MREJESHO: Nimeendesha Uber na Taxify kwa gari yangu ndani ya miezi mitatu

MREJESHO: Nimeendesha Uber na Taxify kwa gari yangu ndani ya miezi mitatu

Yeah nilikutana na mmoja kama week 3 zimepita. Alinibeba East 24. Alinipa huduma nzuri nikampa nyota zote 5 na kombe.
Nilianza process za kujiunga ila shemeji yako akawa ananisisitiza juu ya heshima ya wateja,udhalilishaji wa kijinsia na gender related issues

Nikarudi chini kujitafakari upya.Bado sijapata maamuzi sahihi.
 
Hiyo ni sawa na 1.8M mwisho wa mwezi bado anaona ndogo. Kuna watu wanapata 1/3 ya hiyo na wanapush life kama kawaida.
In life of money the only thing separates the have and the dont have is how they manage their money.

Jamaa huwenda money management inamsumbua.
 
Nilianza process za kujiunga ila shemeji yako akawa ananisisitiza juu ya heshima ya wateja,udhalilishaji wa kijinsia na gender related issues

Nikarudi chini kujitafakari upya.Bado sijapata maamuzi sahihi.
Kwani na driver si huwa wanarate wateja? Vitu vingine ni kazi kuzia lakin. Akili kumkichwa hapo.
 
Hahaaa mkuu umenikumbusha siku nimepewa hela nikaoshe gari
Nikaamua tu nioshe mwenyewe jamaa akanikuta nikamwambia nafanya mazoezi. Mara moja moja siyo mbaya.
Nami umenikumbusha mbali sana, kulikuwa na kamkweche pick-up, kakiharibika vitu vidogo vidogo kama ni cross-joint, bushes, tie rod ends, ball joints au distributor n.k. kwanza najifanya naenda kwa fundi, kumbe chini ya mwembe mbali na home, najifua mwenyewe, mkwanja kwenye wallet! Hatari sana...
 
Kwani na driver si huwa wanarate wateja? Vitu vingine ni kazi kuzia lakin. Akili kumkichwa hapo.

Sure. Wote mnapeana rates.
Dereva rates zikishuka chini ya 4.4 kwa Uber (kama sio 4.6) wana deactivate account yako na unatakiwa uende kuchukua mafunzo tena.

Abiria pia akishuka rate fulani account yake inafungiwa.

NANI ANA HASARA?

Abiria ndani ya dakika 5 anafungua email nyingine na anasajili Uber nyingine kwa namba nyingine ya simu. Ila wewe dereva lazima uende makao makuu wakupangie siku ya mafunzo.
 
Nilianza process za kujiunga ila shemeji yako akawa ananisisitiza juu ya heshima ya wateja,udhalilishaji wa kijinsia na gender related issues

Nikarudi chini kujitafakari upya.Bado sijapata maamuzi sahihi.

Kwa mwanamke sikushauri ile kazi. Labda iwe ndio kazi pekee kwa kupatia kipato. Ila kama una kazi nyingine iyo unataka iwe inakusaidia elfu 10 kwa siku ya mafuta, BIG NO.

Mimi hapa wifi/shemeji yenu alikua hajui. Nikawa nafanya kisiri siri. Nilishawahi kumgusia alikataa sana.
 
MI nadhani kama biashara inakupa walau ka hela kakukidhi mahitaji madogo Sio mbaya as long as Huibi cha mtu ila kama ingekua Hyo biashara haina Faida yoyote yani work done equal to Zero kidogo hapo ningesema kitu.

Hamna biashara yenye Faida asilimia 100 NA NDIO MANA ikaitwa biashara mi nadhani mkUuu una majukumu Mengi kwa sasa ndio maana umeona UBER haina faida kwako ila nahisi ungekua huna MAjukumu makubwa kiasi hicho UBER usingeipondea.

Tatzo ni majukumu na umeshasema ulikua unafanya kama Part time ina mana ulikua na kazi yako binafsi inayokupa Kula na kuya mudu maisha,kitu kinachofanya akili yako iwaze zaidi kule kwingine.

ACHA ILE BIASHARA ULOKUA UNAFANYA THEN RUDI FANYA UBER ktk u serious na UICHUKULIE KAMA AJIRA YAKO TUONE KAMA COMMENT ZAKO ZITABAKI HIVI HIVI nadhani lazima utarudi na THREAD YA KUPONGEZA ZAIDI NA KUSHAWISHI WATU WAENDE.

biashara ni RISK ni Lazima TUKUBALI.
 
Back
Top Bottom