Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Duu u
Sifanye hivyo aisee hawa viumbe usile nao maagano. Andika jina lako tu kama ni mke wa ndoa hakuna wa kuwahangaisha. Wala usiandike jina la mtoto plz jitahdin kujifunza kutokana na historia.

Ukitaka kuwajua hawa viumbe kosa kaz mwaka ushindwe kuhudumia nyumba Ndio utajua hujui.
 
hapana mimi namuona yuko sahihi, inaonesha mwanamke wake anataka kumpanda juu bila kumshirikisha yupo sahihi kabisa baba unatakiwa uwe na sauti yenye mamlaka wanawake tuna manyanyaso sana hapo akimpa hio ruhusa ya kujiandika jina la mwanamke bas wakigombana kidogo utasikia toka kwenye nyumba yangu yan hawa bila huyo mwanaume kua na sauti kama hivo atanyanyasika


unasema akajenge kwengine awaachie hii pia naipinga mwanamke ana kiwanja baba amejenga, baba ametaka anunue kiwanja ili amiliki vyote kihalali bila kunyanyaswa yupo sahihi tena akimpa hizo hela ampe kwa maandishi na mbele ya shahidi huyo mwanamke au wakiona wameshindwa kama inawezekana wawaandikishe watoti wao umiliki
 
Mkuu una ka element ka kitapeli. Andikeni majina yenu yote kwenye hati na sio eti kutaka kuwa kichwa cha nyumba kwa kupachika jina lako pekee. Kiwanja ni chake. Pesa unayotaka kumfidia kajenge kwenye kiwanja chako. Unachowaza leo hujui kitawasumbua vipi wanao miaka ijayo
 
Barikiwa Dada,ni kweli
 
Mkeo mbinafsi. Inaonekana anapata ushauri toka nje yenu. Inaweza ikawa ndugu au rafiki ambaye kwake amefanikiwa kufanya atakavyo.. Nakushauri yafuatayo;

1. Jina lazima liandikwe lako. Kama ambavyo ametamka anajuta kuolewa na wewe, siku moja atakutimua akiwa na hasira kama ambavyo ametamka hayo.

2. Hasira hazina mwisho. Na wenzetu hawa wanawake, wakipatwa na hasira lolote linaweza kuwatoka mdomoni. Na akiwa anamiliki vitu vyake ndani ya familia, kwa asiye na heshima na mumewe, atavitumia hivyo kukunyanyasa navyo. Hivyo piga ua, jina liandikwe lako.

3. Kwa familia za kiafrika zenye baba ndani, mara nyingi kama si zote mali huandikwa kwa jina la mume. Likiandikwa jina la mume maana yake ni mali za familia. Lakini zikiandikwa majina ya mke, mara nyingi, kama si zote mali huwa ni za mke. Nakumbuka kuna nyumba moja, Baba akinunua TV, mama naye ananunua. Baba akinunua hiki, mama ananunua kile. Kuna siku mama alisafiri. Wakati anawaaga watoto wake, akawaambia, nasafiri, lakini humu ndani TV fulani, Friji etc ni vyangu. Hata kama ntakufa huko hivyo ni vyangu, hence ni vyenu. Nikajiuliza vingi sana. Liwe jua iwe mvua andika jina lako.

4. Kitendo cha kusema apewe muda wa kufikiria, maana yake, hataki jina lao lionekane kwenye umiliki..!! Hapo anahitaji tu muda wa kupata ushauri toka anakopewaga ushauri. Ndoa yoyote ile, kama inaendeshwa na watu toka nje yenu (nje ya mke na mume), lazima ipitie matatizo mengi. Fuatilia kwa makini nani mshauri wake mkuu. Kama ni ndugu, basi itisha kikao cha familia, kamchane wazi. Ila kama mshauri huyo siyo ndugu, mtafute kamchane wazi mkiwa wawili wewe na yeye au ikibidi tengeneza mazingira ya kiurafiki then jifanye kama unamtoa out mkeo na huyo mshauri wake, yhen kamchane wazi wote wawili wakiwemo.

