Mrejesho: Msaada, nataka kujiua, shukrani wana JF kwa msaada wenu mkubwa

Mrejesho: Msaada, nataka kujiua, shukrani wana JF kwa msaada wenu mkubwa

Aiseee ushuhuda kama huu unanifanya nitoe machozi hakika Mungu wetu ni mkuu..

Na amekufanya uwe kichwa na amebariki kazi ya mikono yako..

Usiache kumsifu na kumtukuza m happy for you bro like for real hii story imenigusa sanah japo sikujui na machozi yamenitoka
 
Aiseee ushuhuda kama huu unanifanya nitoe machozi hakika Mungu wetu ni mkuu..

Na amekufanya uwe kichwa na amebariki kazi ya mikono yako..

Usiache kumsifu na kumtukuza m happy for you bro like for real hii story imenigusa sanah japo sikujui na machozi yamenitoka
Mungu anabaki kua Mungu. Ubarikiwe mkuu
 
Aisee umeniongezea nguvu ya maombi, umenifanya niendelee kuamini iko siku na mimi atanipa mtoto, Barikiwa sana
Pole sana Mama. Mungu ni tumaini la waliopoteza tumaini. Endelea kumtumainia.
 
Sasa nimeelewa kumbe nina wengine humu huwa wanaleta mada na kuchangia mada wakiwa abnormal
 
Habari ya jioni ndugu zangu wa Jf. Kwanza nimshukuru Mungu wetu Mwema katika jina la Yesu kwa kutulinda na kututunza hata Leo.

Takribani miaka 10 liyo pita, nilipata tatizo la akili yangu mnamo mwaka 2007 na kulazimika kuacha masomo niliyo kua naendelea nayo UDSM na kulazwa Psychiatric unit Muhimbili. Nilipewa madawa niliyo takiwa kuendelea kutumia maisha yote huku nikienselea kuhudhuria clinic zao. Hata hivyo, hali ilikua mbaya 2008 na 2010 nikachanganyikiwa mazima na kutoweka nyumbani kwenda kuokota makopo barabarani. Nilitafutwa na kupatikana na kurudishwa hospital niliko ruhusiwa 2011 March. Hali ilitulia kiasi, ila nikawa nasumbuliwa Sana na hali ya kutaka kujiua!!!

Mwaka 2013 May, nilileta Uzi juu hapa:

MSAADA, Nataka KUJIUA

Nashukuru sana kwa maoni na ushauri wa wadau hapa ambao ulinipa mwanga mwingine.

Kilicho tokea:

1: Nili engage kwenye kumtafuta Mungu katika maombi na kuombewa.

2: Hali ya kutaka kujiua na maumivu vilitoweka kabisa by July

3: August nilirudi hospital kupimwa na kukutwa nimepona kabisa tatizo lililo kua linanisumbua hali iliyo washamgaza hata madaktari!!!!

4: Mwezi October nilirudi Chuoni na kuhitimu 2015.

Kwa sasa ninafanya biashara na nimebariki wengine kwa kujiri jumla ya watu sita.

UTUKUFU WOTE KWA MUNGU.

USHAURI:

Ndugu wana Jf, mtu anapo leta issue yake tusiwe haraka kutukana na kukejeli. Kuna watu walinitukana kwenye Uzi ule ila Mungu awabariki wote mlio nishauri na sasa ni mzima wa afya.

Mbarikiwe wote.
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom