Mrejesho mwingine wa mke wangu, alirudi ila baadae aliondoka tena

Duh sikusoma mwanzo wa hii story ila aiseee
Jamaa anahitaji washauri na watu wazima wa kumtuliza
Hadi nguo????
Au ni mabrand kwamba hata second hand unauza
Ni nini hii
Nguo??
Duh
 
Wewe ni mtu dhaifu sana,nilikwambia kwenye ule uzi wako ku msaliti hua hasamehewi,msaliti akisha saliti hua harudi nyuma,ni sawa na mtu aliyekua addicted na drugs,

Acha ujinga kaza kama Mwanaume,achana na huyo Mbuzi,Wanawake wapo wengi,ukiendekeza huo ujinga wako utakufa kabla ya siku zako,ukweli mchungu ni kwamba,huyo mkeo unakaziwa mpaka leo hii,

Mwanamke anakwambia kabisa kua hana hisia na wewe ila wewe bado una fikra kua eti labda mtakuja kurudiana huko mbeleni!

Seran unakumbuka kwenye ule uzi nilikwambia kua msaliti hua hasamehewi,na huu ndio mfano halisi.
 
Kwakweli sitakuja kutetea msaliti tena mimi🙌🏾
 
ukiskia "siambiliki wala sishauriki" ndo wew sasa😅😅😅,,, toka uzi wa kwanza watu wanakwambia piga chini ila hausikii kazi yako ni kutuletea "mrejesho",,,

anyway huyo ndo chaguo lako usimuache mpaka ufe kwa msongo wa mawazo
 
ukiskia "siambiliki wala sishauriki" ndo wew sasa😅😅😅,,, toka uzi wa kwanza watu wanakwambia piga chini ila hausikii kazi yako ni kutuletea "mrejesho",,,

anyway huyo ndo chaguo lako usimuache mpaka ufe kwa msongo wa mawazo
Matatizo yote yanayomfika yanasababishwa na udhaifu wake,huyo Mwanamke wake alisha msoma toka kitambo ndio maana akamchezea hivyo,

Angesimama kiume,yote hayo yasingemfika,mleta mada ni mtu dhaifu sana asiyekua na maamuzi ya kiume.
 
Matatizo yote yanayomfika yanasababishwa na udhaifu wake,huyo Mwanamke wake alisha msoma toka kitambo ndio maana akamchezea hivyo,

Angesimama kiume,yote hayo yasingemfika,mleta mada ni mtu dhaifu sana asiyekua na maamuzi ya kiume.
tatizo ni mapenzi Ice🤣🤣 sijui anapewa nini na huyo binti,, istoshe mpka kuandika huu uzi ni anaonesha ni kias gani bado anampenda na kashammis tayali,,

mleta mada hajiwezi yuko hoi, kafa kaoza kabisa😅👌,, sema namuonea huruma😢😢 anafanya haya yote ili apate amani ya moyo ila kumuacha huyo binti sio leo
 
Asante kwa taarifa yako.Ni hivi hii ndoa yenu ilishajaribika kiasi nacho hairekebishiki na juhudi zote mlizofanya kuirekebisja hazikufua dafu,hivyo kuivunja ndoa hii ina baraka zote za Mungu.Kika mmoja asnze upya kwdnye maisha na mtampa mtu anayewafaa.
 
Ndoa sio kwa watu msiojielewa kama nyinyi..
Una utoto mwingi halafu una ushamba wa mahusiano, inaonekana kwa demu hujiwezi, na hata sasa akija akalegeza jicho utamsamehe,

Sio ndoa tu, kiujumla mapenzi kwa wanaume, sio kwa wenye mioyo dhaifu kama wewe na msiokuwa na maamuzi ya kiume.
Wewe unajali hisia kuliko akili,

Achana na mapenzi PIGA NYETO
 
Mwanamke akishaondoka kisha akarudi na kuondoka tena huwa harudi tena, huko hupata maambukizi ya magonjwa na kurudi kuugulia kwa mume wa kwanza huwa ngumu. Mwanaume unapaswa utulize kichwa kabla ya kuoa tena. Ukioa harakaharaka unaweza kupata mke pasua kichwa kuliko wa mwanzo! Fanya uchunguzi taratibu kupata mke mpya atakayekidhi sifa bora kuliko wa mwanzo
 
Kumrudisha mtu aliyekusaliti kwa kutembea na mwanaume mwingine, BIG MISTAKE!!

Kumfukuza mke wako na kumnyang'anya nguo, what for?
 
Mwanamke akishafanya kosa la usaliti, the only solution ni kumuacha. Huwezi kupambania ndoa na msaliti mkuu.
 
Pole sana mkuuu ni changamoto kwenye ndoa na hazikosekani tunaona sana uko na uko ata hapa pia jukwaani.

Usisite kuoa tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…