanza itakuwa ya wanao kwa vyovyote vile .. wewe Anza mchakato tafuta kiwanja chenye Jina lako na ujenge nyumba Yako ingine uwe na umiliki wa 100% utairithisha kwa wanao vile vile
 
Nakwambia kwa uzoefu kama unaamua mke wako kila.kitu uandike kwa jina lake umejiroga.bora ungeandika kwa majina ya watoto.

Kama una hela tafuta na mali zako za siri lakini usisahau ilitokea la kutokea mnagawana pasu.

Aisee ndoa ni majanga.
At least nashukuru Mungu wanawake wenye akili BADO wapo!
 
Mkuu

Mleta mada!!!

Umeniabisha Sana Man!

Nguvu za kujenga KWENYE kiwanja cha mwanamke ulizitoa wapi Mkuu!!?

Yaani ulizitoa KWA nani!?KWA Mungu au Mganga!!?

Si bora ungemwambia muwe mnalima mchicha tu!!?

Ulijichoma na kisu moyoni Mkuu!!

Huyo mama akikaza huchomoi kabisa!

Mwisho wa siku atakwambia toa NYUMBA yako ajenge yake utakuwa na guts!!?

Baba yangu mkubwa alioa wa kaskazini mwenye kiwanja akagoma kujenga pale!

Yule mama akazaa Mtoto mmoja hivi kama kiunganishi chao halafu akakomalia NDOA KWA Sana!Hadi ikafungiwa Baada ya kufungwa NDOA Afisa kilimo mifugo yule mzee alikufa KWA ajali ya pk pk miezi miwili Baada ya NDOA kufungwa!!Ni Baada ya migogoro isiyoisha ndani ya miezi hiyo MIWILI Baada ya NDOA yao!!

Mzee alizikwa mimi nikiwa kwenye UE chuo pale!

MIRATHI ilitoka mama kapiga bingo la maana na kujenga Bonge la NYUMBA KWENYE kiwanja chake!!

Yule Mtoto mdogo mmoja waliozaa nae alipewa fedha nyingi co bado mdogo has wengine wakapewa mil. Nane KILA mmoja walikuwa watatu wa walifiwa na mama yao kabla mzee hajamuoa huyo Maza!!

Ushauri

Andikeni Watoto halafu we sepa kaanzishe Maisha mengine usitafute kifo cha kujitakia!!

RIP Dad!

Nilikukataza usifunge NDOA mngeendelea na uchumba sugu Huo uliodumu miaka nane!!!

Writen
Kwa sasa amekubali tuandike Majina yetu Mimi na yeye hataki tuwaandike watoto. Lakini anataka tuandike hivyo halafu na kile kiwanja changu tuandike hivyo pia. Nyumba yenyewe sijamalizia naanza kufikiria kumwachia japo nawafikiria wanangu.
 
Sasa nimeongea na mke wangu kuhusu nyumba ambayo nimejenga kwenye kiwanja chake kuhusu umiliki kwasababu yeye alitaka kuandika jina lake tena kwa siri. Nimemuuliza kwanza kwamba tangu tuoane hatujawahi kuongelea kuhusu hicho kiwanja chake.

Akanikumbusha kwamba wakati tunaoana mimi nilimshauri akiuze na ilituletea mtafaruku kweli. Na ni kweli nilisita sana kujenga kwenye kiwanja cha mke wangu kwasababu nilishaona ni mtu mpenda vyake na asiye na muda na vyangu ilihali tayari sisi ni mke na mume.

Na niwarudishe kidogo kilichonifanya nimuone wa tofauti kidogo baada ya kuhamia pale, siku moja mwisho wa mwezi nilienda kuitembelea familia. Asubuhi tukiwa mimi na watoto akaleta mada kwamba Joyce (siyo jina halisi) ambaye yeye ni shangazi kwa Joyce. Joyce ameniomba Jack (siyo jina halisi) yaani mtoto wa Joyce aje aishi hapa na aende shule akikaa kwetu.

Sasa Joyce tuliwahi kukaa naye kama ndugu yake mke wangu, akawa anatusaidia kazi lakini alikuja kuondoka kwa ugomvi na mke wangu. Aliponipa hizo stori akili yangu iliyafanya mrejeo haraka sana nikakumbuka jinsi Joyce alivyoondoka kwa shangazi yake kwa maneno.