5. Tegemea kupewa majibu ambayo hutayapenda, yaani aandike jina lake kwenye umiliki. Jiandae kwa vurugu na matusi. Najua mwanaume kutukanwa unaweza ukafanya jambo kubwa baya. Lakini ukijiandaa kuwa kuna uwezekano wa jambo hilo kutokea, maana yake athari zinaweza zikapungua. Ukifanya kosa hapa mtaishia polisi. Ambako inaweza ikala kwako kwa namna yoyote ile, iwe kuhonga, kufungwa, kupoteza muda etc. Handle with care

6. Option ya mwisho wanayokuwa nayo wanawake ni kuondoka au kuvunja ndoa. Jua kuwa, huko anakoenda kupewa ushauri hatakuja na jibu la moja kwa moja. Ataanza kwanza kupima upepo au kutikisa kiberiti. Kwenye kutikisa kiberiti, njia moja wapo na kukuambia amechoka anarudi kwao..!! HAPA SIKUPI JIBU LA MOJA KWA MOJA, ILA JIANDAE NA HILO PIA.

KAZI KWAKO
 
Hiyo nyumba ni ya mwanamke jipe muda tuu. Samahani sijaongea ulichotaka kusikia.
Haya uliyoyasema ni ya zamani..!! Siku hizi tathmini inafanywa ya eneo pekee na kilichomo juu ya eneo peke yake..!! Halafu hata mkiachana, zile mambo za kusema nyumba inabaki kwa wtoto yameshabadilika..!! Mnaambiwa hata kama msingekuwa na nyumba au mali au eneo, watoto mngewalea tu..!! Hivi vinathaminishwa na kupigwa bei halafu mnagawana kilichopatikana.
 
Na mwanamke unakubalije kufidiwa pesa na mumeo huku mko ndani ya ndoa?
 
Shukrani kwa ushauri mkuu. Ingawa kuandika majina hakumaanishi kumiliki. Hata nikiandika Kwa majina yangu haitimaanisha nina umiliki wa 100%, kwenye kutengana kuna kugawana 50/50.
 
Wanaume tunapitia magumu sana, mm sikupi pole ila nakushauri uendelee kuwa na msimamo wa unachokitaka.

Ukijilegeza tu UMEKWISHA.
Mbona mnawekana kwenye mkao wa kuachana? Mwenye kiwanja ndiye mwenye nyumba. Sasa ataandikaje jina lako wakati 'hati' inasoma jina lake?
 
Huyo mwanamke paka kutaka hela ya hiko kiwanja umpe kuna uwalakini.maana hiyo nyumba ni yenu wote,ila tu wewe unakuwa msimamizi namba moja.

Huwezi kuuza bila kushirikiana na mke,hawa wanawake wanashida sana,mimi mjengo wangu mwanzo mwisho simshirikishi mwanamke atoe hata cent yake..
 
Kazia hapo hapo mkuu. Nakuunga mkono asilimia 100
 
Kuna siku utatimuliwa nyumbani
 
Kuna siku utatimuliwa nyumbani
🤣🤣🤣. Nina ka-salary ka kunipush siku mbili tatu mkuu. Sintoshindwa kujipanga na kujenga hata ka-master na sebule vya kuzeekea. Ila nitakuwa nimewaacha watoto wakiwa na nyumba. Najua, hatawatelekeza
 
Mkuu Mbona unaongea Kama mtoto mdogo, hivi wewe kweli una Hata chumba kimoja kweli, yaani unasema muachie aandike jina lake na yeye ajenge Nyumba nyingine, hivi ujenzi Ni wa siku moja au? Unajua kipato Cha mleta hoja? Je Kama kastaafu na Sasa ndo kajenga!!?


Utakuwa unaishia kwa Shemeji yako wewe
 
Kweli..aacha mawenge....Tena angeandika watoto kama vipi...Mimi sioni shida..hiyo nyumba kwa mazingira yalivyo..pia hata angeandika mke sawa tu..Mimi sioni shida..hata kama kesho aseme tuachane..binafsi Siwezi kwenda kugombea eti hiyo nyumba..big no.

Wewe mwanaume bhana, fight Jenga kwingwine andika watoto kama vipi..

Kwa kifupi huyo mke hawezi kutelekeza watoto hata siku Moja...ataishi nao humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…