Mrejesho mwingine wa mke wangu, alirudi ila baadae aliondoka tena

Nakusikitikia sana jamaa yangu! Kwa nini hukuchukua ushauri wangu wa tangu kisha chako cha kwanza? Nilikwambia uachane nae kumbe haukuelewa ukaamua umlete nyumbani tena? Pole sana, wewe umeshakuwa kama toy,anakuchezea kadri anavyotaka, na akitaka kurudi sidhani kama utaonesha tena ugumu au msimamo wako. Hapo ulipo hueleweki,umeleta mada hii tukusaidie katika pembe ipi? Ushauri wangu sasa kwako, mke wako huyo anakitembeza huko kazini kwake, na siku akichoka basi atawaza kukurudia,anakuona kama dustbin tu. Narudia tena,kuwa na msimamo,kama talaka mpatie maisha mengine yasonge. Huwezi kumrudia mwanamke msaliti. Seran ataongezea
 
Ni hasira ndugu...baada ya kunitamkia TUACHANE...niliona ili kupunguza maumivu nimyanganye kila kitu...ndo nitakuwa na amani,,,,maana niliona ninunue nguo zote kwa kujinyima,,halafu aende huko anakoenda Wanaume wengine wamuone amependeza kwa nguo zangu nilizomnunulia?
 
Huyo mwanamke nishajua anachokifanya.
Huyo mwenzako anacheza na akili yako amekugeuza wewe ni kituo cha kuja kupumzikia kama likizo bado anapenda maisha ya ujana hapendi kufungiwa ndani maisha yote na mtu mmoja.
Na anachoringia ni kwamba ameshakusoma na kuujua udhaifu wako kwa hiyo anajua ukifika muda wa kurudi kupumzika anajua jinsi gani ya kucheza na akili yako,kuichota na kurudi muda atakaopenda.
Sasa hivi kaondoka tena na muda wa kurudi kwako bado haujafika akishachoka huko alikoenda atakulaghai tena na kurudi
 
Yeah upo sahihi
 
Mkuu nilitaka kukuuliza kama una akili nzuri kumsamehe kahaba.

Baada ya kuona umepiga chini nikaona akili zako zimerudi.

Achana kabisa na huyo malaya fanya mambo mengine
 
Hapo kwenye nguo amekosea sana na nauli angempa tu, ila sijaelewa kwanini unasema ana haki ya kumsaliti? Mwanamke kama unaona huwezi kutulia na mwanaume mmoja usikubali kuolewa, tulia mtaani tembea hata na dunia nzima nani atakusumbua, ila ukitaka ndoa na umalaya kwa pamoja utapoteza shingo


You cant eat your cake and have it too
 
Hii story ni chai. Hakunaga mwanaume wa hivi.
Wapo wengi sana mzee, nilishashuhudia mwanaume kamfuma mke wake wa ndoa na mchepuko wanakunywa bia, jamaa anaanza mbembeleza mwanamke waende nyumbani na mwanamke ndo kwanza anakua mkali kwanini mume wake anamfatilia, hizi bati zimeficha siri nyingi sana aisee
 
Huyo achana naye. Atakuja kukugharibu zaidi. Kwenye maisha kuna vitu vya kukubali kupoteza na ku-move on
 
Narudia tena,
Mojawapo ya tabia ya ndoa iliyo imara ni kuipambania..pambania ndoa yako.

Mtafute mkeo, mrudie muishi vizuri

Pga moyo konde we ni mwanaume, pambania familia yako, pambana mwamba..(HAUTANIELEWA)

USIJE FANYA KOSA LA KUOA MKE WA PILI KISA UNA HASIRA, HAPO UTAKUWA UMEJICHIMBIA KABURI.
 
Ww na huyo wife wako mmezidi sasa tumechoka😂
 
Ndugu hapo ndo Kuna Mtihani
 
Siku ukiukwaa utakuwa superbh baldaa ya superhb
 
Apambanie kivipi?
Mbona huyo mwanamke hapambanii ndoa irudi stable? Kwanini mnawapa umuhimu hawa watu sana?
 
Mi nimeshachoka kutoa ushauri
 
Apambanie kivipi?
Mbona huyo mwanamke hapambanii ndoa irudi stable? Kwanini mnawapa umuhimu hawa watu sana?
1. Tunatakiwa kuishi nao kwa akili sana, tunatakiwa tujitofautishe nao
-jinsi tunavyowashawishi kulala nao hadi kuzaa nao, inatakiwa tuwe na ushawishi huo huo kuwaleta kwenye ndoa kama wakitoka nje ya mstari
-hatupaswi kutafuta na kutazama mabaya yao tu, siku moja moja tuangalie na wema wao!

2. Kwangu mimi nawapa umhimu kwa sababu ni mhimu kwangu.
-mwanamke aliyenizalia mtoto, huyo kwangu mm ni wa mhimu sana hata kama ana madhaifu ya hapa na pale,
-kuna mambo mwanamke anatakiwa ayafanye hususani katika malezi ya mtoto (mamake na mtoto ni mama tu hata ungeleta wanawake mia kumlea mwanao)
-wengne tumezaliwa na akina mama kwa hyo lazima tuwape umhimu
(wale ambao mama zao wametangulia mbele za haki MUNGU awatie nguvu, jitahidi sana kupalilia na kulifanyia usafi kaburi la marehemu mamako)
 
Mkuu nilitaka kukuuliza kama una akili nzuri kumsamehe kahaba.

Baada ya kuona umepiga chini nikaona akili zako zimerudi.

Achana kabisa na huyo malaya fanya mambo mengine
Mkuu utamlaumu bure tu kwa hatua waliyofikia kumkimbia huyo mwanamke labda ahame nchi akaishi Burundi.
Yaani kinachowaunganisha hapo ni mtoto maana yake hata kama wakigombana mwanamke atapiga simu kujifanya anamuulizia mtoto kisha baadae maongezi yanavyoendelea kunoga wanajikuta wamekumbukana kwenye mambo ya Falagha.
Ni watu wachache sana makauzu wana uwezo wa kuukwepa huo mtego walio wengi hawawezi.
 

Yaani hicho kitendo cha jamaa kumnyanganya nguo na kumnyima nauli, it speak alot about this guy.

Akae atulie afix mambo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…