Nikamwambia mke hilo kwasasa haitawezekana na sababu niliyompa ni kwamba mtoto wetu kwasasa anasoma 'English Medium' halafu huyu Jack akija aende shule ya kawaida (serikali) mimi sitajisikia vizuri na haitakuwa sawa hata kwa tafsiri za watu wengi.

Nikamshauri kwamba, kama ni kwa ajili ya kwenda shule basi aende kwa shemeji (kaka yake mke) ambaye kimsingi yupo karibu na shule hiyo ya serikali na ni baba mdogo wake Joyce. Mke wangu alikuja juu sana na kuzua ugomvi kidogo nimpige.

Lakini maneno yaliyonikera sana ni kwamba, mimi siwataki ndugu zake na huwa nakuja hapa kuleta vurugu na kwamba anajuta kuolewa na mimi na akakimbilia nje. Baadaye nilimuita, akaja tukaongea, nikaamua kutulia ili nione maisha yanaendaje baada ya pale.

Na hapa wiki moja kabla alinijulisha swala la kuwekewa 'bcone' kwenye like eneo, kwamba inahitahijika 100,000 akanipa na ukomo wa muda, sikutaka maneno nikampa ile hela akalipa. Niliporudi akanionesha risiti, nikamwambia wafuatilie waweke.

Wiki inayofuata akanitaarifu kwamba wameshaweka 'bcone' lakini wanahitaji paspoti saba kwa maandalizi ya hati nikamwambia sawa. Nilipoenda nikamwambia ebu nenda idara ya maji ukaulizie utaratibu wa kupata maji kwa bomba binafsi, yaani kufungiwa mita ya maji kwenye hiyo nyumba.

Alienda baadaye akaniambia wanahitaji tujaze fomu na paspoti mbili, na fomu hurusiwi kuchukua unajazia kule idara ya maji, nikamwambia sawa. Jioni akaniambia kesho nataka nikapige zile picha ajaze hizo fomu na kupeleka zile picha saba kwa ajili ya hati, mimi nikaitikia sawa.

Asubuhi kulipokucha nikamwambia simamisha hilo zoezi hadi nije. Lakini nilimpigia simu jamaa yangu ambaye naye amejaza hiyo fomu, nikamuulizi hivi hizi fomu hurusiwi kutokana nazo ukajazie nyumbani? Jamaa akasema mbona mimi nilijazie nyumbani nikarudisha?!

Nikamwambia sawa, mimi nilikuwa naendelea kukusanya taarifa zangu. Jana nikafanya ziara ya kustukiza, nikafika nyumba lakini nikiwa njiani niliandika ujumbe kumjulia hali yeye na watoto nikamwambia nipo njiani nakuja huko.

Basi nikafika yeye alikuwa ametoka na watoto, nikafungua nikaingia nikampigia akasema anakuja na kweli wakawasili na watoto, watoto wangu wananipenda sana wakafurahi stori mbili tatu.

Mimi sikutaka kikao kichukue muda, nikaanza kikao na yeye nikamwambia mimi nimekuja kwa mazungumzo na wewe, akastuka sana. Nikamwambia mazungumzo ni ya kawaida ya kifamilia. Tukaongea nikamwambia hiki kiwanja si unajua ni chako, akasema ndiyo.

Nikamwambia lakini bahati nzuri tumejaliwa kujenga nyumba ya familia, akasema ndiyo. Nikamwambia kuna vitu tusipoviweka sawa huko mbeleni vitatuletea shida, akashangaa. Nikamwambia kwasasa tunaelekea kwenye swala la umiliki sasa tuamue mimi na wewe mmliki wa nyumba ya familia yetu kwenye kiwanja chako kitakuwa na umiliki wa nani? Hana jibu!

Nikamuuliza je maji na hilo suala la picha za hati mmiliki ungeandika? Akasema mimi nilijua ni vitu vya kawaida wala sikufikiria yote hayo! Nikamuuliza kwa mkuu wa familia ni nani akasema ni wewe (mimi). Nikamuuliza sasa mbona siku ile ulifanya tu kunipa taarifa tu unataka kwenda kupiga picha bila kuuliza tuandike jina la nani? Akasema mimi niliona hata nikiandika jina langu ni sawa tu na kwasababu nilikupa taarifa niliona hakuna shida.

Nikamwambia sasa mimi natambua kwamba kiwanja ni chako lakini nimejenga nyumba ya familia yangu ambayo ni sisi sote. Nimekuja tupate mwafaka wa hicho kiwanja na mimi nipo kwa ajili kuidhamini familia yangu na katika hii familia tunaojielewa kwasasa ni mimi na wewe vijana wetu bado wadogo.

Nikamwambia mimi nina majibu yangu lakini nahitaji majibu yako juu ya kiwanja hiki. Nikamkumbusha, kwamba siku ile ulivyoongea maneno ya kwamba mimi huwa nakuja kukuletea vurugu na kwamba unajuta kuolewa na mimi nilizingatia na hivyo sitakubaki kuiweka rehani familia kwa kuruhusu mambo yaende kiholela.

Akahamaki na kudai kwanini namkumbusha mambo ya zamani, nikamwambia haikuwa sehemu ya mada lakini nimeona nikukumbushe ili ujirekebishe kimawazo, kauli na kimtazamo na ufahamu mipaka yake kama mke. Akasema yale alitamka kwa hasira kwasababu ulinikemea mbele ya watoto n.k, nikamwambia mimi uliniletea mada yako mbele ya watoto na nilipopinga wewe ndiyo ukaleta ugomvi.

Akasema tuyamalize kwanza haya ndiyo tuje swala la umiliki wa nyumba. Ila nikamwambia mimi siwezi tena kukuruhusu kumiliki hii nyumba kwasababu hustahili, utashindwa kuzuia hisia zako na utaendelea kuropoka zaidi na huenda hata kuna siku utamleta mwanaume humu na sitaweza kuzuia. Naye akasema na wewe unaweza kumleta mwanamke halafu unitoe mimi.

Mwisho akasema nimpe muda atafakari swala la umiliki wa hii nyumba halafu atanipa jibu kwamba hawezi kupata jibu la haraka. Lakini nimemwambia mimi ndiye nina wajibu na jukumu la kulinda, kuhifadhi na kutunza mali za familia hivyo yeye ni mtu wa pili kutoka kwangu na akaona ugumu nipo tayari kumpa pesa yenye thamani ya kiwanja chake, yeye atajua atazifanyaje hizo hela lakini kiwanja kiwe chini ya familia na chini yangu kama mwenyewe dhamana ya familia namba moja.

Kwa hiyo namsubiri aamue halafu nami nitaweka msimamo wa kiti. Japo sasa amenuna lakini mgonjwa haulizwi dawa. Mimi kiukweli sina mpango B ya hilo, nahitaji heshima iwepo kwangu kama mwenye nyumba na siwezi kuwa mtalii kwenye familia yangu. Lazima kiti kiheshimiwe bila hivyo panya watatawala.

Naomba kuwasilisha kwa ajili yenu kujifunza na kutoa ushauri.

Asanteni.

Pia soma: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga
Safi Sana mkuu maamuzi mazuri
 
Kwa sasa amekubali tuandike Majina yetu Mimi na yeye hataki tuwaandike watoto. Lakini anataka tuandike hivyo halafu na kile kiwanja changu tuandike hivyo pia. Nyumba yenyewe sijamalizia naanza kufikiria kumwachia japo nawafikiria wanangu.
Usikubali mkuu!

Andika Watoto TU!!

Kama ndoa ina migogoro usikubali huo mkenge!!!

Mtaviziana kama wachawi vile!

Mwanamke anayepinga wanawe wasiandikwe kwenye hati ni hatari Sana!!

Kinachomfanya aogope kufanya Hivyo Ndio hatari Zaidi!

Wachout!
 
Wanaume tunapitia magumu sana, mm sikupi pole ila nakushauri uendelee kuwa na msimamo wa unachokitaka.

Ukijilegeza tu UMEKWISHA.
Alikosea jambo moja.
Ni onyo kuchangia fedha au mali na mwanamke.
Alikosea sana kujenga nyumba kwenye kiwanja cha mwanamke.
Mimi mwanamke akiniambia tuchangie fedha kwa ajili ya jambo fulani, yeye afanye yake na mimi yangu.
Tulikutana ukubwani kwahiyo lolote linaweza kutokea
 
Back
Top Bottom