Nilivyosoma stori aisee, nimependa namna unavyoweka wazi majibu ya mke, umepata mke mwenye hekima sana, ana majibu yenye busara na upole.
Nikirudi kwako, embu rahisisha tu mambo. Mwache aandike kwa jina lake maana hata kiwanja ni chake, yaan ukiona MTU anakwambia ngoja nikajifikirie ujue bado hajaafiki, watoto analea mama pale ,wewe unakuja Mara mojamoja, kwann usimwamini mkeo, mbona kama umekaa attention sana.
Hata mkiachana kwa ajili ya watoto bado itakubidi uwaachie Nyumba(kwa mwanaume Mwenye akili hawez taka watoto wataabike pa kuishi), ulisema una kiwanja kama ulivyosema wewe ni mwanaume ,kichwa cha familia em pambana tena jenga kwenye kiwanja chako then waandike wanao.
Usitumie ubabe, tafadhali mwachie tu kama zawadi hiyo Nyumba. Ni mkeo huyo analea na kuishi hapo na watoto wako.(usipojiangalia, ndoa yako ndo inaenda kufall apart Mkuu)