Wakuu habari.
Kama kichwa kinavyojieleza hapo naomba nilete experience yangu ya kua Uber/Taxify Driver kwa kutumia gari binafsi.
Gari ni cc1500 Corolla, na niliifanya kama part-time job sio full time. Mara nyingi nilikua naendesha Kuanzia Ijumaa to Jumapili, saa 2 usiku hadi saa 12 Asubuhi. Ingawa sio kila weekends but Most of them. Na nimefanya kwa muda wa kama miezi mitatu, Tokea mwaka jana November /December. Na nilikua na Apps zote mbili, Uber na Taxify.
Kwa siku faida nikitoa mafuta na kula mimi, nilikua na save kati ya 60,000 hadi 100,000 mambo yakiwa mazuri. Hapo ikiwemo ile hela ya kamisheni (25% kwa Uber) nnayotakiwa ipeleka kwa Uber. Mi sijawahi kuwapa kusema kweli.
Guys hii biashara ni kuzeesha gari, kujichosha, stress za kuwaza ratings na faida ni kwaajili ya kupata hela ya kuspend tu siku 2 au 3 .
Kwamaana hako ka faida ulikokapata kesho utataka ukasafishe gari (20,000 Car Wash), ununue marashi mazuri ya kwenye gari kuwavutia wateja wakupe high ratings, ununue MB za kutosha maana muda wote laziwa uwe online so unakuta unabakiwa na hela ya chakula tu.
Kwa muda huo wa masaa 10 niliopo online muda mwingi, karibia masaa 7, nakua gari inatembea tu. Hapo milage zinaongezeka sana na gari inachakaa sana ukichukulia Watanzania wengi hatukai sehemu rafiki, ila mabondeni sana ambako ukipeleka gari lolote linaweza kutokea. Mfano, nimeshachana Bumper na kusababisha gharama kulitengeneza na kupaka rangi ya Tsh 180,000.
Usiku unakuta wateja ni madogo walevi, miguu juu ya viti na maviatu yao machafu, gari inanuka pombe, hafu wanakutreat cheap sana, yaani kisa wanatoa hela basi ni Kero.
Pia Uber maximum ni watu wanne, sasa unakuta kila trip wewe unapakiza watu 3 to wa 4. Gari inakula sana mzigo. Unaichosha sana na wanakaa maporini huko Kimara mabondeni.
Kwa hitimisho, sio biashara mbaya ila ukiwa na gari dedicated kwa hii biashara na sio gari binafsi. Pia, mitaa yako iwe Posta, na uzunguni ambapo pings zinakua nyingi so muda wa kuzurura bila abiria unakua mdogo na kazi iwe full time (uwe na dereva wako), na gari zuri liwe na cc ndogo 1300 IST na vitz, PASSO na nyingine za cc990 ni nzuri.
Ila kwa upande wangu, hii kitu sio kwaajili ya barabara za Tanzania. Inakula sana kwa dereva.