Mrejesho: Msaada, nataka kujiua, shukrani wana JF kwa msaada wenu mkubwa

Mrejesho: Msaada, nataka kujiua, shukrani wana JF kwa msaada wenu mkubwa

Mbwa kala mbwaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
218
Reaction score
389
Habari ya jioni ndugu zangu wa Jf. Kwanza nimshukuru Mungu wetu Mwema katika jina la Yesu kwa kutulinda na kututunza hata Leo.

Takribani miaka 10 liyo pita, nilipata tatizo la akili yangu mnamo mwaka 2007 na kulazimika kuacha masomo niliyo kua naendelea nayo UDSM na kulazwa Psychiatric unit Muhimbili. Nilipewa madawa niliyo takiwa kuendelea kutumia maisha yote huku nikienselea kuhudhuria clinic zao. Hata hivyo, hali ilikua mbaya 2008 na 2010 nikachanganyikiwa mazima na kutoweka nyumbani kwenda kuokota makopo barabarani. Nilitafutwa na kupatikana na kurudishwa hospital niliko ruhusiwa 2011 March. Hali ilitulia kiasi, ila nikawa nasumbuliwa Sana na hali ya kutaka kujiua!!!

Mwaka 2013 May, nilileta Uzi juu hapa:

MSAADA, Nataka KUJIUA

Nashukuru sana kwa maoni na ushauri wa wadau hapa ambao ulinipa mwanga mwingine.

Kilicho tokea:

1: Nili engage kwenye kumtafuta Mungu katika maombi na kuombewa.

2: Hali ya kutaka kujiua na maumivu vilitoweka kabisa by July

3: August nilirudi hospital kupimwa na kukutwa nimepona kabisa tatizo lililo kua linanisumbua hali iliyo washamgaza hata madaktari!!!!

4: Mwezi October nilirudi Chuoni na kuhitimu 2015.

Kwa sasa ninafanya biashara na nimebariki wengine kwa kujiri jumla ya watu sita.

UTUKUFU WOTE KWA MUNGU.

USHAURI:

Ndugu wana Jf, mtu anapo leta issue yake tusiwe haraka kutukana na kukejeli. Kuna watu walinitukana kwenye Uzi ule ila Mungu awabariki wote mlio nishauri na sasa ni mzima wa afya.

Mbarikiwe wote.
 
Pole sana.
Umepona si kwasababu ya Mungu, bali matibabu toka hospitalini.
Mungu asingekubali upate mateso yote afu ane akuponye.
Mkuu, nilikua nitumie dawa zile hadi naingia kaburini, ubongo ulikua na shida, baada ya maombi, nilipimwa na ubongo kukutwa sawa, kitu ambacho madaktar wenyewe walikiri hawaelewi imekuaje na sikuendelea na dawa tena huu ni mwaka wa NNE. Ni Mungu aliniponya, hii case ilishindikana kidaktari.
UTUKUFU WOTE KWA YESU KRISTO!!!
 
Back
Top Bottom